Raia Mwema latishiwa kushitakiwa na Lowassa

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Kuna taarifa kwamba gazeti la Raia Mwema limeandikiwa barua ya kutishwa na mtoto wa Edward Lowassa, wakitakiwa kuomba radhi kwa habari yao vinginevyo watashitakiwa kwa kumkashifu kijana huyo na baba yake Edward Lowassa.

Taarifa ya Lowassa kuchunguzwa balaa


Mwandishi Wetu
Disemba 1, 2010

  • Raia Mwema lapata msukosuko
  • Nakala 10,000 zaharibiwa zisisomwe

HABARI iliyoihusisha familia ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, imeibua utata mkubwa baada ya kuibuka kwa vitisho vilivyosababisha kuzuiwa kuchapwa kwa gazeti la Raia Mwema toleo lililopita Namba 161 katika mazingira ya kutatanisha; huku habari hiyo ikikanushwa kwenye gazeti jingine hata kabla haijatoka.

Utata huo ulisababisha uongozi wa Imprint iliyopo chini ya kampuni ya Jamana Printers kusitisha ghafla kuendelea kuchapwa kwa gazeti la Raia Mwema ikiwa tayari limeshachapwa nakala 10,000 katika mazingira yaliyoonyesha kuwapo shinikizo zito kutoka kwa kigogo mmoja aliye karibu na mwanasiasa huyo la kutaka habari inayomhusu Lowassa iondolewe ndipo gazeti lichapwe.

Raia Mwema ambalo lina makubaliano maalumu na wachapaji hao lilishtushwa na uamuzi huo wa ghafla wa wachapaji hao hasa baada ya uamuzi huo kuambatana na hali ya woga mkubwa uliotawala wafanyakazi wa kiwanda hicho usiku wa Jumanne ya wiki iliyopita.

Taarifa ya Meneja Usambazaji wa Raia Mwema, Omari Mwendapole, ambaye alikuwapo usiku huo, inaeleza kwamba hali ya uchapaji iliendelea katika hali ya kawaida kuanzia saa 11 jioni kabla ya kubadilika ghafla saa 1:30 usiku, ilipotolewa amri ya kusitisha uchapaji wakati zikiwa zimekwishachapwa nakala 10,000.

"Tulifika kiwandani mapema saa 11:00 na hakukua tatizo lolote baada ya wahusika kukagua gazeti letu na kuridhika nalo na wakaanza taratibu
zote ikiwa ni pamoja na kuchoma plate saa 11:15 na saa 12:00 kazi ya uchapaji ilianza taratibu hadi saa 12:30 mashine zilipoanza kuchanganya na kutoa gazeti zuri.

"Lakini baada ya muda kidogo, msimamizi wa uchapaji wa Imprint akaitwa na mlinzi kwenda kusikiliza simu na aliporejea akawaagiza mafundi wazime mashine kabla ya kuamua kuzima mwenyewe baada ya kuona wanachelewa kufanya hivyo.

"Baadaye niliitwa kwa bosi wao na kuambiwa natakiwa kwenda kwa Meneja Mkuu, aitwaye Shaber, ambako nilijulishwa kwamba ni lazima habari kuu (inayomhusu Lowassa) iondolewe vinginevyo gazeti halitochapwa kabisa," anasema Mwendapole.

Kutokana na amri hiyo ya wachapaji, wafanyakazi wote wa Raia Mwema na watu wengine wote waliokuwamo kiwandani wakati huo waliamriwa kutoka eneo la uchapaji na kupekuliwa kuhakikisha hawabebi hata nakala moja ya gazeti hilo.

Habari zinasema kuwa nakala 10,000 ambazo tayari zilishachapwa ziliharibiwa chini ya uangalizi mkali wa maofisa wa kiwanda hicho ili kuhakikisha kuwa haziingii kwenye soko, na hivyo habari hiyo kusomwa na wananchi.

Hata hivyo, wakati uongozi wa Raia Mwema ukihangaika kutafuta mahali pengine pa kuchapa, ilibainika kwamba kigogo huyo pamoja na mbunge mmoja walikuwa tayari na nakala ya gazeti hilo na ilidhihirika siku iliyofuata baada ya gazeti la Mtanzania lenye uhusiano wa karibu na kigogo huyo kuchapisha habari iliyokanusha habari hizo kabla hata ya habari husika kuchapishwa.

Katika habari hiyo, gazeti hilo lilielezea kwamba kuna taarifa "zilizochapwa katika magazeti" huku zikimnukuu Frederick Lowassa, ambaye ndiye aliyekuwa mhusika mkuu katika habari ya Raia Mwema, akijitetea kwa kudai kwamba hakuwahi kusafirisha fedha nyingine Uingereza kama ilivyoandikwa na ‘magazeti hayo.'

Katika tukio hilo la aina yake katika tasnia ya habari, Frederick Lowassa, alisema;

"Jamani mimi nashangaa sana. Watu hawa wanasahau kuwa mimi ni mfanyabiashara kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Na katika kufanya biashara ni lazima nisafirishe fedha nje ya nchi kwa nia ya kununua material (bidhaa). Nasafirisha fedha sehemu mbalimbali duniani, na sijui wameliokota wapi hilo.

"Hakuna wakati nimewahi kusafirisha paundi 495,000 nje ya nchi kwa mara moja, ila nasafirisha fedha nje ya nchi kununua bidhaa mara nyingi tu. Hili wanalozungumza la Uingereza ni kweli kati ya Machi na Aprili nilisafirisha kama Paundi chini ya 200,000 hivi, kwa ajili ya biashara kama kawaida. Benki kama kawaida walijiridhisha fedha hizo zilikotoka, tukawasiliana likaisha.

"Sasa nashangaa watu hawa hili wamelitoa wapi? Na ifahamike kuwa mimi nafanya biashara nyingi tu, na moja ya biashara zangu ni kampuni ya Alphatel. Sisi ni mawakala wa Vodacom. Tunover (mzunguko wa fedha) yetu kwa mwezi ni zaidi ya Sh bilioni 8.0. Hizi ni fedha zinazotumiwa kama sehemu ya mtaji na faida kwa kununua bidhaa na kuuza. Sasa walitarajia mfanyabiashara kama mimi nishindwe kutumia kiasi hicho nje ya nchi? Nanunua vitu kutoka Uingereza, China, Falme za Kiarabu (Dubai), Afrika Kusini, Italia na sehemu nyingine. Watu wa ajabu kweli hawa.

"Nasikitika jinsi wanavyoendelea kumchafua mzee wangu. Na ndio maana nimeelewa barua hiyo ya mwaka jana imeletwa leo wiki hii. Tayari nimewasiliana na mwanasheria wangu katika hili na nitatoa vielelezo vyote, hakuna cha kuficha…. Jamani siasa zao wazibakize huko, kazi waliyofanya kumchafua mzee wangu (Lowassa) hawajaridhika kweli? Katika hili nasema hapana."

Habari hiyo ilifuatiwa na habari nyingine ambayo iliyomnukuu Lowassa mwenyewe akionyesha kwamba Lowassa anaandamwa na katika toleo hilo aligusia tena kuhusu mwanae Fredrick kuchukua hatua za kisheria kuhuhusiana na habari inayohusiana na usafirishaji fedha Uingereza. Habari hiyo imenukuliwa tena katika gazeti lingine jana.

Uongozi wa Raia Mwema tayari umeiandikia barua kampuni hiyo ya uchapaji ukilalamikia tukio hilo la kuzuia gazeti lisichapwe na kuharibu nakala ambazo tayari zilishachapwa, na pia kutoa usiku huo huo baadhi ya nakala za toleo hilo kwa watu wa nje bila idhini ya wamiliki wa gazeti. Pia unataka ulipwe fidia kwa hasara iliyopatikana kwani ililazimu gazeti kuchapwa kwingineko alfajiri, na hivyo kuchelewa kuingia sokoni.

Katika habari yake ya wiki iliyopita iliyoibua mambo yote hayo, Raia Mwema liliripoti kwamba Frederick Lowassa anachunguzwa na Kitengo Maalumu cha Polisi wa Kimataifa wa Uingereza wanaofuatilia utata wa uhamishaji fedha kutoka Tanzania.

Fedha hizo zinahusishwa na ununuzi wa nyumba yenye thamani ya pauni za Uingereza 475,000 (takriban Shilingi bilioni moja) katikati ya Jiji la London.

Hata hivyo, watu walio karibu na Frederick wameelezea kwamba kijana huyo hakuwahi kununua nyumba; bali aliwahi kutaka kupanga kwa ajili ya kuishi akiwa masomoni nchini Uingereza na fedha nyingine alizituma kwa ndugu yake aishie nchini humo.

Nyumba ambayo inatajwa katika maelezo ya awali iko mtaa wa Leinster Gardens, jijini London.

Hata hivyo, hakuna ofisa yeyote wa Serikali ya Tanzania aliyekuwa tayari kuzungumzia suala hilo, pamoja na kuwapo taarifa kwamba tayari vyombo vya dola vya Tanzania vimekwisha kuhusishwa katika uchunguzi huo.

Maofisa wa Polisi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (CID) wanaohusika na uchunguzi wa fedha haramu, wamekwepa kuzungumzia suala hilo na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, hakuweza kupatikana, na alielezwa kuwa nje ya nchi kikazi.

Ofisa wa CID aliyeelezwa kuongoza kitengo kinachochunguza makosa ya uhalifu wa fedha na nyaraka, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Samson Kasala, alikanusha kufahamu chochote kuhusiana na suala hilo, kabla ya kukata simu alipohojiwa na Raia Mwema kuhusu taarifa hizo.

Taarifa zinaeleza kwamba Kitengo cha Ufuatiliaji wa Fedha Haramu (Financial Intelligence Unit-FIU) kilichopo chini ya Wizara ya Fedha nchini, kilipokea taarifa kutoka Polisi wa Kimataifa wa London, Uingereza, wakitaka taarifa muhimu kuhusiana na Frederick, kabla ya kitengo hicho kuomba msaada wa polisi.

Hata hivyo, Kamishna wa FIU, Herman Kessy, hakutoa ushirikiano na Raia Mwema, kuhusiana na sakata hilo.

FIU imeanzishwa chini ya Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu ya mwaka 2006 (Anti-Money Laundering Act-2006) kwa kuundiwa kanuni mwaka 2007, lakini hadi sasa kitengo hicho kimekuwa kikiendeshwa na maofisa watano tu, Kamishna Kessy, mchambuzi mmoja, mtaalamu wa mawasiliano na wasaidizi wawili wasio wataalamu, kitengo kilichopaswa kuendeshwa na watu wengi zaidi kutokana na unyeti wake.

Habari zinaeleza kwamba hata ofisa wa Polisi aliyewahi kuhamishiwa FIU kwa kazi maalumu alijikuta akitengwa na kutopangiwa kazi na maofisa hao ambao wengi wanatoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), baada ya kuwa ‘wameaminiwa' sana na uongozi wa juu wa serikali.

Kwa mujibu wa taarifa hizo ambazo bado zinafanyiwa kazi, Frederick ambaye baba yake alijiuzulu Waziri Mkuu kwa kuhusishwa na kashfa ya ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme iliyokabidhiwa kwa kampuni tata ya Richmond Development LLC, anadaiwa kufanya mawasiliano kupitia kampuni ya uwakala iliyotajwa kwa jina la ‘Mishcon'.

Nyaraka alizowasilisha, zilidai kuwapo ubia kati ya mtuhumiwa huyo na kampuni tatu ikiwamo Integrated Property Investment(T) Ltd na Barare Ltd Company.

Mkataba huo unaonyesha kuwa Frederick Lowassa ana hisa kwenye kampuni hizo, na kwamba fedha za ununuzi wa nyumba hizo zinatokana na fedha za malipo ya hisa anazopata kutokana na kampuni hizo.

Hata hivyo, mkataba huo unaonyesha kusainiwa Machi 25 mwaka 2009 siku moja baada ya Frederick Lowassa kusaini mkataba kati yake na kampuni ya Mishcon kama wakala wake katika ununuzi wa jengo hilo.

Pia aliwasilisha nyaraka zinazoihusisha kampuni ya Alphatel kama moja ya kampuni ambayo pia yeye ni mkurugenzi wake ambayo pia ni chanzo chake kingine cha fedha anazotumia kununua jengo hilo.

Taarifa zimedokeza kuwa ununuzi huo ulikwama baada ya kushindwa kutoa malipo hayo kwa mujibu wa mkataba kati yake na wakala wa ununuzi wa nyumba hiyo (kampuni ya Mishcon) ambao ulimtaka awe amekamilisha kulipa fedha hizo kabla ya Aprili 14, mwaka 2009.

Hata hivyo, siku chache baadaye ndani ya mwezi huo wa Aprili, Frederick aliipelekea Mishcon kiasi cha pauni za Uingereza 199,940 zikitokea kwenye kampuni ya ununuzi fedha ya Wall Street Exchange.

Aidha kiasi cha pauni 100,000 kiliingizwa kwenye akaunti ya kampuni hiyo hiyo ya Mishcon kwa fedha taslimu katika mikupuo 12 tofauti zikitokea kwenye matawi tofauti ya benki ya NatWest Bank plc iliyoko Kaskazini mwa Jiji la London.

Raia Mwema limeelezwa kuwa mazingira ya kuingizwa fedha hizo kwenye akaunti ya wakala huyo ( Mishcon) ndiyo yameifanya Taasisi ya SCD 6 Economics and Specialist Proceeds of Corruption Unit ya Uingereza inayosimamia uchunguzi wa sakata hilo kuwa na mashaka makubwa kuhusu uhalali wa fedha hizo.

Kutokana na mazingira hayo, SCD 6 Economic and Specialist Crime Proceeds of Corruption Unit yenye ofisi zake Victoria Block, New Scotland Yard, London, ililazimika kuwasiliana na FIU ikitaka maelezo ya awali kuwezesha kufanyika kwa uchunguzi kuhusu fedha hizo.

Raia Mwema iliwasiliana na Fred ambaye alikana kununua nyumba Uingereza lakini alikiri kuwahi kutuma fedha huko. Aliliambia Raia Mwema pia kwamba hajawahi kuhojiwa na yeyote kuhusu suala hilo, na pia kwamba hana taarifa kuwa polisi wa Uingereza wanampeleleza.

Hata hivyo kwa upande mwingine, gazeti hili limebaini kuwa, maelezo ya awali ambayo yalitakiwa kutoka Tanzania na makachero hao wa Uingereza, ni pamoja na kutaka kufahamu kama kweli Frederick Edward Lowassa amezaliwa Agosti 26, 1977, Mwanza Tanzania na anamiliki hati ya kusafiria yenye namba AB 109402 iliyotolewa Tanzania na kwamba anwani yake nchini Uingereza ni 71 Hendrix Drive, Milton Keynes, MK8 0DY.

Pia makachero hao waliitaka Serikali ya Tanzania kutoa ufafanuzi wakitaka kujua kama Frederick Lowassa ni mbia katika kampuni za Alphatel Partnership (Tanzania) Barare Ltd na Intergrated Tanzania Limited, kampuni ambazo zimefahamika kumilikiwa na familia ya Lowassa.

Asasi hiyo ya Uingereza pia imeomba kujua kama FIU wana taarifa zozote za uhalifu dhidi ya Frederick Lowassa na kama baba yake Edward Lowassa anachunguzwa kwa tuhuma yoyote ya rushwa na mamlaka za uchunguzi wa rushwa nchini Tanzania kuhusu fedha haramu.

Uchunguzi wa awali uliofanywa na vyombo vya dola, ulielezwa na taarifa hizo kwamba Frederick Lowassa si mbia katika kampuni hizo na kwamba Barare Ltd wenye hisa ni Edward Ngoyai Lowassa mwenye hisa 500 na Regina Mumba Lowassa mwenye hisa 500 huku wakurugenzi wakiwa ni hao hao.

Ofisa wa Uingereza anayesimamia uchunguzi huo, George Simpson, ameliambia Raia Mwema kupitia barua pepe kwamba kanuni za uchunguzi kuhusiana na kesi zenye mguso wa kisiasa huwazuia kukanusha au kuthibitisha kuhusu uchunguzi unaoendelea hadi pale wanapofikia hatua ya kukamata mtuhumiwa ama anapofikishwa mahakamani.

Taarifa ambazo gazeti hili limezipata mwanzoni mwa wiki hii kutoka vyanzo vyake zinasema kwamba uchunguzi wa suala hilo bado unaendelea, na kwamba watendaji wamepewa maelekezo ya kuendelea nao.



Taarifa ya Lowassa kuchunguzwa balaa
 
Ni kweli wakili Fungamtama ndiye aliyewapelekea barua ya kusudio la kushitaki akitaka aombwe radhi, lakini barua yanyewe naambiwa imeandikwa kwa lengo la KUWAFUNGA MDOMO Raia Mwema wasiendelee na hiyo habari na wengine wasiiendeleze, kwa kifupi ni kuiua kabisa.
 
Hii ni mbinu ya vitisho sasa hivi hiyo mafia canibals haina njia nyingine zaidi ya hiyo,kinachotakiwea ni vyombo vya habari kuizingira hiyo camp...they will loose
 
Vitisho vingekuwa ni assassination, wapenda haki wengi tu Tanzania tungekuwa tushawazika. Watatisha hutasikia wameenda mahakamani.
 
Kuna taarifa kwamba gazeti la Raia Mwema limeandikiwa barua ya kutishwa na mtoto wa Edward Lowassa, wakitakiwa kuomba radhi kwa habari yao vinginevyo watashitakiwa kwa kumkashifu kijana huyo na baba yake Edward Lowassa.


Kama wanaushahidi tatizo nini? Mara zote huwa napenda kesi zifike mahakamani na huko mambo mengi yanawekwa adharani.

Mwandishi kama anafuata maadili ya kazi yake hawezi kutishiwa nyau!
 
Mimi siamini katika kutegana.Je wakiomba msamaha kwa maandishi then wakayatumia kama ushahidi kuomba fidia kubwa?Lowasa na familia fungueni kesi mkutane huko huko tuujue ukweli maana kuna madudu kibao huko yamejificha tuyajue
 
Jamani naomba kama Wanauthubutu hata chembe wampeleke raia mwema mahakamani. Hapo ndio nitajua wanajua walisemalo. Nyere alisema " ukijua cha mbele mwenzio atajua cha nyumba , hivyo kudanganya ni ngumu". wakitaka kujikaaanga na mafuta yao waende mahakamani. grrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Kama ni ukweli wasikanushe waende mahakamani. Na kama ni uzushi waacheni wahukumiwe ili tasnia ya habari heshima yake irudi.
Huenda MAGAZETI MAONGO YAKAPUNGUA
 
Kama ni uwongo kwa nini RA na Serukamba walivamia printers usikuusiku kusitisha chapizo? Si wangeenda mahakamani kudai fidia?
 
kumbe kutishia tu, bongo kutishia ndio mtindo... nikajua limeshtakiwa

sie bwana na mabeberu, bila kutisha hatutali... kuanzia mawaziri, wabunge, rais, mafisadi, mwakitaa, mashuleni etc
 
Hakuna lolote, huyu huyu lowassa ameshamtishia mara kibao kubenea na hajawahi kumfanya lolote, RAIA MWEMA hakuna kubabaika,kanyaga twendeeeeeeee!!!!!
 
Hakuna lolote, huyu huyu lowassa ameshamtishia mara kibao kubenea na hajawahi kumfanya lolote, RAIA MWEMA hakuna kubabaika,kanyaga twendeeeeeeee!!!!!

wewe ni kati ya wale waumini wa kubenea kwa kiwango cha kutokuangalia hata ukweli ni nini.subiri tuone kama hio kesi raia mwema atashinda kwa kuwa ina makosa mengi sana
 
Raia mwema ni gazeti makini sana, na hivyo haliwezi kukurupuka kuandika kitu kisicho na ukweli.acha huyo fisadi aende mahakamani, isitoshe tumechoka na banditry wanayoifanyia nchi hii.
 
Hivi kwanini Lowassa anapenda kutisha tu badala ya vitendo? Akiwa waziri alijidai anapenda vitendo kuliko maneno. Iikifika kwenye tuhuma anapenda maneno kuliko vitendo mmasai huyu. Aende mahakamani tu mambo yote yatajulikana huko.
 
wewe ni kati ya wale waumini wa kubenea kwa kiwango cha kutokuangalia hata ukweli ni nini.subiri tuone kama hio kesi raia mwema atashinda kwa kuwa ina makosa mengi sana

Hebu tupe kipengele kimoja wapo unachokiona ni kosa kabla hujatuhumu watu jiangalie wewe nani?
 
QUOTE=Mdondoaji:Hivi kwanini Lowassa ikifika kwenye tuhuma anapenda maneno kuliko vitendo mmasai huyu.

EL a.k.a kichwa cheupe si Mmasai. Ni Mmeru. Baba yake ni Mmeru na mama yake ndo Mmasai. Baba yake alifariki EL akiwa mdogo sana,ivyo akaenda kulelewa Monduli kwa mama na wajomba zake. Bahati yake alipata pesa mingi ivyo amenunua wamasai wote hadi wamempa cheo cha chifu mkuu,EL hasie Mmasai!
 
QUOTE=Mdondoaji:Hivi kwanini Lowassa ikifika kwenye tuhuma anapenda maneno kuliko vitendo mmasai huyu.

EL a.k.a kichwa cheupe si Mmasai. Ni Mmeru. Baba yake ni Mmeru na mama yake ndo Mmasai. Baba yake alifariki EL akiwa mdogo sana,ivyo akaenda kulelewa Monduli kwa mama na wajomba zake. Bahati yake alipata pesa mingi ivyo amenunua wamasai wote hadi wamempa cheo cha chifu mkuu,EL hasie Mmasai!

Asante Nyandaigobeko kumbe jamaa ni Mmeru aka mbulu duh kazi kweli kweli.
 
QUOTE=Mdondoaji;kumbe jamaa ni Mmeru aka mbulu duh kazi kweli kweli.

Not again. Mmbulu sio Mmeru! Kwanza hakuna kabila linaitwa wambulu. Mbulu ni eneo wanapotoka watu wa kabila la wairaqw. Akina Dr Slaa, Marmo,Mary Nagu,Sumaye n.k. Husichanganye makabila ya watu please. Wameru ni wenyeji wa Arusha,na waliishi karibu na Mlima Meru,na sasa wanaendelea kupitakana kwa wingi wilaya za Arumeru Mashariki na Magharibi. Wairaqw wanapatikana kwa wingi Babati Vijijini,Karatu,Mbulu,Hanang' na Katesh. Na tena husije ukamwita muiraqw Mmbulu hata siku moja,ni tusi kwao!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom