Raia Mwema: Makonda Kibarua kizito, wengine wajitokeza kumshitaki

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,937
25,279
makonda.png

Gazeti la Raia Mwema limeripoti kuwa watu wengine wamejitokeza kumshitaki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mfanyabiashara mmoja amenukuliwa na gazeti hilo akisema "Makonda ametufanyia mambo mengi kinyume na sheria za nchi.

Kuna wakati baadhi yetu, tulijaribu kumshitaki, lakini tukatishwa na baadhi ya waliojitambulisha kuwa maofisa wa Serikali hivyo tukalazimika kurudi nyuma"
 
Mengi yapo nyuma ya pazia kuhusu mtu huyu!
  1. Waiiodhulumiwa na kuporwa mali zao kwa kisingizio cha 'madawa ya kulevya' huyu mtu alitumia sana mwanya ule!
  2. Walioporwa fedha zao wakati wa operation chafu ya Bureau de change Huyu mtu alifanya mambo yake yaleyale!.
 
Gazeti linatafuta kiki na wanajua kichwa Cha hbari kitauza gazeti.
 
Katiba ya Tanzania hairuhusu Makonda kushtakiwa kwa sababu ili ufanikiwe kumshtaki Makonda lazima serikali iridhie/ikubali/ipitishe mashtaka hayo kupitia DPP.

Hii maana yake ni kwamba kama serikali haitaki umshtaki Makonda basi hutaweza kumshtaki makonda hata kama alifanya makosa ya wazi na makubwa kiasi gani.Maana yake serikali imehodhi haki za watu.

Kama Serikali ilikuwa haitaki Sabaya ashtakiwe basi hadi leo Sabaya angekuwa uraiani.Aliemshtaki na kumfunga Sabaya ni Serikali na siyo mtu mwingine yoyote yule.Kama siyo Serikali hapakuwa na wa kumshtaki wala kumgusa Sabaya.

Lakini baya zaidi ni kwamba Serikali ina uwezo wa kumshtaki yoyote yule na kumweka ndani bila dhamana(kwa makosa yasiyo na dhamana) hata kama mtu huyo hajatenda makosa haya na hakuna ambae anaweza kuizuia serikali katika hilo.

Nafikiri sasa unaweza kuona ni kwa nini tunahitaji katiba mpya.
 
Hilo gazeti linatafuta kiki sana. Hakuna chochote atakachofanywa makonda
 
View attachment 2031158

Gazeti la Raia Mwema limeripoti kuwa watu wengine wamejitokeza kumshitaki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Mfanyabiashara mmoja amenukuliwa na gazeti hilo akisema "Makonda ametufanyia mambo mengi kinyume na sheria za nchi. Kuna wakati baadhi yetu, tulijaribu kumshitaki, lakini tukatishwa na baadhi ya waliojitambulisha kuwa maofisa wa Serikali hivyo tukalazimika kurudi nyuma"
Mkija na uongo kwamba mlimhonga mjue kuhonga ni jinai itabidi na nyie mjibu mashitaka. Msifikiri sasa kuna serikali inaruhusu kutoa rushwa.
 
Katiba ya Tanzania hairuhusu Makonda kushtakiwa kwa sababu ili ufanikiwe kumshtaki Makonda lazima serikali iridhie/ikubali/ipitishe mashtaka hayo kupitia DPP.

Hii maana yake ni kwamba kama serikali haitaki umshtaki Makonda basi hutaweza kumshtaki makonda hata kama alifanya makosa ya wazi na makubwa kiasi gani.Maana yake serikali imehodhi haki za watu.

Kama Serikali ilikuwa haitaki Sabaya ashtakiwe basi hadi leo Sabaya angekuwa uraiani.Aliemshtaki na kumfunga Sabaya ni Serikali na siyo mtu mwingine yoyote yule.Kama siyo Serikali hapakuwa na wa kumshtaki wala kumgusa Sabaya.

Lakini baya zaidi ni kwamba Serikali ina uwezo wa kumshtaki yoyote yule na kumweka ndani bila dhamana(kwa makosa yasiyo na dhamana) hata kama mtu huyo hajatenda makosa haya na hakuna ambae anaweza kuizuia serikali katika hilo.

Nafikiri sasa unaweza kuona ni kwa nini tunahitaji katiba mpya.
Ulivyojibia hoja nami mambo mengi ninaafiki ILA kwa sababu JF kuna wengi wenye utaalamu tofauti let's tuwaombe wanasheria watusaidie hili la to privately prosecute someone or company etc etc,hebu tusome POA ya 1985 section 6(1)na section 6 (A)also 1985.pls lawyer's help .
 
Ngoja naye asulubiwe, alifanya undava bila kusoma nyakati zijazo ataishije kisiasa. Vijana wawe makini sana wapatapo madaraka makubwa waache siasa za ulimbukeni
 
Ulivyojibia hoja nami mambo mengi ninaafiki ILA kwa sababu JF kuna wengi wenye utaalamu tofauti let's tuwaombe wanasheria watusaidie hili la to privately prosecute someone or company etc etc,hebu tusome POA ya 1985 section 6(1)na section 6 (A)also 1985.pls lawyer's help .
Hata mimi japo ndiye nilieandika hapo ila nina mashaka na nilichoandika.
 
Katiba ya Tanzania hairuhusu Makonda kushtakiwa kwa sababu ili ufanikiwe kumshtaki Makonda lazima serikali iridhie/ikubali/ipitishe mashtaka hayo kupitia DPP.

Hii maana yake ni kwamba kama serikali haitaki umshtaki Makonda basi hutaweza kumshtaki makonda hata kama alifanya makosa ya wazi na makubwa kiasi gani.Maana yake serikali imehodhi haki za watu.

Kama Serikali ilikuwa haitaki Sabaya ashtakiwe basi hadi leo Sabaya angekuwa uraiani.Aliemshtaki na kumfunga Sabaya ni Serikali na siyo mtu mwingine yoyote yule.Kama siyo Serikali hapakuwa na wa kumshtaki wala kumgusa Sabaya.

Lakini baya zaidi ni kwamba Serikali ina uwezo wa kumshtaki yoyote yule na kumweka ndani bila dhamana(kwa makosa yasiyo na dhamana) hata kama mtu huyo hajatenda makosa haya na hakuna ambae anaweza kuizuia serikali katika hilo.

Nafikiri sasa unaweza kuona ni kwa nini tunahitaji katiba mpya.

Ni kweli. Lakini hiyo ipo kwenye makosa ya jinai. Kwenye madai, mtu yeyote ana haki ya kumshtaki yeyote, na DPP hahusiki. Mathalani watu waliochafuliwa majina yao kuwa wanafanya biashara ya madawa ya kulevya, wanaweza kumshtaki Makonda kutaka fidia, kama alivyofanya Membe kwa Musiba. Mathalani kukawa na watu walioteswa kwa amri ya Makonda, wanaweza kumshtaki Makonda. Wapo waliodhalilishwa, mathalani kwa kupitia operesheni yake ya masuala ya ndoa, wana uwezo wa kumshtaki Makonda.
 
Ni kweli. Lakini hiyo ipo kwenye majosa ya jinai. Kwenye madai, mtunyeyote ana haki ya kumshtaki yeyote, na DPP hahusiki. Mathalani watu waliochafuliwa majina yao kuwa wanafanya biashara ya madawa ya kulevya, wanaweza kumshtaki Makonda kutaka fidia, kama alivyofanya Membe kwa Musiba. Mathalani kukawa na watu walioteswa kwa amri ya Makonda, wanaweza kumshtaki Makonda. Wapo waliodhalilishwa, mathalani kwa kuoitia operesheni yake ya masuala ya ndoa, wana uwezo wa kumshtaki Makonda.
Hivi mkuu kuchafua jina la mtu,kutesa watu na kudhalilisha watu siyo jinai?
 
Mengi yapo nyuma ya pazia kuhusu mtu huyu!
  1. Waiiodhulumiwa na kuporwa mali zao kwa kisingizio cha 'madawa ya kulevya' huyu mtu alitumia sana mwanya ule!
  2. Walioporwa fedha zao wakati wa operation chafu ya Bureau de change Huyu mtu alifanya mambo yake yaleyale!.
Huyu ndiyo anatakiwa apigwe uhujumu uchumi
 
Hivi mkuu kuchafua jina la mtu,kutesa watu na kudhalilisha watu siyo jinai?
Kuna jinai na madai.

Kwa makosa hayo, serikali kwa kupitia DPP inaweza kumshtaki kwa kuwa ni jinai.

Aliyetendewa makosa hayo anaweza kufungua kesi ya madai ya kutaka kulipwa fidia kwa kuharibiwa heshima, kusababishiwa maumivu na kutiwa hasara (kama zipo).

Kama DPP hataki kumfungulia kesi ya jinai, wewe uliyetendewa huzuiwi kumfungulia kesi ya madai.
 
Back
Top Bottom