Raia 24 wa Kigeni Waliokamatwa na Madawa ya Kulevya Iran Wanyongwa kwa Mkupuo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia 24 wa Kigeni Waliokamatwa na Madawa ya Kulevya Iran Wanyongwa kwa Mkupuo

Discussion in 'International Forum' started by Bikra, Aug 6, 2009.

 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Iran imewanyonga kwa mkupuo raia 24 wa nchi za kigeni waliokamatwa nchini humo na madawa ya kulevya.
  Wasafirishaji na wauzaji wa madawa ya kulevya 24 waliokamatwa nchini Iran wamenyongwa kwa mkupuo wiki iliyopita na kuweka historia ya idadi kubwa ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya kunyongwa kwa mkupuo nchini humo, limeripoti gazeti la Etemad la nchini Iran.

  "Siku ya alhamisi, raia 24 wa kigeni waliokamatwa na madawa ya kulevya wamenyongwa katika jela ya Karaj" alisema Mahmoud Salarkia mwendesha mashtaka msaidizi wa Tehran na kuongeza "Mahakama kuu iliidhinisha adhabu zao za kunyongwa".

  Hata hivyo majina ya raia hao wa kigeni walionyongwa katika jela ya Karaj iliyopo magharibi mwa Tehran hayakutolewa.

  Kunyongwa kwa watu hao, kumefanya idadi ya watu walionyongwa kwa makosa mbali mbali nchini Iran kufikia 219 ndani ya mwaka huu pekee.

  Mwezi uliopita jela hiyo hiyo ya Karaj iliwanyonga wafanyabiashara 20 wa madawa ya kulevya.

  Mwaka 2008, Iran iliwanyonga jumla ya watu 246 kwa makosa mbali mbali na ilishika nafasi ya pili duniani baada ya China.

  Serikali ya Iran imesema kuwa adhabu ya kifo ni muhimu sana katika kuhakikisha usalama wa raia na adhabu hiyo hutolewa baada ya taratibu za kisheria kufanyika.

  Watuhumiwa wa makosa ya mauaji, ubakaji, ujambazi,watu wanaokamatwa kwa uzinzi huku wakiwa wameoa au kuolewa na wafanyabiashara au wasafirishaji wa madawa ya kulevya wote huhukumiwa adhabu ya kifo nchini Iran.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Dawa ya Biashara chafu ni kutundikwa tu!
   
Loading...