Raia Mwema hatarini kufungiwa makala 'kila awamu ina rekodi ya kuua', mtego kwa JK

Ngoja na mm nikalitafute hilo gazeti sijalisoma siku nyingi
 
Kwa
sasa nilazima busaraitumike badala ya ubabe. Hii si ishara nzuri hatakidogo kwa fani ya uandishi wa habari. Tuwe makini sana.

nimeisoma makala hiyo. kimsingi mwandishi anasema awamu ya nyerere iliua ukoloni. hakuna baya hapo. awamu ya mwinyi iliua azimio la arusha. ni ukweli na hakuna ubaya kukumbusha. awamu ya mkapa mwalimu
aliomboleza kifo cha azimio hadi kuwakera watawala ambao walimnyima chakula matibabu usafiri na mawasiliano. kisha akapelekwa kutibiwa
asipopataka bila ulinzi wala madaktari wake. hapa ndipo tatizo linaanza na linakuwa kubwa anaposema awamu ya kikwete imeingia madarakani kwa
rushwa na imeanza kuiua ccm!!
 
Hivi ni kwanini Raia Mwema isimchukulie hatua za kisheria huyo Zuberi Jamal kwa kusababisha chuki miongoni mwa jamii dhidi ya gazeti huru kwa kuchukua mstari mmoja tu kama ndio msingi wa hoja nzima? Yaani gazeti zima aMEONA HUO MSTARI TU? NI WANGAPI WATAKUA NA UWEZO WA KUSOMA HUO MSTARI NA HIO MAKALA, BINAFSI NILINUNUA GAZETI HILO JANA LAKINI SIJAISOMA HIO MAKALA ZAIDI YA KUSOMA HEADING TU KAMA NI HIVYO KWENYE mWANAhALISI NAKO KUNA UGONJWA UMERIPOTIWA KULE UNAITWA oYSETRBEASISI sYNDROME NA Masakiasys
 
Jamani uchochezi ni mambo ya uongo, sasa hapo jambo la uongo ni lipi? mbona kweli tupu!

Leo nimesikia Mwanajeshi mmoja kapandishwa kizimbani kwa kesi ya kuua vichwa tano na nafikiri habari hiyo si ya kichochezi ila ni hapo tu tukijaribu kuuliza vipi Polisi kule Songea waliua na Serikali haikuwafikisha Mahakamani wahusika wote basi naona habari hiyo itakuwa ya kichochezi kwani inategemea mwandishi kama amekata sana na kagusa mfupa inakuwa uchochezi
 
Asenteni kwa taarifa, kweli uchaguzi arumeru unakwisha tupate vitu vya maana kama zamani
 
..sasa hao maelezo wanataka kubisha nini?

..kama wana ubavu waitoe in public ripoti ya uchunguzi ya Tume ya maadili ya CCM iliyoundwa na Philip Mangula.
 
Mujwahuzia:
Ukweli daima unauma,mwandishi wa makala hii anachozungunza yupo sahihi kabisa wala sio uchochezi kwa Watanzania kwa vile kila mtu macho anayo anaona hivi mtu akiandika jamani nimefanya kazi lakini tajiri wangu hajanipatia haki yangu ni uchochezi kwa waliokuwanacho mfukoni????????? Azimio la Arusha limekufa ni kweli sio kweli???? je halikuwasaidia wanyonge wa nchi hiii ???? je walioliua Azimio walituomba watanzania tutoe maoni yetu juu ya kulifuta Azimio hilo??? walitutaka radhi kulifuta Azimio hilo?? jibu ni hapana Je kweli rushwa nchi hii hakuna???? Je ni kweli viongozi wa nchi hii hawajajisahau katika kutekeleza wajibu wao kwa Wtz??? vyote hivi vimekufa Je ni kweli Watanzania tunapata maisha Bora kama nyimbo zinavyoimbwa kila siku redioni Magazetini, Mikutanoni????????? nini kosa la mwandishi huyu au wewe mwenzetu Msajili wa Magazeti Unajipendekeza upate CHEO?????? ni upi ukweli unaotaka uadikwe na gazeti hili wananchi wazisome. Polisi mmoja huko mkoani Morogoro kaua wananchi 3 kwa bunduki, Mwandishi anaandika tukio kamanda anasema hiyo ni ajali kama magari yanavyogongana je kiongozi huyu aliyekabidhiwa jukumu la kulinda Raia yupo sahihi??? na matamshi yake hayo?? Mwandishi wa gazeti asiandike matamshi ya mkubwa huyo kuwa sio sahihi??? Rais karuka na ndege kwenda Ulaya lakini huku nyuma Madakitari wamegoma kisa wanadai Posho zao huo ni chochezi????? Usijipendekeze watanzania sasa hivi tuna hali mbaya sana ya maisha kupita wakati wowote tangu Uhuru wetu mwaka 1961 inawezekana ulikuwa ujazaliwa kuona neema iliyokuwepo.
 
Kuna mwenye nakala laini ya hiyo makala atubandikie hapa nsi tusome? Raia mwema ya jana iliisha mapema sana mitaani
 
Barua imeandikwa 28 Machi 2012 ikitika maelezo kesho yake. Kwa nini wasito muda wa kutosha kwa Mhariri kuandika hayo maelezo? Inawezekana kukahitajika hata viambatanisho lakini kwa muda huo sijui wanataka kukomoa tu!!
 
Imebidi nipitie Stori nzima kwenye gazeti, kila kilichoandikwa ni point sijaona sehemu yenye makosa, huyo Jamal either hajui kazi yake au katumwa.
 

Huyu Jamal Zuberi ndio nani? na anaishi wapi? ni Mtanzani halisi au mnunuaji uraia? Hicho anachokidai ni uchochezi ni kipi? Hivi jamani, hii serikali yetu inawatendaji wa namna gani jamani? Mimi kwa kweli nipo totally puzzled na watendaji wa Serikali ya Tanzania. Yaani kwa kweli sijui tena sijui kabisa ni watu wa namna gani.
 
Hii barua inaonesha kuwa watendaji wa wizara ni mambumbumbu na mazuzu, wakisoma kilichomo watatofautisha propaganda na ukweli. Hizo ofisi ni za UMMA siyo zao binafsi, wasizitumie watakavyo kujipendekeza kwa watawala na wananchi ambao tayari wameshachoka na maisha wanasubiri kauli za mapinduzi. Kamwe wakae wakijua chachu ya MSOMAJI Raia ishasambaa hapa nchini na itaenea zaidi ya moto wa PETROLI.
Washindweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
[h=1]Kila Awamu ina Rekodi ya Kuua[/h]
Msomaji Raia


Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete…


KAMPENI za uchaguzi mdogo jimboni Arumeru Mashariki zitakumbukwa kwa mengi. Kuna rekodi muhimu zimewekwa na zitakumbukwa.
Kura za maoni zilirudiwa mara mbili ndani ya CCM. Pamoja na malalamiko ya wazi juu ya matumizi ya rushwa, Kamati Kuu ya CCM iliamua kurudiwa kwa uchaguzi huo na hatimaye mtuhumiwa mkuu wa utoaji rushwa akapitishwa na Kamati Kuu.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ambaye hakukubaliana na uteuzi amenukuliwa akisema kwa utani kuwa, “hatukuridhika na rushwa katika awamu ya kwanza, tukaagiza ahonge zaidi awamu ya pili ndipo apitishwe”.
Makeke ya TAKUKURU yalikoishia ni wao tu wanaweza kueleza. Kuna wasiwasi kuwa walipokuwa na makeke walikuwa hawajapata mgawo wao. Huwezi kuwa mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, kisha ukamkamata mjumbe mwenzako wa kamati hiyo.
Rekodi nyingine ilikuwa ni ya mapingamizi dhidi ya wagombea. CCM ilianzisha mtindo huo pale wagombea wake walipomwekea mgombea mwenzao kuwa si raia wa Tanzania. Pingamizi hili lilipuuzwa lakini likaibuliwa na CHADEMA kabla halijatupwa na kukatiwa rufaa mbele ya Tume ya Uchaguzi. Tume hiyo ililitupilia mbali japokuwa kuna maelfu ya Watanzania wananyimwa pasi ya kusafiria kwa sababu hiyo hiyo ya kuzaliwa nje ya nchi. Rekodi na ushahidi umewekwa kuwa, ukiwa ndani ya CCM lolote linawezekana.
Rekodi nyingine ni ya matumizi ya matusi katika kampeini. Chama cha Mapinduzi kiliasisi mtindo huo na CHADEMA kufuatia kwa njia ya kujibu vijembe na matusi hayo. Rais Mkapa atakumbukwa kwa kuzindua mtiririko huo wa matusi na vijembe vilivyochukua nafasi ya sera na mikakati. Enzi za CCM kukejeli kuwa vyama vya upinzani vinatumia matusi katika kampeini zimeisha. Ukienda mkutano wa CCM utajihisi uko mkutano wa wapinzani, na ukienda mkutano wa wapinzani, utadhani uko CCM ya Nyerere. Watu wamehojiana kuhusu ndoa zao, sura zao, kazi zao, urefu wao na ufupi wao.
Rekodi kubwa zaidi ilikuwa ni ya tuhuma ya kifo cha hayati Baba wa Taifa. Kwamba, Serikali ya Awamu ya Tatu ilimlazimishia kifo Baba yetu wa Taifa. Kama ni kejeli au kijembe si hoja. Cha msingi rekodi imewekwa kuwa Baba wa Taifa alikufa na kifo chake kiliacha mashaka makubwa.
Wahenga husema “hakuna utawala usioua”. Yaelekea kila awamu ya Taifa letu imeua kitu fulani. Baba wa Taifa na Awamu yake ya Kwanza aliua ukoloni. Ni sahihi kuwa Baba wa Taifa alipanga, akaamua na kutekeleza mpango mahsusi wa kuua ukoloni mkongwe na hatimaye akajitahidi kuupa sumu ukoloni mamboleo.
Hata watoto wetu wanaojifunza historia na uraia wanalijua hilo, kuwa Rais Julius Kambarage Nyerere aliuua ukoloni, Tanzania ikawa huru. Tarehe, mwezi na mwaka vinajulikana. Tumesherehekea nusu karne hivi karibuni.
Awamu ya pili chini ya Mzee Ali Hassan Mwinyi ililiua Azimio la Arusha na Ujamaa wake. Azimio hili lilibeba matarajio ya usoni na mustakabali wa Watanzania. Azimio lilipouawa lilikufa na ndoto za Watanzania kujiletea maendeleo na kuwarejesha Watanzania mikononi mwa wakoloni mamboleo.
Kaburi lake liko Zanzibar lakini Watanzania hawakuruhusiwa kuweka matanga wala kupata siku za mapumziko ya maombolezo kitaifa. Mzee Mwinyi yuko hai hadi leo, historia inamhukumu akiwa hai, kuwa kwa mkono wake, Azimio la Arusha lilihukumiwa adhabu ya kifo bila rufaa.
Kifo cha Azimio la Arusha kilidhoofisha kinga ya mwili wa Taifa letu na kwa hiyo likaanza kushambuliwa na magonjwa ya ajabu kila wakati. Bila kinga madhubuti mwilini, taifa lilishambuliwa na dumuzi kila kona na maghala ya taifa yakaishiwa akiba yote.
Awamu ya tatu ilipoingia ilikuta Ikulu ni sawa na mahame au shamba la mahindi lililoshambuliwa na nyani wenye njaa.
Awamu ya tatu chini ya Benjamin Mkapa ilimuumiza muasisi wa Taifa letu. Muasisi wa Taifa letu ndiye muuaji wa ukoloni na fundi msanifu wa Azimio la Arusha. Mara kadhaa, Baba wa Taifa alisimama hadharani kuomboleza kifo cha Azimio la Arusha kwa uchungu na machozi. Hakuwahi kumaliza hotuba yoyote, iwe ya birthday au ya rambirambi za msiba fulani bila kuzungumzia Azimio la Arusha.
Mwalimu alienda kanisani na Azimio la Arusha, alisafiri ndani na nje akiwa nalo. Lilipouawa alipata kihoro kilichoharakisha kifo chake.
Alipopiga kelele, aliwakera watawala. Wakamnyima chakula, matibabu, usafiri na mawasiliano. Alipogoma kwenda hospitali ili afe haraka, walimlazimisha kwenda asipotaka kwenda. Waliondoa walinzi, madaktari na kimsingi wakazuia hata wageni wa kumtembelea. Alipolazwa hospitali hawakuwapa nafasi madakatari wake waeleze maendeleo ya matibabu yake. Watawala waligeuka madaktari wake na kuanza kueleza Watanzania kwa nini Mwalimu hawezi kupona badala ya kwa nini amewahi mno kufa. Walilia na kuweka viapo vya ajabu juu ya kaburi lake. Mwalimu aliwapenda upeo, wakamjibu kwa misumari kwenye jeneza lake.
Awamu ya nne imeanza kuua. Chini ya Jakaya Mrisho Kikwete, kisu kiko shingoni mwa CCM na kichwa chake kimeelekezwa kibra tayari kwa kuchinjwa. Katibu Mwenezi Nape Nnauye anashangilia kuwa anayechinjwa ni CHADEMA lakini anahitaji miwani ya aina nyingine kuliko aliyo nayo. Ni kudra za Mwenyezi tu zinazoweza kubadili mwendokasi wa CCM kufia mikononi mwa Kikwete. Aliingia madarakani kwa rushwa, rushwa hiyo ikaziba macho na masikio yake.
Mafisadi wakaweka kitanzi shingoni mwake. Akifurukuta wanavuta kamba, akikosa hewa wanalegeza, muafaka unapatikana. Kauli mbiu zote duniani ametumia kukipa chama uhai, imeshindikana. Aliingia kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya.
Masikio yalipoichoka akaja na “Maisha bora kwa kila Mtanzania”. Aliposhtukiwa, akapaka rangi kauli mbiu ya awali na kuja na “Kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi”. Chini ya utawala wake kila kitu kinawezekana na hapo hapo hakitendeki. Tanzania bila maralia inawezekana, Tanzania bila ukimwi inawezekana, Tanzania bila rushwa inawezekana, madarasa yenye kompyuta yanawezekana, taxi mpaka Mtwara inawezekana, na uchumi unaopaa bila kubadili hali za watu unawezekana.
Jamhuri yetu imejaa wanasiasa na watawala. Wanasiasa ambao Plato alidai wanapenda kuongoza lakini hawajui kuongoza. Jamhuri yetu ina watawala ambao sayansi ya siasa inasema hawapendi kugawana madaraka na watu wengine ingawa wakiondoka madarakani wanadai haki ya kugawana madaraka. Jamhuri yetu haina viongozi walio tayari kuongoza kwa mifano.
Tuna watawala wanaojiita viongozi lakini hawana usalama wakati wote na ndiyo maana wanatumia kila njia kubaki madarakani. Wako tayari kuiba, kuua, kudanganya, kutukana, kutisha na hata kufanya usanii, ili kubakia madarakani.
Kwa mtindo huu, tutarajie nini katika awamu ya tano ya Jamhuri yetu? Nini kitauawa katika awamu hiyo? Utaifa wetu? Taifa letu?








My take...awamu ya tano itaua wawekezaji na majambazi wote wanaopitia CCM, itawezekana tu kama CCM itaanguka 2015.....
 
Hawa watu wana matatizo sana,

Ngoja tuendelee kuwatazama ila wajue kuwa yana mwisho. Na mwisho wao wanautengeneza wenyewe kwa mikono yao!!
 
Back
Top Bottom