Raia kumiliki pingu si kosa - Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia kumiliki pingu si kosa - Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 17, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  JESHI la Polisi nchini limesema kuwa hakuna sheria inayokataza raia kumiliki pingu licha ya jeshi hilo kuwa na mwongozo wa utaratibu wa matumizi ya vifaa hivyo kwa askari wake. Aidha jeshi hilo limetoa mapendekezo serikalini ya kutungwa kwa sheria itakayozuia raia kumiliki kifaa hicho ambacho kinapaswa kimilikiwe na mamlaka zinazojihusisha na kuzuia na kuwashughulikia wahalifu.
  Ufafanuzi huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI), Robert Manumba, alipokuwa akijibu maswali ya wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini waliotaka kujua kama kuna sheria ya kuzuia raia kumiliki pingu.
  DCI Manumba alisema ni jambo la ajabu kwa raia kumiliki pingu kwa kuwa inazua maswali mengi kuwa anaitumia kwa matumizi gani hasa kwa kuwa si miongoni mwa mamlaka zilizopewa jukumu la kusimamia usalama wa raia na mali zao.
  Aliongeza kuwa jeshi hilo lilipata utata wa kumuwajibisha raia mmoja aliyepatikana na pingu kwa kuwa hakuna sheria zinazokataza raia kumiliki pingu lakini hivi sasa wataalamu wa jeshi hilo wamepeleka mapendekezo ya kutungwa kwa sheria hiyo.
  Alisema walijitahidi kupata maarifa kutoka kwa nchi nyingine juu ya raia kumilikii pingu ambapo walibaini utofauti kwani kuna nyingine zimekataa huku nyingine zikiruhusu
  “Wakati mwingine sheria haiwezi kuwekwa bila kuwepo kwa jambo fulani, sisi tulikuwa hatujawahi kupata raia mwenye kumiliki pingu lakini kwa kuwa imebainika kuna raia wanazimiliki, tumeomba sheria itungwe kuzuia raia kuzimiliki,” alisema.
  Naye Kamishna wa Operesheni Paul Chagonja, alisema katika mazingira ya kawaida kifaa cha pingi si silaha kwa raia hivyo yeyote anayebainika kukimiliki huushangaza umma hasa juu ya kazi anazozitumia.
  Katika hatua nyingine jeshi la polisi limetaka waandishi wa habari wasikubali kuivuruga nchi katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 31 mwaka huu.
  Mkuu wa jeshi hilo, Said Mwema, aliwaambia wahariri kuwa waandishi wa habari hawapaswi kuwa sehemu ya kuchochea vurugu au kueneza maneno yatakayosababisha kuvurugika kwa amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
  Alibainisha kuwa nchi itakuwa salama kama wananchi watashirikiana na jeshi hilo kuwafichua wahalifu ambao wanaishi ndani ya jamii.


  Chanzo ni Raia kumiliki pingu si kosa - Polisi

  Kwa mawazo yangu Serikali iwaachie Raia kuwa na hicho kifaa cha pingu ili pia iwasaidie kuwakamata Wahalifu kiurahisi, unampomkamata Mwizi inakuwa kwanjia moja au ingine kumfunga pingu na kumpeleka kituo cha Polisi sio kumuuwa Mwizi. Naona Serikali ingetunga sheria wale wanao uwa Wezi wafungwe jela. Nashangaa sana Nchi yetu Mtu akiiba kuku wa jirani anauliwa,Wakati Kiongozi wa Serikali anaiba Mamilioni ya pesa kesi yake utasikia ameachiwa ushahidi hakuna au ameachiwa kwa dhamana. Wakati Mwizi wa Kuku anauliwa Mitaani kasheshe kweli nchi yetu. Wananchi hujichukulia Sheria mikononi mwao pasipo Ruhusa ya Serikali.
   
 2. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  PINGU,inatumika kwa kazi nyingi,mmojawapo ni kufikia the ultimate in sexual arousment,mpenzi hufungwa pingu na huchapwa viboko na mwenzie mpaka hatimaye a earth shattering of biblical proportions current passes through the body. In the process watu saa ingine huumia,but once you are into this you are hooked
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Son Of Alaska,...Are we really together in this matter? Naona wewe umeenda mbali zaidi ya mahitaji ya muulizaji! By the way, pingu si silaha ya kumjeruhi mhalifu, mi naona kama ushahidi upo basi apigwe pingu kusubiria hatua za kipolisi!...But zikitumika vibaya ni udhalilishaji wa juu sana mbele ya jamii, na aliyezitumia anaweza kudaiwa demages kubwa.
   
 4. M

  Manchala New Member

  #4
  Jul 31, 2010
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nijuacho mimi pingu ni kama moja ya vifaa kama bunduki. Nadhani utaratibu wa kupata pingu utakuwa hauna tofauti na jinsi silaha nyingine kama bastola zinavopatikana. Kwa hiyo kama mtu amefuata utaratibu wa kupata hiyo pingu sio tatizo, na umiliki wake utakuwa ni halali mbele ya sheria.
   
 5. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duh!!!!!!kamba si zipo mpaka lazima mtu apate pingu kesho kutwa mtadai hata uniform!
   
Loading...