Raia Masikini Vs. Watawala Mafisadi..."Kesi Inayoiangusha Serikali Ya JK" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia Masikini Vs. Watawala Mafisadi..."Kesi Inayoiangusha Serikali Ya JK"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Jul 25, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mdogo Wangu Ridhiwani,Nakuandikia hii barua nikiwa na uchungu mkali sana. Nimekuwa mshabiki wako na ningependa kukuona ukipata nafasi nzuri ya uongozi ndani ya chama na serikali. Ndani ya UVCCM nilitegemea kwamba siku moja tungeungana kuleta mabadiliko ya kweli, lakini mdogo wangu umeniangusha. Kesi uliyopeleka mahakamani ni ni kesi ambayo siyo yako dhidi na Dr. Slaa au Rev. Mtikila, bali ni kesi ya Watawala dhidi ya raia masikini.Nasikitika sana, licha ya wewe mwenyewe kufahamu ukweli kwamba unamiliki mali nyingi ambazo hauwezi kuelezea chanzo chake, umediriki kwenda mahakamani kujishitaki wewe mwenyewe, mzazi wako, chama na serikali dhidi ya raia walala hoi.Umejishtaki mwenyewe na nguvu ya umma inakuja kukumaliza na serikali ya CCM. Mdogo wangu Ridhiwani, tangu umalize shule, haujawa na ajira ambayo unaweza kusema kwamba imekupa kiasi cha fedha ulizonazo. Ridhiwani unamiliki mali nyngi na za gharama kubwa

  -Toyota Land-Cruiser VX Mpya Nyeusi
  -Toyota Camry (mpya)
  -Toyota Harrier (mpya)
  -Hammer (mpya)
  -Mercedes ML (mpya)
  -Unamiliki maghorofa
  -Unamiliki vituo vya mafuta
  -Unamiliki mahoteli
  -Majumba matatu ya kifahari Dar...

  Listi ni ndefu mdogo wangu. Mbaya zaidi, umekuwa ukifanya biashara na Rostam Aziz, baba yako kamsaliti Rostam na hauna uhakika kwamba ni siri zako ngapi kazimwaga kwa wakina Mtikila. Ridhiwani nipo upande wako kwa maana kwamba msaidizi wa baba yako wa Zamani ambaye sasa ni mbunge wa bumbuli pia katoa ushahidi mwingi tu ambao hautaweza kujinasua. Kijana umekanyaga pabaya, nadhani umeamua kummaliza baba yako kisiasa. Hii kesi ndiyo chanzo ya kuanguka kwa JK, kwa maana kwamba, inaenda kufichua makubwa, jinsi watoto wa wenye madaraka wanavyotafuna nchi wakati raia wa kawaida masikini wanakufa na njaa. Mamillioni ya wanafunzi wanakaa ardhini, chini ya miti wakati wewe unazunguka na VX- ya millioni 250. Haki iko wapi? Mwisho wa siku raia wa kawaida wanakuja kudai haki yao... hela za wananchi unazovuja... kwa maana mshahara wako haufiki hata millioni 3 wakati unamiliki mabilioni ya fedha

  Mdogo wangu Ridhiwani, maandamano yataanzia pale mahakamani kumhukumu mzazi wako. Na wewe mwenyewe unajijengea na tayari umeshajijengea chuki kubwa katika jamii kutokana na hizi tabia zako. Utalazimika kutafuta maficho nje ya nchi, kwa sababu machafuko unayoyaanzisha wewe yatakukosesha amani ndani ya Tanzania. Ridhiwani, kutokana na machungu niliyonayo, nachelea kuitimisha maandiko yangu kwa siku ya leo. Kabla ya kwenda mahakamani, unegongea na baba yako kwanza. Umedanganyika na kuingia kwenye mtego na kamwe hautanasuka. Unafahamu fika jinsi chama chetu kinavyochukiwa na raia, muda wowote nchi inaweza kulipuka, sasa baada ya raia walalahoi kundua mali unazomiliki unadhani itakuwaje? Kuna mengi dhidi yako ambayo yanakuja kufichuka. Mimi mwenyewe nafahamu machache unadhani watu kwenye vyombo vya usalama wanafahamu mangapi? Umeiua CCM mdogo wangu
   
 2. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  jamani vipi
   
 3. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Ridhiwani ali disko mlimani mara mbili kwa hiyo mnaweza kutafakari
   
 4. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hapa Masha(Mbunge na waziri wa zamani serikalini ambaye ndo rafiki mkubwa wa huyu dogo na ni wanasheria)kafanya kazi yake,kamdanganya huyu dogo na sasa ndo ukweli utafahamika.
   
 5. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hakuna mwanzo usokua na mwisho,Ipo siku Mwenyezi mungu atakisikia kilio cha wa Tanzania inasikitisha sana kwakweli.
   
 6. G

  Giroy Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utamu wa pipi ni mate
   
 7. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Habari nzito hii.umesahau na viwanja!
   
 8. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  ndo kama hivyo
   
 9. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2013
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...