RAIA MWEMA: Kina Zitto hatarini; CCM yataka kubadili aliyoanzisha Samuel Sitta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAIA MWEMA: Kina Zitto hatarini; CCM yataka kubadili aliyoanzisha Samuel Sitta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 23, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mwandishi Wetu
  Dodoma
  22 Jun 2011
  Toleo na 191

  [​IMG]

  • CCM yataka kubadili aliyoanzisha Samuel Sitta

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama, kimeanza kushawishi ili kiongoze Kamati nyeti za Bunge ambazo Spika aliyepita Samuel Sitta, aliziweka katika uongozi wa wabunge wa Upinzani, imefahamika.

  Mukama alidokeza mwelekeo huo wa ushawishi wakati akihutubia mamia ya wahitimu wa vyuo vikuu mkoani Dodoma, mwishoni mwa wiki, katika hafla maalumu iliyofanyika ukumbi wa Royal Village, Dodoma na kwamba kazi hiyo itawezekana kwa kuwa tayari wakati huo CCM kitakuwa kimekwisha kujivua gamba na mpango huo utawezeshwa na kuwapo kwa wabunge wake makini.

  Kama Mukama ataendelea na ushawishi huo, ni dhahiri kuwa unaweza kufanikiwa kutokana na ukweli kuwa wabunge wengi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni wa CCM na kwa kuzingatia mazingira maalumu, kanuni za Bunge zinaweza kubadilishwa.

  Ingawa katika maelezo yake kwa wahitimu hao wa vyuo vikuu Mukama hakuweka bayana, lakini kamati za kudumu za Bunge ambazo zimetengwa kwa mujibu wa kanuni kuongozwa na wabunge wa Upinzani ni kamati tatu za kudumu.

  Hizo ni Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Kabwe Zitto na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema.

  “CCM ina wabunge wengi wasomi na wenye uwezo mkubwa sana kuliko hata wengine. Tunataka chama hiki kiwe wazi zaidi na kuisimamia karibu zaidi Serikali....sasa mimi nashangaa pamoja na kuwa na wabunge wengi hao kamati muhimu wanawapa wapinzani,” alihoji Mukama katika hali inayotafsirika kuwa malengo ya CCM kujivua gamba ni kuimarisha uwazi zaidi na chama hicho kutaka kuisukuma moja kwa moja Serikali katika utendaji, uadilifu na kusikiliza kilio cha wananchi wakati wote.

  Hata hivyo, bado haijawekwa bayana kama suala hilo tayari limejadiliwa na Sekretariati ya CCM ambayo pia kama imejadili ni lazima kulifikisha suala hilo kwa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu yake, ikitarajiwa kuwa ni suala linaloweza kufanywa kwa ‘usiri’ ili kukwepa kile kinachoweza kuelezwa kuwa kuingilia mhimili huru wa Bunge.

  Uamuzi wa kamati hizo kutakiwa kuongozwa na Upinzani uliasisiwa na Spika aliyepita Sitta, ambaye aliweka bayana kuwa lengo lilikuwa kusaidia uwajibikaji zaidi na kuondoa mgogoro wa maslahi kwa kuwa hesabu zinazosimamiwa ni za Serikali ya chama tawala.

  Hata hivyo, Sitta alishawishi uamuzi huo akirejea taratibu za mabunge ya Jumuiya ya Madola katika mazingira ambayo CCM na Serikali ilikuwa imezongwa na kashfa kubwa za kampuni ya kufua umeme ya Richmond iliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Edward Lowassa kujiuzulu pamoja na mawaziri wawili waliopata kuongoza Wizara ya Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha.

  Mbali na kashfa hizo, kashfa nyingine zilizoshika kasi ni pamoja na kashfa ya wizi wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) Benki Kuu ya Tanzania.

  Kansa ya CCM
  Katibu Mkuu huyo wa CCM, katika hatua nyingine alisema hatua iliyochukuliwa na chama hicho ya kujivua gamba inagusa masuala mengi ikiwamo kuondoa kansa ya baadhi ya vigogo kujipangia safu binafsi za uongozi hasa nyakati za uchaguzi wa ndani, akiweka bayana kuwa hayo ndiyo mazingira yanayokitafuna chama hicho katia maeneo mengi, ukiwamo Mkoa wa Arusha.

  Mgogoro umekuwa ukirindima mkoani Arusha kati ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), James Millya na Katibu wa CCM Mkoa Mary Chatanda huku taarifa zikieleza kuwa katikati ya mtafaruku huo mkubwa, unaoelezwa kuwa sasa umepozwa, yupo Lowassa ambaye ana waumini katika makundi ya vijana yanayoongozwa na Millya.

  “Kuna kansa ya kupanga safu za uongozi katika chama na haya ni matatizo pia yaliyojitokeza Arusha. Kuna rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia wakati fulani wajumbe wote wa huko hawatokani na wanachama bali ni wajumbe wa kiongozi fulani,” alisema Mukama akiwahutubia mamia ya wahitimu hao wa vyuo vikuu mkoani Dodoma, ambao ni wanachama wa CCM.

  Udhaifu wa CCM
  Kama vile akiachia wenye akili kumaizi, Mukama hakwenda kwenye undani wa suala hilo la magomvi ndani ya CCM na badala yake aliendelea kufichua orodha ya maeneo dhaifu katika kuimarisha chama hicho.
  Kwa mujibu wa Mukama, kuna mazingira mahsusi ya udhaifu yaliyoshinikiza chama hicho kujipanga upya katika mwekeleo wa kujivua gamba ambao alisisitiza kuwa ni kipindi cha mpito na si msukosuko.

  Maeneo hayo ni mosi; dhuluma za ufisadi, pili; udhaifu wa vyombo vya uamuzi katika chama hicho, tatu; kujipenyeza kwa wafanyabiashara wasio waaminifu na nne; kujilimbikizia vyeo. Maeneo mengine aliyotaja ni kupomoroka kwa utamaduni wa kuwajibishana; kushindwa kusimamia sSrikali yake katika maeneo kadhaa, ikiwamo baadhi ya mikataba ya uwekezaji.

  Alisema ni kutokana na matatizo hayo yote ndiyo maana hatimaye CCM imebebeshwa mzigo na umma kwamba ni chama kinachobeba mafisadi.

  “Ndiyo maana tunatakiwa kufanya mabadiliko ili chama hiki kirejee kuwa chama cha wanyonge. Hata Mwenyekiti wetu (Rais Jakaya Kikwete) amekwishakusema hata kama tukitekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa asilimia 100 kama jamii haina imani nasi katika suala la maadili tutashindwa tu.

  “Na hili limekwishajitokeza. Pale Nyamagana (Mwanza) tumetekeleza Ilani yetu vizuri, lakini tumekataliwa (kukosa ubunge),” alieleza Mukama katika mkutano huo.

  Ubunge Viti Maalumu

  Mukama ameeleza kuwa yapo makundi mengi maalumu ambayo CCM imeshindwa kujikita na kujipambanua nayo, ingawa pia kuna nafasi maalumu za kufanya hivyo zikiwamo za Ubunge wa Viti Maalumu.

  “Kuna makundi mengi ambayo CCM haijaweza kujipambanua nayo, mfano baadhi ya Wabunge wa Viti Maalumu wanaochaguliwa hawana mizizi sawasawa katika makundi hayo,” alieleza Mukama.

  Wateule wanaohoji chama
  Kwa mara ya kwanza, Mukama ameweka bayana kuwa licha ya kwamba yeye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalumu iliyoundwa na Rais Kikwete kufanyia kazi mchakato wa kujivua gamba, lakini Kikwete aliwateua kutokana na sababu kubwa mbili.

  Alitaja sababu hizo kuwa ni kwanza, watu wanaokijua vizuri chama lakini si wenye madaraka kwa wakati huo wa mchakato wa kutafiti namna ya kujivua gamba. Pili, ni timu ya watu wanaoweza kukihoji chama hicho ili baadaye kijijengee uhalali wa kuihoji na kuisimamia serikali.

  “Tuliandaa waraka ambao Mwenyekiti aliuita A case for reform . Ameunda timu ya watu wanaokielewa vizuri chama lakini pia wasio na dhamana yoyote katika chama ili wafanye kazi hiyo kwa uhuru...watu wa kukihoji chama,” alisema Mukama.
   
 2. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,976
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mfa maji haachi kutapatapa. Kuna namna CC-Magamba wanafikiri wanaweza kuzaliwa upya na kurudia hali ya zamani. hili nasema wasahau na waendelee na shughuli nyingine. Kuna tabia ya kujidanganya kwa watu waliolewa madaraka kwamba pamoja na kashfa zinazoikumba CC-Magamba kwamba bado wanapendwa jambo ambalo si kweli. Wacha Mukama atafune perdiems za Chama na akimaliza atajikuta kama mtu aliyejaza maji kwenye gunia. Namwonea huruma kwani anakwenda tafuta msaada kwa wanafunzi ambao ni desperate kwa kunyanyaswa na CC-Magamba. Mzee lazima ukubali tukutafutie Joti akuimbie ule wimbo wa umefu.....
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Now the party is becoming a dictatorial
   
 4. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Porojo
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Wanawafuata watoto (wadogo) wa udom kuwahadaa. Wanawawekea magamba tu
   
 6. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Mkuu hapo umechemka, hayo yalikuwa masharti ya wafadhili kuwa kamati nyeti za:
  1. Kamati ya kudumu ya hesabu za mashirika ya umma-zitto kabwe-CDM
  2. Kamati ya kudumu ya hesabu za serikali za mitaa-August Lyatonga Mmrema-TLP
  3. Kamati ya kudumu ya hesabu za Serikali kuu- Mamose Cheyo-UDP
  4. Independence ya CAG
  Hizi zote zinamulikwa kwa karibu wa wanaotufadhili(donor countries) CCM wasijidanganye hao akina Mukama na Nape wanapendekeza wasichokijua watachemsha
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  It has always been dictatorial...Yaani katibu wa chama anaweza vipi kuingilia maswala ya Bunge kama sio Udikteta.

  Siku Anna Kilango alipolazimisha kuweka kipengele cha sheria within a day ili kuwashirikisha wabunge wa CCM (ambao hawatakiwi) kupiga kura ktk uchaguzi wa viongozi wa mabarza hayo wakimpa Cheyo, Zitto na Mrema ndipo nilipojua kwamba CCM inatawala kimabavu.
   
 8. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Katibu kilaza kweli' hajui hizo kamati 'watch dog' zinafuatwa na mabunge yote ya madola.HAJUI AU NI KUJIUGUZA WEHU!.
   
 9. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kama ni umafia sawa na umafia mwisho ni kuanguka kabisa, kutakata hakupo kabisaa maana wa kukitakatisha wamekana hadharani kwamba hilo halipo!Kufanikiwa kuzirejesha hizo kamati itategemea uwezo wa kuendesha serikali kama bado ni kwa mtindo wa bakuli basi hilo wasahau maana wenye kuchangia hawawezi kukubali hilo
   
 10. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  OMG, this must be the understatement of the year ! CCM is and has always been dictatorial in every sense of the word. CCM is founded on party supremacy and so lives, survives and thrives on dictatorship, take that away and it will crumble like a pillar of snow when the sun comes out ! CCM might have been forced to preach democracy but what it practices is something much more akin to an autocratic form of leadership than a government of the people, by the people and for the people.

  And now as the situation gets worse following the awareness sweeping across the nation, CCM finds itself fighting for survival and has to employ any means to retain what little hold it still has on the hapless citizenry. When coaxing, rumour-mongering and cajolery fail, CCM has it all ready-made and laid out - the security organs, armed to the teeth. And so like all faschist regimes do, it has no alternative but come down hard on any voices of dissent and this is one area where CCM beats all expectation.
   
 11. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dalili zilishaonekana siku nyingi, maana kamati mbili za hesabu za serikali za mitaa (lyatonga) na ile ya Bw. Mapesa hatuwezi kusema zimepewa wapinzani
   
 12. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hao members wa ccm kutoka udom inabidi sampuli za ubongo wao zipelekwe maabara.Nathani uwezo wao wa kufikiri unazidiwa na ule wa nzi.
   
 13. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  udom si ndio wale walimchangia mkuu wa kaya pesa ya kuchukulia fomu au? then mwisho wa siku wakanyimwa mikopo na pesa ya filed na walipigwa mabomu juu...waache wadanganywe hao wameshazoea.
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hivi Mukama naye haoni nje ya box anadhani watu wote wako ndani ya box ? Haya yetu macho na mwendo wao tutauona .
   
Loading...