Raia Mpenda Misifa: Ukiambiwa umefanana na mtu wa usalama usifurahie. Hiyo sio sifa nzuri. Unaweza ukadhurika kwa bahati mbaya (Mistaken Identity)

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu yangu;

Mtanzania Raia Mpenda Misifa: Ukiambiwa umefanana na mtu wa usalama wa taifa usifurahie wala kuchekelea. Hiyo sio sifa njema hata kidogo. Unaweza ukadhurika au kuuwawa kwa bahati mbaya (Mistaken Identity);

Huko mtaani mnapoishi kuna watu ambao ni hatari sana kwa ustawi wa Tanzania yetu. Huko mnaishi na majambazi, magaidi (kama wale wa Mkuranga, Kibiti na Rufiji), wezi, vibaka, wauza mihadarati (bangi, gongo) ambao wote hao hawawapendi watu wa usalama wa nchi hata kidogo.

Nimeamua kuliongelea hili suala leo kwa maana kwamba, kwa siku za hivi karibuni kumeibuka na wimbi kubwa sana la vijana wenzangu wanaopenda kujitambulisha kuwa wao ni watu wa kwenye system kwa lengo/minadi ya kujitafutia umaarufu pamoja na sifa huko mitaani, mbele ya kadamnasi na wanawake warembo. Wengine wameenda mbali zaidi wakijitambulisha kuwa wao ni watumishi wa usalama wa taifa kwa lengo la kutaka kufanya utapeli jambo ambalo sio sahihi kabisa.

Soma thread hii hapa: Watu wanahisi mimi ni usalama wa taifa, naombeni ushauri

KISA KIDOGO CHA WATU WA USALAMA WA MOSSAD WALIVYOMUUA MTU KWA KUMFANANISHA (MISTAKEN IDENTITY)
===========
Miezi tisa baada ya tukio la Munich, July 1973 majasusi wa Mossad walipewa taarifa na mashushu wao wa Ulaya kuhusu uwepo wa Ali Hassan Salameh huko mjini Lillehammer, kaskazini mwa Norway.

Michael Harari, aliyekuwa msaidizi wa Zvi Zamir alichukua vijana wake wa kazi na kwenda nchini Norway.

Siku chache baadaye, mkurugenzi wa Mossad Zvi Zamir alijiunga na timu hiyo. Ilikuwa ni utamaduni wa wakuu wa vyombo vya dola wa Israel kuwepo mstari wa mbele wakati wa kazi maalum.

Zamir alifuata utamaduni huo huo na kufika nchini Norway ili kumuua Ali Hassan Salameh. Kwa masaa mengi walimfuatilia mtu waliyeamini ni Salameh.

Ilikuwa usiku, lakini binti mmoja aliyeitwa Marianne Gladnikoff, aliyeletwa na Michael Hariri kwenye timu hiyo ya Mossad alishtuka akasema mtu yule hakuwa Salameh, wakampuuza.

Walipomfuatilia hadi sehemu muafaka, Vijana wa Mossad waliofunzwa mahususi kwa kuua, walirusha risasi na kumuua mtu yule, bila kumjeruhi mwanamke aliyekua akitembea naye barabarani.

Kisha wauaji walirudi hadi jijini Oslo na kujificha kwenye nyumba salama. Hakukuwahi kufanyika mauaji katika mji wa Lillehammer kwa miaka 40, kwa hiyo ilikuwa tukio la ajabu sana kwa wakazi wa mji huo.

Lakini kesho yake iligundulika kuwa, aliyeuawa sio Ali Hassan Salameh, na mtu mwenye jina hilo hakuwepo nchini Norway.

Ilikuwa ni pigo kwa Mossad, lakini pigo kubwa lilikuwa kukamatwa kwa timu yote iliyohusika na mauaji yale, isipokuwa Mkurugenzi Zamir na msaidizi wake Harari ambao walitoroka kwa njia zao binafsi kurudi Israel.

Zamir alitumia boti maalum iliyoandalia na muisrael aishiye Norway ,ambaye ni wakala malum wa Mossad.

Jamii ya kimataifa ilishangaa, kwamba Mossad inayosifika kwa ufanisi wake imefanya makosa ya kijinga. Lakini zaidi timu iliyohusika na mauaji hayo ilishindwa kujificha na hivyo kukamatwa kirahisi na polisi wa Norway.

Pamoja na makosa mengime, kosa la kijinga walilofanya ni kutumia usafiri wa kukodi, badala ya kutumia usafiri wa umma.

Serikali ya Israel haikuwahi kukubali hadharani kuhusika na tukio hilo, lakini ilizungumza na serikali ya Norway namna ya kwasaidia raia wake waliokamatwa huko Norway.

Ahmed Bouchiki, raia wa Moroko aliuawa na Mossad kwa kufananishwa na Ali Hassan Salameh.
=======

Hii story niliisoma mwaka 2008 katika moja ya vitabu vyangu vingi nikiwa bado chuoni mwaka wa 2 pale IFM.

Kama raia mwema unaweza ukashiriki katika usalama wa taifa lako kwa kutoa ushirikiano kuanzia ngazi ya mjumbe, serikali ya mtaa wako au ikiwezekana toa taarifa hata kituo kidogo cha polisi kilicho karibu yako pindi uonapo dalili ama vitendo vya uvunjifu wa amani.

Usalama na ustawi wa nchi hii ni jukumu la kila mtanzania, mzalendo anayeilipenda taifa lake kwa dhati na moyo mmoja.

Tupo watanzania takribani milioni 50 sasa, jenga picha kila mmoja akitimiza wajibu wake ipasavyo nchii hii itakuwa mbali kiasi gani?

Kuwa mtu wa usalama wa taifa ni pamoja na kuweza kuhamasisha vijana wenzako hapo mtaani/kijijini unapokaa kuunda vikundi vya upandaji wa miti pamoja na kutunza mazingira.

Kuwa mtu wa usalama wa taifa ni pamoja na kukusanya vijana wenzako na kuwapa elimu ya afya (ulevi/mihadarati) na usalama barabarani hivyo kuwafanya kuwa maderava wazuri wa bodaboda watakaoepusha ajali za kizembe na wanaojitambua wasiovuta bangi wala kunywa gongo.

Unakuta kijana anatamani kufanya kazi TISS au kuwa askari Jeshi lakini wanafunzi wa secondary na primary wanapewa mimba na wahuni mtaa anapoishi anashindwa kwenda kutoa taarifa ofisi ya serikali ya mtaa, kwa mjumbe au hata kituo cha police kilicho karibu yake.

Wahusika watajueaje kama una mapenzi mema na taifa lako bila kuona matendo ya kizalendo?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Huu ushauri unawahusu sana vijana wapenda misifa mijini.

Ukimwambia anafanana sana na watu wa kitengo/usalama, basi lazima achekelee sana kwa furaha.

Wahalifu wakubwa huko mitaani watawadhuru ki makosa (Mistaken Identity)
 
Huo ni ukweli ambao wengi hawaujui au hawauoendi. Hakuna jambo la kiboya kama kufananiana na watu wa hizo kazi
Upo sahihi sana mkuu.

Mimi hii trend nilianza kuiona muda mrefu sana mkuu, hususan kwa ndugu, jamaa na rafiki zangu ninaokutana nao mara kwa mara.

Unakuta mtu amenyoa kichwani kama askari (Crew Cut) kisha mustache amenyoa kama Police, alafu amechomekea mkanda nje kama boss fulani hivi na kuanza kuwadanganya watu kuwa yupo kwenye system.

Niliwahi kuwaambia kuwa hii ni hatari sana kwa maisha yao na wasidhanie kuwa ni sifa nzuri hata kidogo.
 
Hao usalama wenyewe njaa tupu.

Kwa asiyewajua atajinasibu nao.

Ila nao njaa tu

Majungu mengi huko.


Labda wanaokuwa katika misafara ya waongozi wanaposho yao nono.

Mbali na hapo hamna ishu kubwa sana hiko usalama wa taifa,ni kawaida tu kama watu wengine.
 
Unawaita njaa tupu wakati panya road walivyoibuka mkawa mnaomba msaada wao?

Acha kukejeli kazi za watu.
Njaa tupu maana yake hawafanyi kazi yao au ?

Njaa tupu maana yake nakusidia ni kazi ya kawaida sio kwamba ina mpunga mnene kwa hawa usalama wadogo wadogo

Njaa tupu haina maana kuwa hawafanyi kazi.

Nasema hivyo kitokana na watu kutamani sana kuingia huko na kujifananisha nao ili waonekane matawi,ila kiukweli ni kazi ua njaa kama kazi zingine za polisi n.k hamna kikubwa

Au ulielewa vipi boss
 
Na hizo njaa zao ila si wanakulinda? Kwanini unawakejeli?
Kwani polisi na njaa zao hawatulindi ?

Polisi wanafanya kazi zao ila nao ni njaa kama kazi zingine.

Usalama nao hivyo hivyo mi njaa kama kazi zingine tu.

Watu wanadhani kuna mpunga mreeefu huko wanapata,ni njaa kama njaanzingine tu.

Nakubali njaa wanayo kama nilivyokuwa nayo mimi,na kazi wanafanya kama ninavyofanya mimi.

Sioni haja ya watu kujifanya wao ni usalama ili waonekane wana mpunga wakati uhalisia ni kuwa usalama wana njaa kali kama kazi zingine tu
 
vijana wa mtaani wanafurahi kufananishwa na maafisa upelelezi/TISS nk

wahusika
IMG_0370.jpg
 
Hakuna kazi anayofanya binadamu akiwa na wenzake pasipo kuwa na majungu.

Watu wanapokaa pamoja lazima changamoto zijitokeze, laa sivyo kaa peke yako.

Hata Lucifer alianzaisha majungu Mbinguni ndio maana akafukuzwa.
Bila shaka tunakubaliana hilo.

Nataka kuwaonesha kwamba hiyo ni kazi kama kazi zingine.

Kuna majungu kama kazi zingine.

Kuna njaa kama kazi zingine

Kuna kudharaulika kama kazi zingine.

Kwa hito hakuna haja ya vijana kujinasibu na usalama kwa kudhani kuwa wataonekana matawi na mpunga wa nguvu.
 
Back
Top Bottom