Raia Mwema: Kikwete na porojo za CCM kujivua gamba II; Ana mchezo mchafu kubagua kwa misingi ya Dini

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Mwandishi Maalum
1 Jun 2011
Toleo na 188
  • Ni ‘usanii' wa kusafisha njia kwa anayemtaka 2015
  • Anayemtaka ni Asha-Rose Migiro?

NI vigumu kuamini kwamba rais wa nchi anaweza kuhusika na mchezo mchafu kama huu wa kuwabagua wananchi wake kwa misingi ya dini zao, lakini matukio ya hivi karibuni yanathibitisha hilo.

Baada ya uchaguzi mwaka jana na hasa tukio la Arusha la Watanzania kupigwa na polisi kwenye maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kisha harufu ya udini kuibuka, baadhi ya Waislamu wachache wenye mtazamo mkali walianza kuzunguka nchi nzima wakitoa mahubiri ya chuki.

Mkutano mmoja ulifanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na inadaiwa ulipata baraka za Kikwete. Baadhi ya mikutano hiyo ilijadili masuala tata, na baadhi ikaibuka hata na mapendekezo ya ajabu ukiachilia yale ya muda mrefu kama vile kudai Mahakama ya Kadhi na Tanzania kuingia kwenye Jumuiya ya Kiislamu Duniani (OIC).

Madai mengine yalihusu malalamiko kwamba Wakristo wamekuwa wakipendelewa tangu enzi za ukoloni na kwamba ingawa Waislamu ni wengi zaidi Tanzania, lakini hawana nafasi nyingi za madaraka. Madai mengine yaliyotolewa ni kwamba Wakristo wana shule na mahospitali lakini Waislamu hawana, na kwamba serikali hutoa fedha kuzisaidia hospitali za Wakristo na walimu wa kufundisha shule za Wakristo, lakini Waislamu wanaachwa hivi hivi tu.
Baadhi walifikia hata hatua ya kumlaani Mwalimu Nyerere na kusema kwamba hastahili kuitwa Baba wa Taifa; bali anastahili kuitwa Baba wa Kanisa Katoliki. Baadhi yao, akiwemo kigogo wetu, hawamwiti Mwalimu Nyerere kwa hadhi yake iliyozoeleka ya Baba wa Taifa, na badala yake humwita Mzee Nyerere.

Kwa ufupi, kuna imani kubwa miongoni mwa Watanzania kwamba utawala wa Rais Kikwete unalea udini, na asipokuwa makini nyufa hii yenye msingi wa kidini inaweza kupanuka na kuutia dosari umoja wa kitaifa tulionao ambao misingi yake si udini.

Geresha ya kujivua gamba

Pamoja na kubadili safu ya uongozi mjini Dodoma, CCM pia ilitangaza kwamba wanachama wake watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe wenyewe; la sivyo wataondolewa kwa nguvu. Wanachama hao wanatajwa kuwa ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, na wabunge wawili, Andrew Chenge na Rostam Aziz. Ni kweli matajiri hawa hawapendwi na Watanzania wengi isipokuwa pengine wa majimboni mwao tu.
Lakini pia watu hawa watatu wana sifa nyingine: Kwamba ndio tishio pekee na la kweli dhidi ya mpango wa Kikwete wa kusaka mgombea urais wa mwaka 2015 ambaye ni Mwislamu. Wanaotaka kumweka Lowassa kwenye urais mwaka 2015, si tu wanakwamishwa na tuhuma hizi zinazomwandama na hatihati hii ya kung'olewa CCM, lakini pia wanakwazwa na Kikwete mwenyewe. Inadaiwa kwamba, kwenye mbio za urais za 2015, tatizo la Kikwete kuhusu Lowassa si kwamba anakabiliwa na tuhuma za ufisadi; bali kwamba si Mwislamu.

Kundi hili la kina Lowassa inaaminika lina urafiki wa karibu na Makamba ambaye inadaiwa kuwa agenda yake kubwa kwa mwaka 2015 haikuwa udini; licha ya kuwa naye amesikika mara kadhaa akilumbana na maaskofu; bali yeye (Makamba) ana ndoto ya mwanae (January) aje kuachiwa urais mwaka 2025 na kundi hili. Makamba hutamba kwamba mwanae anafaa kuwa kiongozi, na hakuna ubishi kwamba alihakikisha mwanae anapata ubunge, uenyekiti wa kamati ya Bunge, na kisha kuingia kwenye Sekretarieti ya CCM.

Aidha, mtoto huyo wa Makamba pia anaelezwa kuwemo kwenye kundi linalowaunga mkono watuhumiwa hawa wa ufisadi ambalo lina idadi kubwa ya wabunge na viongozi wa CCM wa ngazi za wilaya, mikoa na taifa. Hii ndiyo sababu tangu CCM ilipoanza kushambulia mafisadi hadharani, yeye amepotea jukwaani!

Kimsingi, kuna kutofautiana kati ya Makamba na Kikwete kuhusiana na nani awe rais mwaka 2015 na kuhusu nini wafanyiwe hawa watuhumiwa wa ufisadi. Hivyo; tangazo la kujivua gamba pamoja na kutajwa kwa watuhumiwa hao ambao Kikwete mwenyewe aliwapigia kampeni mwaka jana kwenye uchaguzi wa wabunge, ni geresha tu. Ukweli ni kwamba Kikwete alikuwa anaunda timu itakayomrithi mwaka 2015.
Kimsingi, hadi sasa Kikwete ameshawaacha ‘wabaya' wake wote nje ya Kamati Kuu ambao ‘dhambi' yao kuu ni kuutaka urais wa mwaka 2015. Watu hao ni pamoja na Membe na Andrew Chenge ambaye anamtaka Lowassa.

Kwa ufupi, janja hii ya Mwenyekiti Kikwete ya "kujivua gamba" ililenga katika kuwaengua wale wote wanaoweza kumsumbua kwenye suala la urais wa mwaka 2015; ingawa pia ni kweli kwamba ukiuangalia juujuu utaona kuwa mpango huo wa "CCM kujivua gamba" unalenga katika kupunguza nguvu za CHADEMA kwa kuirejeshea CCM mvuto wake wa zamani.
Vyovyote vile; hakuna ushujaa wala maamuzi magumu yaliyofanyika Dodoma. Ulikuwa ni ‘usanii' tu, na ndiyo sababu hakuna kiongozi wa CCM anayepigia kelele kung'olewa chamani mafisadi zaidi ya kijana Nape na Katibu Mkuu mpya, Wilson Mukama ambao, hata hivyo, nao wamefungwa "gavana" hivi karibuni kuhusu kulipigia debe suala hilo. Hata Chiligati aliyejitokeza mwanzoni kuhubiri nia ya kuwavua uongozi wa CCM kina Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge, sasa naye ameingia mitini!


Kauli ya Joseph Butiku
Labda nigusie pia kidogo kuhusu malalamiko ya Joseph Butiku aliyoyatoa katika mahojiano na gazeti la Raia Mwema, hivi karibuni, kwamba viongozi wa CCM wamemwachia Mwenyekiti Kikwete mzigo wa kupambana na mafisadi.

Mimi nadhani madai hayo ya Butiku ameyatoa bila kujua ukweli wa mambo. CCM haiko kwenye mapambano na mafisadi; bali Mwenyekiti Kikwete ndiye anapambana na maadui zake kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta mrithi wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015; ila tu amepata bahati kwamba watu hao hao ndio wanaolalamikiwa kwa ufisadi. Ni bahati tu ya mtende iliyotoa fursa ya ‘usanii' huu kuchezwa! Aidha, kelele za CCM kupitia kwa Nape kwamba kuna vyombo vya habari, viongozi wa Upinzani na viongozi wa dini ambao wamepangwa kuwatetea mafisadi na kuishambulia familia ya Kikwete, ni janja ya kuwatangulia mbele ili wakisema jambo, wananchi waambiwe: "Si tulisema, mnaona sasa!?"

Hata hivyo, inafahamika kuwa makundi haya matatu ndiyo yako mstari wa mbele kupinga ufisadi na udini unaosambazwa na Kikwete na watu wake, hivyo lolote litakalosemwa halitakuwa geni; bali ni muendelezo unaofahamika. Pengine CCM haijui kuwa wananchi wanajua kinachoendelea.

Wagombea wa Kikwete 2015

Kwa kufuatilia mambo ya kisiasa yanavyokwenda na jinsi Rais Kikwete anavyoendesha mambo yake, kuna majina mawili ya watu wanaotajwa ambao angependa wachukue urais na umakamu wa rais wa Muungano mwaka 2015. Hii inatokana pia na imani yake kwamba Katiba mpya haitabadili mfumo wa sasa.

Sababu kubwa ni mbili: Kwanza, kutekeleza ahadi yake ya siri kwamba hawezi kuacha nchi kwa Mkristo; na pili, kuhakikisha uongozi mpya unamlinda yeye na familia yake dhidi ya misukosuko ya hapa na pale ambayo kawaida kote duniani hutokea mtu akishaacha urais. Hakika, naye hatapenda kushambuliwa kama inavyotokea kwa Mkapa.

Baada ya kufanikiwa kuwaengua pembeni Lowassa na Membe (Prof. Mwandosya kanusurika?) ni nani, basi, ambaye Kikwete anamtaka kwa urais wa 2015 na atachezaje karata zake kuhakikisha jina la mtu huyo linapeta?

Ili watu hao wawili anaowataka wakubalike, inaaminika kuwa Kikwete atatumia mtindo ule ule wa funika kombe mwanaharamu apite. Atawapendekeza kwa kutumia vigezo vinavyoficha ukweli. Kutokana na hali ya kisiasa itakavyokuwa, anaweza kusema: "Jamani ni zamu ya wanawake sasa, tusitawale akina baba tu, nchi yetu wote."

Iwapo wazo hili litakwama, basi, Kikwete anaweza kusema hivi: "Jamani sasa wenzetu wa Zanzibar nao, miaka 20 imepita, tuwape nao nafasi jamani." Msemo huu, hata hivyo, hauna mashiko iwapo Katiba haitakuwa na agizo hilo; kwani upande wa Upinzani unaweza kuweka wagombea wote wa Bara.

Mbinu hiyo Kikwete ameshawahi kuitumia kwenye kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana ambapo alimpendekeza kijana wa Visiwani, na pia aliitumia kwenye kupata jina la mgombea wa uspika. Anaamini kuwa mbinu hiyo itasaidia kufunika hoja yake ya udini isionekane, na hivyo kufanikisha kupata rais Mwislamu.

Asha-Rose Migiro na Dk. Mwinyi
Katika miaka ya karibuni Kikwete amekuwa na mahusiano ya karibu ya kikazi na mwanamama mmoja ambaye kila baada ya miezi michache hufika Ikulu, na kisha picha nyingi hupigwa kuonesha kwamba wawili hao wanaelewana na wanashirikiana kisiasa pia.

Huyu ni mwanamama ambaye ni mmoja wa wanasiasa wachanga waliofaidika na vyeo vya uwaziri wa Kikwete mwaka 2005. Aidha, pale Tanzania ilipopewa mwanya wa kutoa jina la mwanamke wa kushika nafasi ya juu kimataifa, Kikwete hakusita kumtaja mwanamama huyu.
Nafasi hii ilikuwa baada ya Tanzania kufanya kampeni kubwa barani Afrika kuunga mkono jina la Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Ban ki-Moon, kwenye kugombea nafasi ya ukatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Mwanamama huyo pia ana kisomo kizuri kinachokubalika na kinachoweza kuwaaminisha watu wanaotaka kuuliza maswali kuhusu uwezo wake kiutendaji wa kuiongoza nchi yenye matatizo ya uchumi na yenye mipasuko kibao kama Tanzania. Mwanamama huyo ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro ambaye anaelezwa kuanza kujiandaa kurejea nyumbani Tanzania siku si nyingi.

Kwa upande wa Zanzibar, ni waziri mmoja kijana ambaye urafiki wake na Kikwete huwashangaza viongozi wengine wa Zanzibar; mathalani jinsi wanavyosalimiana kama watoto wa mjini. Katika mtandao wa YouTube Watanzania waliweka picha ya video ya Kikwete akisalimiana ‘kishkaji' na waziri huyu kwenye Uwanja wa Amani, Zanzibar siku ya Januari 12, mwaka huu. Picha hiyo iliibua gumzo kubwa.
Hivi karibuni Waziri huyu alipokabiliwa na msukosuko wa kutakiwa na wananchi kwamba ajiuzulu ambao kimsingi ulisababishwa na utendaji dhaifu wa Jeshi la Wananchi uliochukua maisha ya watu kwenye milipuko ya maghala ya silaha, alikataa na Kikwete hakusema kitu. Huyu ni Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi.


Hitimisho langu
Inaaminika kuwa hao wawili ndio chaguo la Kikwete katika mbio za urais za 2015, na chaguo lake hilo linachagizwa zaidi na dini zao badala ya vigezo vya jumla vya sifa ambazo Watanzania wote tunataka mtu anayetaka kuwania urais kuwa nazo.

Hata hivyo, napenda nieleweke kwamba sina tatizo na rais ajaye kuwa Mwislamu au Mkristo; ilimradi tu awe ni kiongozi hodari, mchapakazi, mwadilifu na mwona mbali. Angalizo langu ni kwamba rais huyo ajaye asitafutwe kwa msingi wa dini yake; bali kwa vigezo hivyo vya ubora.
Nasisitiza hivyo; maana Watanzania katika ujumla wao hawajali dini ya mtu ila uadilifu na uchapakazi tu, lakini viongozi wetu ndio wenye matatizo ya udini. Na kwa hakika, Kikwete analo tatizo hilo.
Nihitimishe kwa kusisitiza kwamba wajibu wa wana-CCM ni kukisafisha chama chao kwa uaminifu na werevu, na kisha kuachia demokrasia iamue nani awe mgombea wa CCM mwaka 2015. CCM na Kikwete wawe waangalifu na dhana hii ya "sasa ni zamu yetu kutawala" ili Tanzania isitumbukie kwenye matatizo yanayosikika kwenye nchi zingine.
 
Kwanini Kikwete anamchukia Nyerere? Ni sababu ya kuingilia NEC 1995? Kumchagua Mkapa badala ya yeye?

Anatupeleka kubaya kweli huyu Mzee

What I can say is Religion is regarded by the common people as true, by the wise as false, and by the rulers as useful just to evil people doing bad things, but for good people as well to do bad things, it takes religion for him now the wall of Separation between Church and State is not there
 
Kwanini Kikwete anamchukia Nyerere? Ni sababu ya kuingilia NEC 1995? Kumchagua Mkapa badala ya yeye?

Anatupeleka kubaya kweli huyu Mzee

What I can say is Religion is regarded by the common people as true, by the wise as false, and by the rulers as useful just to evil people doing bad things, but for good people as well to do bad things, it takes religion for him now the wall of Separation between Church and State is not there

Kila mtu anahaki ya kuexpress vile anavyoona ni haki yake. Nyerere kuitwa Mzee Nyerere ni haki yake, kwa sababu ya umri aliokuwa nao. Kwa wanaojua Kiswahili, especially watu wa coast, kumwita mtu, au kumwambia mtu amwite mtu "Baba" wakati SI "Baba" yake ni tusi kubwa. Huwezi kuwalazimisha watu wamwite "Baba" wakati wanajua ukweli ndani yake.
 
Habari hii imeandikwa ili tuzingatie kuwa ccm itaendelea kutoa maraisi wa Tanzania kwa miaka ijayo. Hata hivyo, ccm imejidhihirisha wazi kwa vitendo vya wanachama wake waliopo madarakani kuwa hawapo hapo kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa Tanzania, bali kwa maslahi yao wenyewe.

Jinsi siku zinavyokwenda, ccm wanazidi kujichanganya kwa kutoa habari za maamuzi, ambazo ni kinyume na vitendo vinavyofanyika. Kwa mifano michache ni zoezi la kujivua gamba, ambalo kwa sasa limeonekana kwa wengi kuwa ni usanii; mada ya kupunguza posho zisizo na tija, jambo ambalo viongozi wa ccm, bila kujali athari za kuipinga mada hiyo, wameng'nga'nia kutopunguzwa posho kwa maslahi ya wafanyakazi na wananchi wote kwa ujumla.

Mapingufu hayo ni makubwa mno na muda uliobaki mpaka uchaguzi ujao ni mfupi mno, kiasi ambacho kwamba itakuwa ni vigumu kurudisha imani kwa wananchi, hata kama huyo mgombea ataonekana ni msafi na anazo sifa.
 
Mwandishi Maalum




Hitimisho langu
Inaaminika kuwa hao wawili ndio chaguo la Kikwete katika mbio za urais za 2015, na chaguo lake hilo linachagizwa zaidi na dini zao badala ya vigezo vya jumla vya sifa ambazo Watanzania wote tunataka mtu anayetaka kuwania urais kuwa nazo.

Hapo umenena mzee.

Hata hivyo, napenda nieleweke kwamba sina tatizo na rais ajaye kuwa Mwislamu au Mkristo; ilimradi tu awe ni kiongozi hodari, mchapakazi, mwadilifu na mwona mbali. Angalizo langu ni kwamba rais huyo ajaye asitafutwe kwa msingi wa dini yake; bali kwa vigezo hivyo vya ubora.
Nasisitiza hivyo; maana Watanzania katika ujumla wao hawajali dini ya mtu ila uadilifu na uchapakazi tu, lakini viongozi wetu ndio wenye matatizo ya udini. Na kwa hakika, Kikwete analo tatizo hilo.
Nihitimishe kwa kusisitiza kwamba wajibu wa wana-CCM ni kukisafisha chama chao kwa uaminifu na werevu, na kisha kuachia demokrasia iamue nani awe mgombea wa CCM mwaka 2015. CCM na Kikwete wawe waangalifu na dhana hii ya "sasa ni zamu yetu kutawala" ili Tanzania isitumbukie kwenye matatizo yanayosikika kwenye nchi zingine.
[/QUOTE]

Nina wasiswasi mzee Mwinyi is behind this move of his son to be the fifth president of Tanzania. Maana nasikia alimpigia kifua ****** 2005 kwamba 1995 alinyang'anywa hiyo nafasi kwa hivyo 2005 apewe ******. Kwa hivyo ****** anaweza akarudisha fadhila.
 
Nina shaka kama hii storu imetokea Raia Mwema; huyu mwandishi ana mawazo yake juu ya hali ya kisisa ilivyo hapa nchini na anachukulia eti ndio maoni ya wengi!

Juu ya hou udini anoudai wandishi; hivi mbona hata huyo Asharose Migiro dini yake sio Muisilamu?
 
Ni wazi JK anaandaa njia kwa ASHA ROSE MIGIRO kwa sababu za kidini and not otherwise
Kwa nini ASIWASOGEZEE NAFASI AKINA SAMWELI SITTA au MEMBE?
 
Sisi watu wa pwani hatumwiti kila mtu baba, hata kwa mfano kule zanzibar raisi karume marehemu huitwa mzee karume, na baba ni yule aliekuzaa sasa munaposema mzee nyerere aitwe baba kwa sababu gani au kigezo gani ? Baba ni cheo cha kanisa. mheshimiwa yupo sabibi kabisa ndio maana harakati zote za ubaba na kutawaza utakatifu zinafanyika kanisani.
 
There now we have a class struggle... which leads to Dictatorship.

Dictatorship is a constant lecture instructing you that your feelings, your thoughts and desires are of no account, that you are a nobody and must live as you are told by other people who desire and think for you, Now President Kikwete is now instructing our feelings through CCM CENTRAL COMMITEE... where are we heading???
 
Nimefuatilia kwa Makini habari hii na kugundua yafuatayo:-

1)Mwandishi anaonekana ni MDINI mkubwa kuliko hata huo udini anaouongelea kwenye thread yake kwani ameonekana kuwachukia waislaam kuliko hata kuelezea hali halisi ya mambo yanavyoenda;
ii) Mwandishi amejaribu kuelezea hisia za waislaam km upumbavu kana kwamba ni za kizushi na upumbavu na kujaribu kujifanya yeye na makala ya ke ambayo ni biaseda yuko sahihi sn:
iii) Mwandishi amejiaminisha kwa Mwl. Nyerer asa if ndio Mungu wake na wa watu wote na kwamba anaye enda kinyume nae ni sawa na mtu mwenye zambi nyingi na asiyefaa kusamehewa ikiwa ni pamoja na yule anaeshindwa kumwita kwa jina la Mwalimu, sijui kwake yy ina maana ya uungu;
iv) Mwandishi ameshindwa kuhusianisha huu anaouita UDINI na Kikwete ,na hata dhana ya kujivua gamba;
v) Mwandishi ameshindwa kuelewa kwamba kupitia makala yake ametuelimisha kwamba kumbe kipindi kile Mzee Nyerere ana ingilia maamuzi ya NEC kumpitisha Mkapa na kumwacha Kikwete haikuwa suala la uchanga wake bali ni DHANA YA UDINI UKTAKA KUENDELEA KULISIMIKA KANISA KATOLIKI IKULU; Kumbea hii dhana aliyoirithi Mkapa ya kutaka kumuweka Sumaye Ikulu pengine ni muendelezo wa kutotaka Muislama aongoze tena TZ;
vi) Mwandishi ameshindwa kuutambua mchango wa Nyerere kwa kutoju au kwa makusudi aliyoutoa kwa kanisa Katoliki hadi kufikia kuitwa mwenye kheri;

vii) Mwandishi alivyokuwa KILAZA ameshindwa kutushawishi kuwa yeye anaijua ccm sn kuliko Mzee Butiku ambaye anaijua in anda out ccm. Eti anajaribu kumumbua mzee Butiku mission ya ccm, lol!!!
viii) Mwandishi asivyo na uelewa ameajaribu kuulezea umahiri wa Asha Rose na kusema eti kaibuliwa na Kikwete!! ameshindwa kujua kuwa ameibuliwa na Mkapa wakati akiwa WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO NA Naibu wake akiwa Shimimu Khan(Mhindi) ambae hata kiswahili alikuwa hajui kwa ufasaha. Amesahau kuwa amemsifia kwa uwezo wake lkn conlusion yke eti haoni tatizi rais ajaye kuwa muislam ila awe na uwezo!!!!!!!!!!!!! CRAP!!!
ix) MDINI HUYU ameshindwa kuelewa kuwa CCm inatoa mgombea wa URAIS NI SI RAIS, kwa hivyo bado ana nafasi ya KUKAA VIKAO NA MAKANISA KM WALIVYOFANYA UCHAGUZI WA 2010 KWA AJILI YA KUMPITISHA TENA PADRE SLAA;
X) Hivi amewezaje kumzungumzia Mwinyi kuhusu kutaka kuwajibika km kiongozi asiyefaa na kumtetea Lowasa aliyewajibika kwa ajili ya UBADHIRIFU NA TUHUMA ZA KUMILIKI RICHMOND as if ni MALAIKA?
My take
KAMA HAYA ANAYOFANYA KIKWETE NI UDINI? BASI WAISLAM TUMESHABAGULIWA SN KWA DINI YETU TANGU ENZI ZA NYERERE HADI MKAPA. kUCHAGULIWA MGOMBEA 1995 NA NYERERE KWA SABABU YA UDINI WAKE, NA KUTAKA KUCHAGULIWA SUMAYE 2005 ETI TU KWA SABABU KIKWETE NI MUISLAM.
ALIYEUA KWA UPANGA ATAKUFA KWA UPANGA.
 
Mhhh jamani naomba mnifahamishe. Kwani Dr Asha-rose Migiro ni Muislamu????? Kama ni Muislamu, iweje mumewe ni Mkristo??? Kwani kuna ndoa kati ya Muislamu na Mkristo????
 
Nina shaka kama hii storu imetokea Raia Mwema; huyu mwandishi ana mawazo yake juu ya hali ya kisisa ilivyo hapa nchini na anachukulia eti ndio maoni ya wengi!

Juu ya hou udini anoudai wandishi; hivi mbona hata huyo Asharose Migiro dini yake sio Muisilamu?

Ni Raia mwema la nyuma kidogo kama 3-4 weeks ago na niliisoma,nilishawahi kusikia huyu mama ni muislamu (sina tatizo na hilo).Hoja ni kwa nini viongozi wanakuwa na mawazo ya kuandaa watu wao?
 
Mhhh jamani naomba mnifahamishe. Kwani Dr Asha-rose Migiro ni Muislamu????? Kama ni Muislamu, iweje mumewe ni Mkristo??? Kwani kuna ndoa kati ya Muislamu na Mkristo????

Yes, Asha Rose ni Muislamu, yeah Mumewe ni Mkristo... Yeah kuna Ndoa nyingi tu Tanzania kati ya Wakristo na Waislamu
 
Kwa kuwa Kikwete mwenyewe kashindwa kuiongoza nchi hana sifa tena ya kutuchagulia rais ajaye. 2015 Tanzania itakuwa na sura nyingine kabisa ya serikali na huwenda ikaundwa na vyama kadhaa nje ya ccm hii ikiwa ni pamoja wagombea binafsi. Watanzania wanayo haki ya kumchagua kiongozi wao. Ijulikane kuwa 2015 hakuna chama wala mtu kuvuruga uchaguzi. Mipango ya kidini na siri zote ziko mitaani usijali.
 
Uchambuzi mzuri..ni kweli hii ishu itakuwa kweli..all in all, slaa ndo rais 2015
 
Kila mtu anahaki ya kuexpress vile anavyoona ni haki yake. Nyerere kuitwa Mzee Nyerere ni haki yake, kwa sababu ya umri aliokuwa nao. Kwa wanaojua Kiswahili, especially watu wa coast, kumwita mtu, au kumwambia mtu amwite mtu "Baba" wakati SI "Baba" yake ni tusi kubwa. Huwezi kuwalazimisha watu wamwite "Baba" wakati wanajua ukweli ndani yake.
"Mohandas Karamchand Gandhi is often referred to as Mahatma... In India, he is also called Bapu (Gujarati: બાપુ, bāpu or "Father") and officially honoured in India as the Father of the Nation..." [Wikipedia] - kwa hiyo si kweli kwamba "Baba wa Taifa" imekaa zaidi "kikanisa", na haina maana kwamba huyo ni baba mzazi wa kila mtu. ila ni Baba wa Taifa - kwa maana kwamba amehusika katika uundaji wa taifa hilo. kama unaona Nyerere hahusiki na uundaji wa taifa la Tanzania, basi unayo haki ya kukwazika na hiyo title. lakini kutoa mifano ya kwamba ati kwa huku pwani kumwita mtu baba wakati si babake ni tusi, ni kutoelewa tu. huyu si baba wa Shamu, ni baba wa Taifa.
 
Back
Top Bottom