RAIA MWEMA: Bastola ya kigogo UVCCM yatoboa tumbo mwanafunzi wa CBE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAIA MWEMA: Bastola ya kigogo UVCCM yatoboa tumbo mwanafunzi wa CBE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Dec 21, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot] [/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]

  WANAJAMVI WENZANGU:


  Kuna hii stori katika Raia Mwema le ukurasa wa 3 ambayo naona vyema ni-share nayni, na hasa iwapo kama kuna mtu analifahamu tukio hili na ni nani huyo kigogo wa UVCCM.  Bastola ya kigogo UVCCM yatoiboa tumbo mwanafunzi wa CBE.

  [FONT=&quot] [/FONT]


  Na Mwandishi wetu.  Bastola ya kigogo wa makao makuu ya UVCCM mjini Dar es Salaam imemjeruhi tumboni mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Raia Mwwema imeelezwa.

  Habari za uhakika zinaeleza kwamba mtu mmoja anayetajwa kuwa dereva wa kigogo huyo, alikwaruzana na mwanafunzi huyo Emmanuel James (30) eneo la Sinza Mugabe karibu na Hoteli ya City Style.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, wakati wa tukio hilo kigogo huyo hakuwepo kwenye gari ambalo aliacha bastola yake na dereva aliitumia kuwafyatulia risasi vijana waliomhoji sababu ya kuwamwagia maji machafu.


  “Baada ya vijana hao kupiga kelele za kwa nini wamemwagiwa maji machafu, dereva huyo alipaki gari na kuanza kuwafokea vijana hao na walipojibizana naye alifyatua risasi mbili hewani na baadaye moja kumlenga tumboni Emmanuel James,” kinaeleza chanzo cha habari.

  Tukio hilo ambali limertokea saa saba usiku wa Novemba 30 2011 limeibua maswali mengi baada ya kuwapo taarifa za kutokamatwa kwa wahusika wala silaha iliyotumika katika tukio hilo.

  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa (kipolisi) Kinondoni, Camillus Wambura, hakuwa katika nafasi ya kuzungumzia tukio hilo kutokana na kuwa katika majukumu mengine ya kitaifa.


  Juhudi za kumpata Emmanuel kujua hali yake na kueleza kuhusiana na tukio hilo hazikuweza kufanikiwa wiki hii, huku wahusika wakielezwa kutamba kutochukuliwa hatua zozote.

  Taarifa ya tukio hilo zimeripotiwa katika kituo cha polisi cha Urafiki Dar es Salaam ambako imeelezwa kwamba hadi sasa wamekuwa wazito kuwahoji wahusika na kufanya uchunguzi zaidi kuhusu silaha iliyotumika.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ama kweli... yaani mtu kuhoji tu kwa nini kamwagiwa maji machafu ndo itolewe bastola?
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hatuwezi tukawa mahakimu hapa hadi hapo tutakapopata ushahidi wa pande zote mbili. Hadi wakati huo naomba hii thread isichangiwe kitu.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Nchi ilianza kuharibika mara tu baada ya kujifanya kuwa na sisi tuna Second Amendment inayoturuhusu kuwa kumiliki silaha kiholela kama njugu. Sehemu nyingi za Ulaya hawana uhalali wa kumiliki silaha kioholela kama Marekani, na leo hii Tanzania nayo imekuwa kama Marekani kwenye upaned wa silaha. Matokeao yake zinatumika hovyo hovyo tu; na watu kuuwawa na kujeruhiwa bila sababu ya maana. Matukio ya mauaji au matishio ya kutumia bastola yamekuwa ya kawaida Tanzania Tangu Ditopile aue mtu, na baadaye kuachiwa huru na serikali yetu hadi hapo mwenyezi Mungu alipoingilia kati. Siku moja kuna mtu alimpiga mwenzake risasi ya kifuani kwa short range na kumwua papo hapo wakiwa kwenye baa, lakini kesi yake bado inasuasua. Tumesikia mastaa wacheza michezo ya kuigiza, watoto wa wakubwa, wanasiasa na watu wa kawaida tu wakitishia wenzao kuwapiga risasi bila hatua zozote kuchukuliwa dhidi yao
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Ushahidi utapatikanaje iwapo polisi wamelala? Tukisema mapolisi wetu wanaburuzwa kwa pua na vigogo wa CCM yanakuja maneno.
  Wanajamvi msimsikilize huyu magamba, changieni hii thread ili pengine huyo kigogo abainike.
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  This is a form of class struggle between those who have motorised vehicles and pedestrians!! Barabara zetu ni makorongo matupu hivyo basi wakati mvua ikinyesha kunakuwa na madimbwi makubwa ya maji barabarani na kwavile barabara zenyewe ni nyembamba magari yakipita sehemu za madimbwi hurusha maji; na kama watembea kwa miguu wakiwa karibu ya hayo madimbwi maji hayo huwafikia!! Sasa hapo dereva wa gari ana makosa gani; au walitaka alibebe hilo gari mgongoni? Ni juu ya waenda kwa miguu kuhakikisha kuwa wanakuwa mbali na madimbwi ya maji barabarani magari yanapopita.
   
 7. mirindimo

  mirindimo JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 522
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 60
  I hate this corrupted government na hizo siraha zitawarudia wao am just count down:alien:
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  utashangaa inapotezewa tu
   
 9. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  lipo tatizo pia la watu/mashahidi kutokuwa tayari kufika polisi kushirikiana nao kufanikisha upelelezi. Katika tukio hili walioona wenzie na James wanapaswa kutaja namba za hiyo gari ili kufanikisha utambuzi hatimaye ukamataji
   
 10. k

  kuzou JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mapinduzi yote ya arab world yalianzia Tunisia ambapo mchuuzi wa matunda aliporwa matunda yake,na askari wa manispaa walotaka rushwa,alijilipua kwa hasira na petrol na maandamano kufuatia kesho yake.VISA VIDOGO HIVI KAMA HICHO HAPO JUU NI HATARI KATIKA JAMII ILOCHOKA
   
 11. K

  Kibori Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa huyu kigogo ndio nani ?
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sheria za nchi zinapogeuka kuwa ni ya kutumika kwa akina wale ndio uozo wote wa serikali unapodhihirika wazi. Who heartlessly pulled the triger on young Emmanuel's stomach and why?
   
 13. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyu mwandishi pia anaweza kusaidia kumbaini mtenda kosa pamoja na majeruhi wale walioshuhudia wakati tendo linatendeka
   
 14. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,112
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Mashahidi wanaogopa unajua tena utakapotoa ushahidi, basi kesi litakugeukia ww. Ila nawashauri kama ni bora hata wakaandika hizo no za gari kwa kutumia hili jukwaa halafu wahusika watajulikana tu
   
 15. W

  WILLS Member

  #15
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nduguyangu bulesi unakosea unavyosema kuwa, dereva hakuwa na kosa..maana angetumia ustaarabu tuu..yasingetokea yote ayo..
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nyie hamjui kwamba siku hizi bongo dereva wa kigogo nae ni kigogo....!yani kila mtu mkubwa bongo
   
 17. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  raia mwema nao siku hizi halina tofauti na magazeti yale ya marangi rangi.
  Hii habari sasa tuiweke ktk fungu gani kama si fungu la udaku?....puumbav
   
 18. k

  kijukuu kindo Member

  #18
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi maelezo yako yanajustify dereva kutumia bastola na kujeruhi watu? Halafu unahoji eti dereva ana kosa gani? Wewe kumbe bure kabisa! Wanaokutegemea unawashauri nini?Mijitu mingine hovyo!!.
   
 19. R

  Rev J Member

  #19
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bulesi huna lolote ujualo,mtu akihoji juu ya kosa lako ndo umfyatulie risasi.Nina wasiwasi na upeo wako wa kufikiri,nibora kutochangia chochote kama huelewi mambo kuliko kuchangia FYONGO NA UPUPU kama huo.Huna maana hata chembe,nashauli ukaombewe uwe na hekima na busara.
   
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Kama kesi ipo mahakamani tusijadili mwenendo wa kesi, lakini tunaweza kujadili suala la bastola ya kigogo ilivyotumika kutoboa tumbo la mwanafunzi.
   
Loading...