RAIA MWEMA: Kukwama kwa Bajeti ya Nishati; Kasi ya CHADEMA yaizindua CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAIA MWEMA: Kukwama kwa Bajeti ya Nishati; Kasi ya CHADEMA yaizindua CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Jul 22, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Kukwama kwa Bajeti ya Nishati

  Kasi ya CHADEMA yaizindua CCM

  Mwandishi Wetu
  20 Jul 2011
  Toleo na 195

  [​IMG]
  • Januari Makamba, Nape, Mukama watajwa kuhusika
  • Sitta, Mwakyembe, Nyalandu watoa makucha
  • Makundi nayo yaelezwa kutumika kuitisha serikali
  CHANGAMOTO za wabunge wa upinzani wakiongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), zimefanikisha kuwazindua wenzao wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao wiki hii wameamua kuigomea bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, kwa baraka za sekretarieti mpya ya chama hicho, Raia Mwema limebaini.

  Uchunguzi wa Raia Mwema mjini Dodoma na Dar es Salaam, umebaini kwamba changamoto zilizotolewa na wabunge wa upinzani zimeonekana zitasababisha CCM kupoteza mvuto kwa umma na baada ya kuonekana tatizo la umeme kuwa kero kubwa kwa wananchi, chama hicho tawala kikaona ni lazima wabunge wake wawe wakali kuwapiku wenzao wa upinzani katika kutetea wananchi.

  Wabunge wa CCM ambao huunda takriban asilimia 78 ya Bunge, walikutana na kupokea taarifa ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, huku wakiwa na baraka zote kutoka kwa sekretariati ya chama hicho, inayoongozwa na Katibu Mkuu, Wilson Mukama.

  Pamoja na changamoto la wabunge wa CHADEMA, habari zinaeleza kwamba makundi ndani ya CCM yamechangia kwa kiasi kikubwa kuwabadilisha wabunge wa CCM, baadhi wakiwa na malengo ya kuwatetea wananchi na wengine wakiwa na malengo ya kuiyumbisha serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kulipa kisasi kwa wanaotaka kutoswa kutokana na kuhusishwa na kashfa za ufisadi.


  Kwa mujibu wa habari hizo, hata baadhi ya watu wanaotajwa kuwa mstari wa mbele katika kuitikisa serikali kuhusiana na sakata la umeme, wanaelezwa kuwa na mahusiano ya kisiasa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi na mmoja amewahi kunukuliwa akisema mmoja wa watuhumiwa wakuu anastahili kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015.


  Kwa upande wa sekretarieti ya CCM kubariki mpango huo, imeelezwa kwamba siku chache kabla ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kusoma bajeti yake bungeni, sekretariati hiyo ilikutana, ambapo ilimbana mmoja wa wajumbe wake, ambaye ni mbunge.


  Wizara hiyo ambayo sasa inaongozwa na Waziri Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima, imekabiliwa na changamoto kubwa la uhaba wa nishati ya umeme, changamoto ambayo imekuwa mwiba kwa mawaziri waliotangulia Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi ambao walilazimika kujiuzulu.


  Imeelezwa kwamba Sekretariati CCM ilipewa taarifa hizo na mjumbe mwenzao Katibu NEC wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Januari Makamba na haikuridhishwa na umakini wa wizara kwa mujibu wa taarifa hizo zilizowasilishwa kwao.


  "Sekretariati ilijadili suala hili na kwa kweli tulimbana Januari Makamba, mjumbe mwenzenu na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, atueleze kama serikali imewasilisha bajeti inayokidhi haja.


  "Kwa njia zetu wenyewe pamoja na maelezo ya Januari, tuliridhika kuwa wizara haikuwa imekuja na hoja zinazokidhi haja," alieleza mmoja wa washiriki wa kikao hicho.


  Kutokana na sekretaeriati hiyo kutoridhishwa na Wizara ya Nishati na Madini, Jumamosi wiki iliyopita, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alihutubia mkutano wa hadhara, mkoani Mbeya na kutoa wito kuwa wabunge wa CCM wasipitishe bajeti hiyo kama wizara bado itaendelea kuwa na hoja zisizokidhi haja.


  Kauli hiyo ya Nape ilipewa uzito na kauli nyingine za waliohutubia mkutano wa Mbeya, akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, aliyesema tatizo la umeme nchini limechangiwa na mambo mengi si tu uhaba wa maji.


  Kwa mujibu wa Sitta, tatizo hilo la umeme nchini pia limechangiwa na baadhi ya viongozi waliopita kushiriki katika vitendo vya ufisadi.


  Ikiwa kama mwendelezo wa moto ulioanzia kwenye sekretariati ya CCM iliyokutana mjini Dodoma wiki iliyopita, wabunge wa CCM walianza kuchangia bajeti ya Wizara hiyo, Ijumaa wiki iliyopita waliishambulia wizara na kuweka bayana kuwa hawataiunga mkono.


  Msimamo huo ulioanzishwa na wabunge, Anne Kilango Malecela, James Lembeli, Beatrice Shelukindo, Ester Bulaya, Dk. Hamis Kigwangala, Nyambari Nyangwine na wengine wengi, ulishika kasi siku ya Jumatatu wiki hii, kiasi cha wabunge wote wa CCM kukutanishwa kwenye kikao maalumu, mchana siku hiyo.


  Taarifa zinaeleza kuwa ndani ya kikao hicho msimamo uliwekwa kuwa Waziri Ngeleja asijibu hoja za wabunge isipokuwa Serikali ije na mpango unaoeleza lini umeme utapatikana.


  Ni kutokana na hali hiyo, mara baada ya kuanza kwa sehemu ya pili ya kikao cha Bunge Jumatatu wiki hii, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliliomba Bunge likubali Serikali iondoe bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini hadi itakapowasilishwa tena katika wiki tatu zijazo, katika tarehe itakayopangwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda.


  Hata hivyo, Waziri Mkuu hakuishia kuomba tu Bunge likubali kuondoa hoja ya bajeti hiyo bali alieleza mipango ya Serikali inayothibitisha uwezekano wa kuondoa tatizo la umeme hadi kufikia Desemba, mwaka huu.


  Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Pinda, umeme utaweza kupungua makali ifikapo Agosti 31, mwaka huu na upungufu unaweza kukabiliwa kabisa ifikapo Desemba.

  Waziri Mkuu aliwaeleza wabunge kuwa Serikali itanunua mitambo ya kuzalisha umeme ili hatimaye iweze kuzalisha megawati 65 za umeme wa ziada na kwamba mchakato huo utahusisha Bunge kupitia kamati zake zote zinazohusika.
   
 2. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  NAUNGA MKONO hoja
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Huu ni upuuzi wa ajabu sana, ina maana makosa yaliopo huyu mwandishi wa habari hayaoni? Nape na wenzie ndio waliomtuma Jairo atoe Rushwa? hamna kitu hapa Nishati ujinga huu, anataka kusema wabunge hawakuwa na hoja juu ya kupinga ile bajeti?

  Sijawai kuona mwandishi wa habari mpuuzi kama huyu.
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli huyu Mwandishi ni Mbuzi wa Kafara!
   
 5. k

  kabyex Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umeshafanyiwa lobbyng nin ya kutetea chama.
   
 6. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  another piece of crap...so these actors wanadhani audience haijui kuwa wao wana-act tu basi
   
Loading...