Raia Mwema hatarini kufungiwa makala 'kila awamu ina rekodi ya kuua', mtego kwa JK

nimehamasika, ntapitia hiyo makala maana sikuisoma bado. Wadau kesho nitapost soft copy ya makala hiyo isomwe kote.
 
Leo nilipita hapa Dar Wizara ya Habari kwa mambo binafsi, nikakutana na taarifa kwamba gazeti la Raia Mwema limeandikiwa barua kutishiwa kufungiwa. Nikadodosa, nikaambiwa ni kuhusu makala isemayo, "KILA AWAMU INA REKODI YA KUUA, Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete...." nikanunua gazeti na kuisoma na kuona ni nzuri na imeandikwa kitaalamu sana na mwandishi "Msomaji Raia" ambaye alipotea sana akielezwa kuwa nje ya nchi kwa matibabu kabla ya kurejea na kuanza kuandika na hii ilikuwa makala yake ya kwanza tokea augue.

Kabla hata ya kusoma na kuondoka Wizara ya Habari, nikasikia mmoja wa maofisa akisema maneno haya, "unajua hii ni hatari sana, maana itakuwa ni sawa na kuisambaza hiyo makala na si kuizuia. Hata wale ambao hawakuisoma sasa wataitafuta na kuisoma. Raia Mwema limekuwa makini katika kutushambulia na limetusaidia sana katika vita ya ufisadi, lakini sasa tukigombana nao, tutakuwa tunamharibia Rais (JK) badala ya kumsaidia, na kwa kutumia jina lake badala ya majina ya marais wote waliotajwa, tutazidi kumchonganisha na wananchi na hata na hao wastaafu na familia zake na tutaonekana ni wabinafsi na Rais ataonekana mbinafsi na anajitetea mwenyewe. Tumefanya kosa kuwaandikia barua, tungawaita tu tukazungumza nao."..... mzungumzaji huyo naona hakupata support yoyote na wenzake walioendelea na kazi zao hadi naondoka eneo hilo na kwenda kusima makala husika.

Nimemuomba mshikaji wangu wa Maelezo nakala ya barua akinipa nitairusha hapa. Wahusika hata ndani ya maelezo naomba watusaidie kuweka barua hiyo hapa kama hawatojali. Nasikia kosa lao ni kusema JK CCM itamfia mikononi kwa kukuthiri kwa ufisadi ndani ya CCM tokea mchakato wa 2005 na ndio maana anapata kigugumizi kuwashughulikia.

Maoni yangu;
Ni kweli kwamba gazeti la Raia Mwema limekua likiegemea sana upande wa JK hasa katika vita inayoendelea ndani ya CCM kati yake na mafisadi na sitoshangaa kusikia kwamba huo ni mkakati wa mafisadi kulidhibiti ama kulichonganisha na JK na hapo watakuwa wamefanikiwa mambo yao, kwani vyombo vingi wameshavishika ama kupandikiza watu. Sitoshangaa maana hata TBC iko mikononi mwa mafisadi na mambo yao huwa yanaenda kiulaini kuliko hata watawala.

View attachment 50461

Vyombo vyetu vitafikia hatua vyote kutekwa na wanasiasa wanaotaka kuneemesha familia zao tu. Kupitia makala inaonesha wanataka kunyong'onyesha gazeti letu raia mwema.
 
Hili si kufungiwa tu, inafaa wachukuliwe hatua za kisheria kali sana, na wapelekwe mahakamani, mhariri na muandishi wa hiyo makala, na wakishindwa kuthibitisha hizo kauli zao, wafungwe maisha. Hawa ni watu hatari sana na wanaweza kusababisha maafa makubwa sana kwa huu uzandiki wao.
 
Ukimsoma Msomaji raia, utagundua kuwa ni mtu yuko kwenye inner circle, makala ya juzi ilikuwa ni ya kwanza baada ya kuwa nje muda mrefu kwa matibabu, je huyu jamaa ni nani?

tusimvue kinyago ati...wacha aendelee kutupa makala motomoto toka jikoni kwenyewe
 
HAYA WADAU MAKALA YENYEWE NDOO HIIO

[h=1]Kila Awamu ina Rekodi ya Kuua[/h] Msomaji Raia

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete…

KAMPENI za uchaguzi mdogo jimboni Arumeru Mashariki zitakumbukwa kwa mengi. Kuna rekodi muhimu zimewekwa na zitakumbukwa.
Kura za maoni zilirudiwa mara mbili ndani ya CCM. Pamoja na malalamiko ya wazi juu ya matumizi ya rushwa, Kamati Kuu ya CCM iliamua kurudiwa kwa uchaguzi huo na hatimaye mtuhumiwa mkuu wa utoaji rushwa akapitishwa na Kamati Kuu.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ambaye hakukubaliana na uteuzi amenukuliwa akisema kwa utani kuwa, "hatukuridhika na rushwa katika awamu ya kwanza, tukaagiza ahonge zaidi awamu ya pili ndipo apitishwe".
Makeke ya TAKUKURU yalikoishia ni wao tu wanaweza kueleza. Kuna wasiwasi kuwa walipokuwa na makeke walikuwa hawajapata mgawo wao. Huwezi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, kisha ukamkamata mjumbe mwenzako wa kamati hiyo.
Rekodi nyingine ilikuwa ni ya mapingamizi dhidi ya wagombea. CCM ilianzisha mtindo huo pale wagombea wake walipomwekea mgombea mwenzao kuwa si raia wa Tanzania. Pingamizi hili lilipuuzwa lakini likaibuliwa na CHADEMA kabla halijatupwa na kukatiwa rufaa mbele ya Tume ya Uchaguzi. Tume hiyo ililitupilia mbali japokuwa kuna maelfu ya Watanzania wananyimwa pasi ya kusafiria kwa sababu hiyo hiyo ya kuzaliwa nje ya nchi. Rekodi na ushahidi umewekwa kuwa, ukiwa ndani ya CCM lolote linawezekana.
Rekodi nyingine ni ya matumizi ya matusi katika kampeini. Chama cha Mapinduzi kiliasisi mtindo huo na CHADEMA kufuatia kwa njia ya kujibu vijembe na matusi hayo. Rais Mkapa atakumbukwa kwa kuzindua mtiririko huo wa matusi na vijembe vilivyochukua nafasi ya sera na mikakati. Enzi za CCM kukejeli kuwa vyama vya upinzani vinatumia matusi katika kampeini zimeisha. Ukienda mkutano wa CCM utajihisi uko mkutano wa wapinzani, na ukienda mkutano wa wapinzani, utadhani uko CCM ya Nyerere. Watu wamehojiana kuhusu ndoa zao, sura zao, kazi zao, urefu wao na ufupi wao.
Rekodi kubwa zaidi ilikuwa ni ya tuhuma ya kifo cha hayati Baba wa Taifa. Kwamba, Serikali ya Awamu ya Tatu ilimlazimishia kifo Baba yetu wa Taifa. Kama ni kejeli au kijembe si hoja. Cha msingi rekodi imewekwa kuwa Baba wa Taifa alikufa na kifo chake kiliacha mashaka makubwa.
Wahenga husema "hakuna utawala usioua". Yaelekea kila awamu ya Taifa letu imeua kitu fulani. Baba wa Taifa na Awamu yake ya Kwanza aliua ukoloni. Ni sahihi kuwa Baba wa Taifa alipanga, akaamua na kutekeleza mpango mahsusi wa kuua ukoloni mkongwe na hatimaye akajitahidi kuupa sumu ukoloni mamboleo.
Hata watoto wetu wanaojifunza historia na uraia wanalijua hilo, kuwa Rais Julius Kambarage Nyerere aliuua ukoloni, Tanzania ikawa huru. Tarehe, mwezi na mwaka vinajulikana. Tumesherehekea nusu karne hivi karibuni.
Awamu ya pili chini ya Mzee Ali Hassan Mwinyi ililiua Azimio la Arusha na Ujamaa wake. Azimio hili lilibeba matarajio ya usoni na mustakabali wa Watanzania. Azimio lilipouawa lilikufa na ndoto za Watanzania kujiletea maendeleo na kuwarejesha Watanzania mikononi mwa wakoloni mamboleo.
Kaburi lake liko Zanzibar lakini Watanzania hawakuruhusiwa kuweka matanga wala kupata siku za mapumziko ya maombolezo kitaifa. Mzee Mwinyi yuko hai hadi leo, historia inamhukumu akiwa hai, kuwa kwa mkono wake, Azimio la Arusha lilihukumiwa adhabu ya kifo bila rufaa.
Kifo cha Azimio la Arusha kilidhoofisha kinga ya mwili wa Taifa letu na kwa hiyo likaanza kushambuliwa na magonjwa ya ajabu kila wakati. Bila kinga madhubuti mwilini, taifa lilishambuliwa na dumuzi kila kona na maghala ya taifa yakaishiwa akiba yote.
Awamu ya tatu ilipoingia ilikuta Ikulu ni sawa na mahame au shamba la mahindi lililoshambuliwa na nyani wenye njaa.
Awamu ya tatu chini ya Benjamin Mkapa ilimuumiza muasisi wa Taifa letu. Muasisi wa Taifa letu ndiye muuaji wa ukoloni na fundi msanifu wa Azimio la Arusha. Mara kadhaa, Baba wa Taifa alisimama hadharani kuomboleza kifo cha Azimio la Arusha kwa uchungu na machozi. Hakuwahi kumaliza hotuba yoyote, iwe ya birthday au ya rambirambi za msiba fulani bila kuzungumzia Azimio la Arusha.
Mwalimu alienda kanisani na Azimio la Arusha, alisafiri ndani na nje akiwa nalo. Lilipouawa alipata kihoro kilichoharakisha kifo chake.
Alipopiga kelele, aliwakera watawala. Wakamnyima chakula, matibabu, usafiri na mawasiliano. Alipogoma kwenda hospitali ili afe haraka, walimlazimisha kwenda asipotaka kwenda. Waliondoa walinzi, madaktari na kimsingi wakazuia hata wageni wa kumtembelea. Alipolazwa hospitali hawakuwapa nafasi madakatari wake waeleze maendeleo ya matibabu yake. Watawala waligeuka madaktari wake na kuanza kueleza Watanzania kwa nini Mwalimu hawezi kupona badala ya kwa nini amewahi mno kufa. Walilia na kuweka viapo vya ajabu juu ya kaburi lake. Mwalimu aliwapenda upeo, wakamjibu kwa misumari kwenye jeneza lake.

Awamu ya nne imeanza kuua. Chini ya Jakaya Mrisho Kikwete, kisu kiko shingoni mwa CCM na kichwa chake kimeelekezwa kibra tayari kwa kuchinjwa. Katibu Mwenezi Nape Nnauye anashangilia kuwa anayechinjwa ni CHADEMA lakini anahitaji miwani ya aina nyingine kuliko aliyo nayo. Ni kudra za Mwenyezi tu zinazoweza kubadili mwendokasi wa CCM kufia mikononi mwa Kikwete. Aliingia madarakani kwa rushwa, rushwa hiyo ikaziba macho na masikio yake.

Mafisadi wakaweka kitanzi shingoni mwake. Akifurukuta wanavuta kamba, akikosa hewa wanalegeza, muafaka unapatikana. Kauli mbiu zote duniani ametumia kukipa chama uhai, imeshindikana. Aliingia kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya.
Masikio yalipoichoka akaja na "Maisha bora kwa kila Mtanzania". Aliposhtukiwa, akapaka rangi kauli mbiu ya awali na kuja na "Kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi". Chini ya utawala wake kila kitu kinawezekana na hapo hapo hakitendeki. Tanzania bila maralia inawezekana, Tanzania bila ukimwi inawezekana, Tanzania bila rushwa inawezekana, madarasa yenye kompyuta yanawezekana, taxi mpaka Mtwara inawezekana, na uchumi unaopaa bila kubadili hali za watu unawezekana.

Jamhuri yetu imejaa wanasiasa na watawala. Wanasiasa ambao Plato alidai wanapenda kuongoza lakini hawajui kuongoza. Jamhuri yetu ina watawala ambao sayansi ya siasa inasema hawapendi kugawana madaraka na watu wengine ingawa wakiondoka madarakani wanadai haki ya kugawana madaraka. Jamhuri yetu haina viongozi walio tayari kuongoza kwa mifano.
Tuna watawala wanaojiita viongozi lakini hawana usalama wakati wote na ndiyo maana wanatumia kila njia kubaki madarakani. Wako tayari kuiba, kuua, kudanganya, kutukana, kutisha na hata kufanya usanii, ili kubakia madarakani.
Kwa mtindo huu, tutarajie nini katika awamu ya tano ya Jamhuri yetu? Nini kitauawa katika awamu hiyo? Utaifa wetu? Taifa letu?

Kiongozi hii mada imetulia, tena imetulia vizuri sana. Mara nyingi napenda waandishi muwe mnaandika makala kama hizi makala ambazo ukisoma unapenda kuirudia kuisoma, makala ambazo ukisoma unaweza kuunganisha habari na kutabiri yajayo. Hii kwa kweli ni nzuri, si zile za Megawati.....Hongera Kiongozi.
 
Kwanza mi huwa sisomi magazeti ya aina hii hasa Raia Mwema coz dhahiri ni ya uchochezi,haiwezekani wao kila toleo lazima kuwe na jina JK,bora walifungie tu
 
Hili si kufungiwa tu, inafaa wachukuliwe hatua za kisheria kali sana, na wapelekwe mahakamani, mhariri na muandishi wa hiyo makala, na wakishindwa kuthibitisha hizo kauli zao, wafungwe maisha. Hawa ni watu hatari sana na wanaweza kusababisha maafa makubwa sana kwa huu uzandiki wao.
Kwa makosa gani ndugu yangu? Ushahasahu kuwa siku hizi serikali zinaogopa kufungia magazeti na kuwakamata waandishi kwa sababu malalamiko yatasikika dunia nzima? Kama ripoti si kweli mwambie Salva asute. Enzi za kamatakamata zilishapitwa na wakati, ama mtajikuta mmepelekwa Hague. Makala tumeisoma mbona sijaona mtu anahatarishiwa maisha yake?
 
RaiaMwema halitafungiwa, naona Hii barua naona ni mtego wa kumtafuta huyo mwandishi anayejiita Msomaji Raia; hapa Wahariri watabanwa mbavu hadi watamsalimia huyu mpiganaji na baada ya hapo utasikia kesi kama za akina Mwigamba na TzDaima.

Mwisho wa yote huwa ni compromise na mafisadi, bado tunakumbuka jinsi jamaa hawa hawa wa RaiaMwema walivyoiuza Rai kwa mafisadi miaka ya 2006/7
 
kwa ujumla watawala inaonekana wanataka kutuaminisha kuwa mtu akisema ukweli kuhusu masuala yanayowahusu basi watayaita uchochezi. Cha kujiuliza ni kwa nini wanansema huu ni uchochezi? Isije ikawa ni suala la muono/mtazamo wao tu na si vinginevyo.
 
Ukimsoma Msomaji raia, utagundua kuwa ni mtu yuko kwenye inner circle, makala ya juzi ilikuwa ni ya kwanza baada ya kuwa nje muda mrefu kwa matibabu, je huyu jamaa ni nani?

kwa hakika ukisoma utajua ni mwakyembe!
 
Kwanza mi huwa sisomi magazeti ya aina hii hasa Raia Mwema coz dhahiri ni ya uchochezi,haiwezekani wao kila toleo lazima kuwe na jina JK,bora walifungie tu
wewe lazima la kwako ni uhuru, mzalendo, jamboleo au tazama tanzania! yoooye lazima yamtukane slaa!
 
attachment.php
 
HAYA WADAU MAKALA YENYEWE NDOO HIIO

Kila Awamu ina Rekodi ya Kuua

Msomaji Raia

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete…

KAMPENI za uchaguzi mdogo jimboni Arumeru Mashariki zitakumbukwa kwa mengi. Kuna rekodi muhimu zimewekwa na zitakumbukwa.
Kura za maoni zilirudiwa mara mbili ndani ya CCM. Pamoja na malalamiko ya wazi juu ya matumizi ya rushwa, Kamati Kuu ya CCM iliamua kurudiwa kwa uchaguzi huo na hatimaye mtuhumiwa mkuu wa utoaji rushwa akapitishwa na Kamati Kuu.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ambaye hakukubaliana na uteuzi amenukuliwa akisema kwa utani kuwa, "hatukuridhika na rushwa katika awamu ya kwanza, tukaagiza ahonge zaidi awamu ya pili ndipo apitishwe".
Makeke ya TAKUKURU yalikoishia ni wao tu wanaweza kueleza. Kuna wasiwasi kuwa walipokuwa na makeke walikuwa hawajapata mgawo wao. Huwezi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, kisha ukamkamata mjumbe mwenzako wa kamati hiyo.
Rekodi nyingine ilikuwa ni ya mapingamizi dhidi ya wagombea. CCM ilianzisha mtindo huo pale wagombea wake walipomwekea mgombea mwenzao kuwa si raia wa Tanzania. Pingamizi hili lilipuuzwa lakini likaibuliwa na CHADEMA kabla halijatupwa na kukatiwa rufaa mbele ya Tume ya Uchaguzi. Tume hiyo ililitupilia mbali japokuwa kuna maelfu ya Watanzania wananyimwa pasi ya kusafiria kwa sababu hiyo hiyo ya kuzaliwa nje ya nchi. Rekodi na ushahidi umewekwa kuwa, ukiwa ndani ya CCM lolote linawezekana.
Rekodi nyingine ni ya matumizi ya matusi katika kampeini. Chama cha Mapinduzi kiliasisi mtindo huo na CHADEMA kufuatia kwa njia ya kujibu vijembe na matusi hayo. Rais Mkapa atakumbukwa kwa kuzindua mtiririko huo wa matusi na vijembe vilivyochukua nafasi ya sera na mikakati. Enzi za CCM kukejeli kuwa vyama vya upinzani vinatumia matusi katika kampeini zimeisha. Ukienda mkutano wa CCM utajihisi uko mkutano wa wapinzani, na ukienda mkutano wa wapinzani, utadhani uko CCM ya Nyerere. Watu wamehojiana kuhusu ndoa zao, sura zao, kazi zao, urefu wao na ufupi wao.
Rekodi kubwa zaidi ilikuwa ni ya tuhuma ya kifo cha hayati Baba wa Taifa. Kwamba, Serikali ya Awamu ya Tatu ilimlazimishia kifo Baba yetu wa Taifa. Kama ni kejeli au kijembe si hoja. Cha msingi rekodi imewekwa kuwa Baba wa Taifa alikufa na kifo chake kiliacha mashaka makubwa.
Wahenga husema "hakuna utawala usioua". Yaelekea kila awamu ya Taifa letu imeua kitu fulani. Baba wa Taifa na Awamu yake ya Kwanza aliua ukoloni. Ni sahihi kuwa Baba wa Taifa alipanga, akaamua na kutekeleza mpango mahsusi wa kuua ukoloni mkongwe na hatimaye akajitahidi kuupa sumu ukoloni mamboleo.
Hata watoto wetu wanaojifunza historia na uraia wanalijua hilo, kuwa Rais Julius Kambarage Nyerere aliuua ukoloni, Tanzania ikawa huru. Tarehe, mwezi na mwaka vinajulikana. Tumesherehekea nusu karne hivi karibuni.
Awamu ya pili chini ya Mzee Ali Hassan Mwinyi ililiua Azimio la Arusha na Ujamaa wake. Azimio hili lilibeba matarajio ya usoni na mustakabali wa Watanzania. Azimio lilipouawa lilikufa na ndoto za Watanzania kujiletea maendeleo na kuwarejesha Watanzania mikononi mwa wakoloni mamboleo.
Kaburi lake liko Zanzibar lakini Watanzania hawakuruhusiwa kuweka matanga wala kupata siku za mapumziko ya maombolezo kitaifa. Mzee Mwinyi yuko hai hadi leo, historia inamhukumu akiwa hai, kuwa kwa mkono wake, Azimio la Arusha lilihukumiwa adhabu ya kifo bila rufaa.
Kifo cha Azimio la Arusha kilidhoofisha kinga ya mwili wa Taifa letu na kwa hiyo likaanza kushambuliwa na magonjwa ya ajabu kila wakati. Bila kinga madhubuti mwilini, taifa lilishambuliwa na dumuzi kila kona na maghala ya taifa yakaishiwa akiba yote.
Awamu ya tatu ilipoingia ilikuta Ikulu ni sawa na mahame au shamba la mahindi lililoshambuliwa na nyani wenye njaa.
Awamu ya tatu chini ya Benjamin Mkapa ilimuumiza muasisi wa Taifa letu. Muasisi wa Taifa letu ndiye muuaji wa ukoloni na fundi msanifu wa Azimio la Arusha. Mara kadhaa, Baba wa Taifa alisimama hadharani kuomboleza kifo cha Azimio la Arusha kwa uchungu na machozi. Hakuwahi kumaliza hotuba yoyote, iwe ya birthday au ya rambirambi za msiba fulani bila kuzungumzia Azimio la Arusha.
Mwalimu alienda kanisani na Azimio la Arusha, alisafiri ndani na nje akiwa nalo. Lilipouawa alipata kihoro kilichoharakisha kifo chake.
Alipopiga kelele, aliwakera watawala. Wakamnyima chakula, matibabu, usafiri na mawasiliano. Alipogoma kwenda hospitali ili afe haraka, walimlazimisha kwenda asipotaka kwenda. Waliondoa walinzi, madaktari na kimsingi wakazuia hata wageni wa kumtembelea. Alipolazwa hospitali hawakuwapa nafasi madakatari wake waeleze maendeleo ya matibabu yake. Watawala waligeuka madaktari wake na kuanza kueleza Watanzania kwa nini Mwalimu hawezi kupona badala ya kwa nini amewahi mno kufa. Walilia na kuweka viapo vya ajabu juu ya kaburi lake. Mwalimu aliwapenda upeo, wakamjibu kwa misumari kwenye jeneza lake.

Awamu ya nne imeanza kuua. Chini ya Jakaya Mrisho Kikwete, kisu kiko shingoni mwa CCM na kichwa chake kimeelekezwa kibra tayari kwa kuchinjwa. Katibu Mwenezi Nape Nnauye anashangilia kuwa anayechinjwa ni CHADEMA lakini anahitaji miwani ya aina nyingine kuliko aliyo nayo. Ni kudra za Mwenyezi tu zinazoweza kubadili mwendokasi wa CCM kufia mikononi mwa Kikwete. Aliingia madarakani kwa rushwa, rushwa hiyo ikaziba macho na masikio yake.

Mafisadi wakaweka kitanzi shingoni mwake. Akifurukuta wanavuta kamba, akikosa hewa wanalegeza, muafaka unapatikana. Kauli mbiu zote duniani ametumia kukipa chama uhai, imeshindikana. Aliingia kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya.
Masikio yalipoichoka akaja na "Maisha bora kwa kila Mtanzania". Aliposhtukiwa, akapaka rangi kauli mbiu ya awali na kuja na "Kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi". Chini ya utawala wake kila kitu kinawezekana na hapo hapo hakitendeki. Tanzania bila maralia inawezekana, Tanzania bila ukimwi inawezekana, Tanzania bila rushwa inawezekana, madarasa yenye kompyuta yanawezekana, taxi mpaka Mtwara inawezekana, na uchumi unaopaa bila kubadili hali za watu unawezekana.

Jamhuri yetu imejaa wanasiasa na watawala. Wanasiasa ambao Plato alidai wanapenda kuongoza lakini hawajui kuongoza. Jamhuri yetu ina watawala ambao sayansi ya siasa inasema hawapendi kugawana madaraka na watu wengine ingawa wakiondoka madarakani wanadai haki ya kugawana madaraka. Jamhuri yetu haina viongozi walio tayari kuongoza kwa mifano.
Tuna watawala wanaojiita viongozi lakini hawana usalama wakati wote na ndiyo maana wanatumia kila njia kubaki madarakani. Wako tayari kuiba, kuua, kudanganya, kutukana, kutisha na hata kufanya usanii, ili kubakia madarakani.
Kwa mtindo huu, tutarajie nini katika awamu ya tano ya Jamhuri yetu? Nini kitauawa katika awamu hiyo? Utaifa wetu? Taifa letu?

lazima aliyeandika barua kwenda raia mwema ni punguani! Mtu analilia Taifa na mstakabali wake nyie mko kwenyeichochezi!
 
QUOTE=Mzizi wa Mbuyu;3583122]Mimi nikifikri zaidi na zaidi.......
Wala makala hii si sababu, sababu ni Ulimwengu. Siku hizi ameanza kurusha makombora ya hapa na pale kwa JK, mengine yanaonekana kama kumdharirisha kabisa kwa mfano hivi karibuni aliandika kuwa raisi wa sasa ni kama anaomba Mungu kipindi chake kiishe tu maana hana kabisa mbinu yoyote ya kuiendeleza nchi!

Mhh! tusubiri![/QUOTE]
Ndio ukweli wenyewe..
 
Nadhani kuna haja huko mbeleni kuwashughulikia huku mtaani watendaji wa namna hii iliwajue kuwa sisi wananchi ambao ndio waajiri wao hatukuwatuma kutumikia Mafisadi.

Pili nashindwa kuelewa ni kifungu ipi ya kanuni inayosimamia magazeti Bwana J.Zuberi anayotaka kuirejea ilikujenga hoja yake ya uchochezi.
Kwani ni UONGO UCHAGUZI WA 2010 ULIKUWA NA RUSHWA KUPINDUKIA!!!!!
Kwani ni UONGO AHADI YA MAISHA BORA HAIPO NA ILIKUWA UONGO !!!!! na mengineyo mengi .

Mwenye CV ya huyu Bwana JAMAL ZUberi aturushia humu.
 
Mwageni hiyo makala hapa.

Siku nyingine usome post za kabla yako....haya makala hio hapo

Kila Awamu ina Rekodi ya Kuua

Msomaji Raia

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete…

KAMPENI za uchaguzi mdogo jimboni Arumeru Mashariki zitakumbukwa kwa mengi. Kuna rekodi muhimu zimewekwa na zitakumbukwa.
Kura za maoni zilirudiwa mara mbili ndani ya CCM. Pamoja na malalamiko ya wazi juu ya matumizi ya rushwa, Kamati Kuu ya CCM iliamua kurudiwa kwa uchaguzi huo na hatimaye mtuhumiwa mkuu wa utoaji rushwa akapitishwa na Kamati Kuu.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ambaye hakukubaliana na uteuzi amenukuliwa akisema kwa utani kuwa, "hatukuridhika na rushwa katika awamu ya kwanza, tukaagiza ahonge zaidi awamu ya pili ndipo apitishwe".
Makeke ya TAKUKURU yalikoishia ni wao tu wanaweza kueleza. Kuna wasiwasi kuwa walipokuwa na makeke walikuwa hawajapata mgawo wao. Huwezi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, kisha ukamkamata mjumbe mwenzako wa kamati hiyo.
Rekodi nyingine ilikuwa ni ya mapingamizi dhidi ya wagombea. CCM ilianzisha mtindo huo pale wagombea wake walipomwekea mgombea mwenzao kuwa si raia wa Tanzania. Pingamizi hili lilipuuzwa lakini likaibuliwa na CHADEMA kabla halijatupwa na kukatiwa rufaa mbele ya Tume ya Uchaguzi. Tume hiyo ililitupilia mbali japokuwa kuna maelfu ya Watanzania wananyimwa pasi ya kusafiria kwa sababu hiyo hiyo ya kuzaliwa nje ya nchi. Rekodi na ushahidi umewekwa kuwa, ukiwa ndani ya CCM lolote linawezekana.
Rekodi nyingine ni ya matumizi ya matusi katika kampeini. Chama cha Mapinduzi kiliasisi mtindo huo na CHADEMA kufuatia kwa njia ya kujibu vijembe na matusi hayo. Rais Mkapa atakumbukwa kwa kuzindua mtiririko huo wa matusi na vijembe vilivyochukua nafasi ya sera na mikakati. Enzi za CCM kukejeli kuwa vyama vya upinzani vinatumia matusi katika kampeini zimeisha. Ukienda mkutano wa CCM utajihisi uko mkutano wa wapinzani, na ukienda mkutano wa wapinzani, utadhani uko CCM ya Nyerere. Watu wamehojiana kuhusu ndoa zao, sura zao, kazi zao, urefu wao na ufupi wao.
Rekodi kubwa zaidi ilikuwa ni ya tuhuma ya kifo cha hayati Baba wa Taifa. Kwamba, Serikali ya Awamu ya Tatu ilimlazimishia kifo Baba yetu wa Taifa. Kama ni kejeli au kijembe si hoja. Cha msingi rekodi imewekwa kuwa Baba wa Taifa alikufa na kifo chake kiliacha mashaka makubwa.
Wahenga husema "hakuna utawala usioua". Yaelekea kila awamu ya Taifa letu imeua kitu fulani. Baba wa Taifa na Awamu yake ya Kwanza aliua ukoloni. Ni sahihi kuwa Baba wa Taifa alipanga, akaamua na kutekeleza mpango mahsusi wa kuua ukoloni mkongwe na hatimaye akajitahidi kuupa sumu ukoloni mamboleo.
Hata watoto wetu wanaojifunza historia na uraia wanalijua hilo, kuwa Rais Julius Kambarage Nyerere aliuua ukoloni, Tanzania ikawa huru. Tarehe, mwezi na mwaka vinajulikana. Tumesherehekea nusu karne hivi karibuni.
Awamu ya pili chini ya Mzee Ali Hassan Mwinyi ililiua Azimio la Arusha na Ujamaa wake. Azimio hili lilibeba matarajio ya usoni na mustakabali wa Watanzania. Azimio lilipouawa lilikufa na ndoto za Watanzania kujiletea maendeleo na kuwarejesha Watanzania mikononi mwa wakoloni mamboleo.
Kaburi lake liko Zanzibar lakini Watanzania hawakuruhusiwa kuweka matanga wala kupata siku za mapumziko ya maombolezo kitaifa. Mzee Mwinyi yuko hai hadi leo, historia inamhukumu akiwa hai, kuwa kwa mkono wake, Azimio la Arusha lilihukumiwa adhabu ya kifo bila rufaa.
Kifo cha Azimio la Arusha kilidhoofisha kinga ya mwili wa Taifa letu na kwa hiyo likaanza kushambuliwa na magonjwa ya ajabu kila wakati. Bila kinga madhubuti mwilini, taifa lilishambuliwa na dumuzi kila kona na maghala ya taifa yakaishiwa akiba yote.
Awamu ya tatu ilipoingia ilikuta Ikulu ni sawa na mahame au shamba la mahindi lililoshambuliwa na nyani wenye njaa.
Awamu ya tatu chini ya Benjamin Mkapa ilimuumiza muasisi wa Taifa letu. Muasisi wa Taifa letu ndiye muuaji wa ukoloni na fundi msanifu wa Azimio la Arusha. Mara kadhaa, Baba wa Taifa alisimama hadharani kuomboleza kifo cha Azimio la Arusha kwa uchungu na machozi. Hakuwahi kumaliza hotuba yoyote, iwe ya birthday au ya rambirambi za msiba fulani bila kuzungumzia Azimio la Arusha.
Mwalimu alienda kanisani na Azimio la Arusha, alisafiri ndani na nje akiwa nalo. Lilipouawa alipata kihoro kilichoharakisha kifo chake.
Alipopiga kelele, aliwakera watawala. Wakamnyima chakula, matibabu, usafiri na mawasiliano. Alipogoma kwenda hospitali ili afe haraka, walimlazimisha kwenda asipotaka kwenda. Waliondoa walinzi, madaktari na kimsingi wakazuia hata wageni wa kumtembelea. Alipolazwa hospitali hawakuwapa nafasi madakatari wake waeleze maendeleo ya matibabu yake. Watawala waligeuka madaktari wake na kuanza kueleza Watanzania kwa nini Mwalimu hawezi kupona badala ya kwa nini amewahi mno kufa. Walilia na kuweka viapo vya ajabu juu ya kaburi lake. Mwalimu aliwapenda upeo, wakamjibu kwa misumari kwenye jeneza lake.

Awamu ya nne imeanza kuua. Chini ya Jakaya Mrisho Kikwete, kisu kiko shingoni mwa CCM na kichwa chake kimeelekezwa kibra tayari kwa kuchinjwa. Katibu Mwenezi Nape Nnauye anashangilia kuwa anayechinjwa ni CHADEMA lakini anahitaji miwani ya aina nyingine kuliko aliyo nayo. Ni kudra za Mwenyezi tu zinazoweza kubadili mwendokasi wa CCM kufia mikononi mwa Kikwete. Aliingia madarakani kwa rushwa, rushwa hiyo ikaziba macho na masikio yake.

Mafisadi wakaweka kitanzi shingoni mwake. Akifurukuta wanavuta kamba, akikosa hewa wanalegeza, muafaka unapatikana. Kauli mbiu zote duniani ametumia kukipa chama uhai, imeshindikana. Aliingia kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya.
Masikio yalipoichoka akaja na "Maisha bora kwa kila Mtanzania". Aliposhtukiwa, akapaka rangi kauli mbiu ya awali na kuja na "Kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi". Chini ya utawala wake kila kitu kinawezekana na hapo hapo hakitendeki. Tanzania bila maralia inawezekana, Tanzania bila ukimwi inawezekana, Tanzania bila rushwa inawezekana, madarasa yenye kompyuta yanawezekana, taxi mpaka Mtwara inawezekana, na uchumi unaopaa bila kubadili hali za watu unawezekana.

Jamhuri yetu imejaa wanasiasa na watawala. Wanasiasa ambao Plato alidai wanapenda kuongoza lakini hawajui kuongoza. Jamhuri yetu ina watawala ambao sayansi ya siasa inasema hawapendi kugawana madaraka na watu wengine ingawa wakiondoka madarakani wanadai haki ya kugawana madaraka. Jamhuri yetu haina viongozi walio tayari kuongoza kwa mifano.
Tuna watawala wanaojiita viongozi lakini hawana usalama wakati wote na ndiyo maana wanatumia kila njia kubaki madarakani. Wako tayari kuiba, kuua, kudanganya, kutukana, kutisha na hata kufanya usanii, ili kubakia madarakani.
Kwa mtindo huu, tutarajie nini katika awamu ya tano ya Jamhuri yetu? Nini kitauawa katika awamu hiyo? Utaifa wetu? Taifa letu?
 
kwa hakika ukisoma utajua ni mwakyembe!

Wapi alisema ameenda kwenye ,atibabu ww Mpanzi?..............Mwakyembe mhh sidhani hio sio staili yake ya uandishi....kwanza yuko bizze kupambana na Mafisadi wanaotaka kumnyofoa karoho kake ka ngama..
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom