Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 579
Leo nilipita hapa Dar Wizara ya Habari kwa mambo binafsi, nikakutana na taarifa kwamba gazeti la Raia Mwema limeandikiwa barua kutishiwa kufungiwa. Nikadodosa, nikaambiwa ni kuhusu makala isemayo, "KILA AWAMU INA REKODI YA KUUA, Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete...." nikanunua gazeti na kuisoma na kuona ni nzuri na imeandikwa kitaalamu sana na mwandishi "Msomaji Raia" ambaye alipotea sana akielezwa kuwa nje ya nchi kwa matibabu kabla ya kurejea na kuanza kuandika na hii ilikuwa makala yake ya kwanza tokea augue.
Kabla hata ya kusoma na kuondoka Wizara ya Habari, nikasikia mmoja wa maofisa akisema maneno haya, "unajua hii ni hatari sana, maana itakuwa ni sawa na kuisambaza hiyo makala na si kuizuia. Hata wale ambao hawakuisoma sasa wataitafuta na kuisoma. Raia Mwema limekuwa makini katika kutushambulia na limetusaidia sana katika vita ya ufisadi, lakini sasa tukigombana nao, tutakuwa tunamharibia Rais (JK) badala ya kumsaidia, na kwa kutumia jina lake badala ya majina ya marais wote waliotajwa, tutazidi kumchonganisha na wananchi na hata na hao wastaafu na familia zake na tutaonekana ni wabinafsi na Rais ataonekana mbinafsi na anajitetea mwenyewe. Tumefanya kosa kuwaandikia barua, tungawaita tu tukazungumza nao."..... mzungumzaji huyo naona hakupata support yoyote na wenzake walioendelea na kazi zao hadi naondoka eneo hilo na kwenda kusima makala husika.
Nimemuomba mshikaji wangu wa Maelezo nakala ya barua akinipa nitairusha hapa. Wahusika hata ndani ya maelezo naomba watusaidie kuweka barua hiyo hapa kama hawatojali. Nasikia kosa lao ni kusema JK CCM itamfia mikononi kwa kukuthiri kwa ufisadi ndani ya CCM tokea mchakato wa 2005 na ndio maana anapata kigugumizi kuwashughulikia.
Maoni yangu;
Ni kweli kwamba gazeti la Raia Mwema limekua likiegemea sana upande wa JK hasa katika vita inayoendelea ndani ya CCM kati yake na mafisadi na sitoshangaa kusikia kwamba huo ni mkakati wa mafisadi kulidhibiti ama kulichonganisha na JK na hapo watakuwa wamefanikiwa mambo yao, kwani vyombo vingi wameshavishika ama kupandikiza watu. Sitoshangaa maana hata TBC iko mikononi mwa mafisadi na mambo yao huwa yanaenda kiulaini kuliko hata watawala.