mkulima gwakikolo
JF-Expert Member
- Nov 22, 2014
- 1,767
- 2,851
Ukweli ni kwamba siku atakapofikishwa kizimbani mtaona atakavyoshambuliwA na wananchi. SERIKALI ITAPIMA UPEPO UTAKAVYOKUA..KAMA ITAONA WATU WENGI WANAMWELEKEO KWAMBA JAMAA AFUNGWE BASI, kesi haitafutw ili kukidhi haja ya wananchi. Kumbukeni Sirikali ikishakutumia kukutupa jalalani pia ni rahisi. Hvyo Hii kesi ni fifty fifty. Subilini!!Katiba ya Tanzania hairuhusu Makonda kushtakiwa kwa sababu ili ufanikiwe kumshtaki Makonda lazima serikali iridhie/ikubali/ipitishe mashtaka hayo kupitia DPP.
Hii maana yake ni kwamba kama serikali haitaki umshtaki Makonda basi hutaweza kumshtaki makonda hata kama alifanya makosa ya wazi na makubwa kiasi gani.Maana yake serikali imehodhi haki za watu.
Kama Serikali ilikuwa haitaki Sabaya ashtakiwe basi hadi leo Sabaya angekuwa uraiani.Aliemshtaki na kumfunga Sabaya ni Serikali na siyo mtu mwingine yoyote yule.Kama siyo Serikali hapakuwa na wa kumshtaki wala kumgusa Sabaya.
Lakini baya zaidi ni kwamba Serikali ina uwezo wa kumshtaki yoyote yule na kumweka ndani bila dhamana(kwa makosa yasiyo na dhamana) hata kama mtu huyo hajatenda makosa haya na hakuna ambae anaweza kuizuia serikali katika hilo.
Nafikiri sasa unaweza kuona ni kwa nini tunahitaji katiba mpya.