Rai yangu kwa watanzania kupitia JF

Kweli jamani, sio tu jukwaa la siasa hata kule jukwaa la elimu kuna watu wanaliharibu kwa threads za hovyo hvyo. Mods geukieni na lile jukwaa.
 
May be sasa umefika wakati JF iwe katika pande mbili au kuwe na members wa aina mbili, yaani wale wa kuchangia kutokana na weledi na uelewa bila kuweka ushabiki, kejeli, ujinga n.k. kama JF ya kabla ya 2010 (wawe na jukwaa lao na Mods wawe wanamoderate nani wa kuwa jukwaa hilo) na pia kuwa na jukwaa hili la jamaa zetu wa majungu, udini, ushabiki wa vyama n.k.

Limbani nimeikubali hii!
Kwa kuongezea, ningeshauri Mods waweke a mini jukwaa kwenye siasa la "cheap politics'.Hapa wajimwage wale wote wenye michango hafifu ya rejareja na ushabiki-mbuzi. Mods watakuwa na kazi ya kuhamishia kila "trash" ya siasa huko.Jukwaa la siasa litabaki kwa mambo serious.Nadhani wale waliomwagwa kuchafua hali ya hewa kama kweli wapo baada ya muda watajisikia redundant maana hawatapata mwanya tena wa kuchafua michango makini. Kila kitu chao kitaishia kwenye "trash bin"

Nakubaliana na mawazo haya.Mkuu invisible ikiwezekana kwa atakayeleta ukorofi kwenye jukwaa jipya la 'siasa za kistaarabu',apewe server ban tu.JF ilikuwa ya kuelimisha sana,mtu unalala unaota JF,uko kitaa una check michongo,unawazia JF,na ukiingia JF kwa ilivyosheheni habari motomoto,huwezi kubanduka kabisa walau siyo chini ya masaa matatu.Lakini sasa mhh na siyo siri yote yameanza wakati na baada ya uchaguzi wa 2010
 
Ya Mini-jukwaa inafurahisha lkn end of the day bado watu watapatumia vibaya. Kifupi tutakuwa strict kwenye jukwaa hili, tunalifanyia kazi.

We'll be releasing the mobile app soon hopefully baada ya hapo tutapata muda wa kui-manage JF vema.

WOS,

Nakushukuru sana kwa kuianzisha but kuna some serious note needs to be clarify in detail kwako na MOD. Kitu kinachoitwa udini kimekuwa maarufu hapa JF ila udini hauzungumzwi ni udini upi. Mfano unapowaita waislamu masheikh ubwabwa , waswahili, watu wanaopenda tabia chafu fulani (mfano watoto wa kiume) wakati sio ukweli je huo ni udini? Au wakristo wanavyoitwa wanapenda tabia chafu fulani (za kupenda watoto wa kiume), wabaguzi ,wapenda ufisadi je huo ni udini?

Ikiwa kama udini ni kudhihaki watu wa dhehebu fulani (hasa waislamu) na kuacha wakristo wajisemee wanavyojisikia wao hapo nadhani suala la udini halitaisha kabisa humu jamvini kwani hakuna mtu anayependa kukashifiwa dini yake. Ingelikuwa vizuri na vema mijadala ya kistaarabu inayotawaliwa na hoja za msingi kujadiliwa na sio kuitana majina au sifa zisizopendeza mbele ya watu.

Pia naunga mkono hoja kufutwa kwa thread za kipuuzi kwani zinapoteza mwelekeo na kutia uvivu hata wa kuzisoma. Mie nashauri MOD wawe na wasaidizi wao wanaofuatilia mada zisizo na msingi. Wasaidizi watoke katika members wenye ufahamu mzuri kwenye mada husika. Hilo litasaidia kuweka majadiliano katika mistari husika.

Kuhusu watu waliotuma na CCM kuja kuchafua hali ya hewa sioni ni kikwazo kwani watakaokuja humu watashughulikiwa na wasaidizi wa MOD. watakaopewa Ban na MOD watakuwa ni wale ambao wasaidizi wa MOD watashauri wapewe BAN. MOD watapima uzito wa ushauri wenyewe (judges) ikisha watoe ban hilo litasaidia kupunguza baadhi ya MOD kutoa Ban kwa hisia au emotional zao.
 
Mie nilipojiunga na JF niliamini kuwa hili lilikuwa jukwaa kwa ajili ya great thinkers ili kujadili mambo magumu yahusuyo mstakabali wa nchi yetu; sasa hawa great sinkers nao wametokea wapi?. Sasa tunaanza kupoteza maana. Utakuta hata matusi ya ajabu humu ndani nk. Tunaomba jukwaa hili lilindwe kwa manufaa ya umma. Niliwahi kusema hapa hapa kuwa great thinkers hujadili hoja na si vioja!
 
nafikiri ni ngumu sana kusema mambo yote yasichanganywe,dini na matusi na ubinafsi,tujei nchi yetu imekaa vibaya sana kiutawala,kama viongozi wa nchi wenyewe wanaongea sana mambo ya dini hapa itakuwaje?
kama ni msimu nafikiri hii itapita na hali itarudi kama ilivyokuwa,vilevile tukumbuke tumetoka kwenye uchaguzi mkuu naona watu bado wana hasira na mambo jinsi yalivyokwenda,tuvute pumzi kidogo tuone itakuwaje,lakini mimi binafsi nafaidika mno na jf.
 
WomanOfSubstance umena jambo la busara lakini ukiona hivyo wameruhusiwa na MODS au uwezo wa Mods ni mdogo kugundua wanaobadili mada.
 
Inaonekana hii ni siku mbaya sana hasa kwangu mie ambaye ndo kwanza najitambulisha hapa JF. Jamani, sijatumwa mie nipo kivyangu tu hapa JF kwa hiyo noamba nipokeeni
Karibu sana ukumbini Dakta Gracemary,
Hakijaharibika kitu, umetukuta katikati ya mazungumzo, vuta kiti usikilize na uchangie pia. Jisikie nyumbani kabisa.
 
WOS,

Nakushukuru sana kwa kuianzisha but kuna some serious note needs to be clarify in detail kwako na MOD. Kitu kinachoitwa udini kimekuwa maarufu hapa JF ila udini hauzungumzwi ni udini upi. Mfano unapowaita waislamu masheikh ubwabwa , waswahili, watu wanaopenda tabia chafu fulani (mfano watoto wa kiume) wakati sio ukweli je huo ni udini? Au wakristo wanavyoitwa wanapenda tabia chafu fulani (za kupenda watoto wa kiume), wabaguzi ,wapenda ufisadi je huo ni udini?

Ikiwa kama udini ni kudhihaki watu wa dhehebu fulani (hasa waislamu) na kuacha wakristo wajisemee wanavyojisikia wao hapo nadhani suala la udini halitaisha kabisa humu jamvini kwani hakuna mtu anayependa kukashifiwa dini yake. Ingelikuwa vizuri na vema mijadala ya kistaarabu inayotawaliwa na hoja za msingi kujadiliwa na sio kuitana majina au sifa zisizopendeza mbele ya watu.

Pia naunga mkono hoja kufutwa kwa thread za kipuuzi kwani zinapoteza mwelekeo na kutia uvivu hata wa kuzisoma. Mie nashauri MOD wawe na wasaidizi wao wanaofuatilia mada zisizo na msingi. Wasaidizi watoke katika members wenye ufahamu mzuri kwenye mada husika. Hilo litasaidia kuweka majadiliano katika mistari husika.

Kuhusu watu waliotuma na CCM kuja kuchafua hali ya hewa sioni ni kikwazo kwani watakaokuja humu watashughulikiwa na wasaidizi wa MOD. watakaopewa Ban na MOD watakuwa ni wale ambao wasaidizi wa MOD watashauri wapewe BAN. MOD watapima uzito wa ushauri wenyewe (judges) ikisha watoe ban hilo litasaidia kupunguza baadhi ya MOD kutoa Ban kwa hisia au emotional zao.
Mkuu wangu nadhani huelewi maana ya UDINI na unatokana na vitu gani, dalili zake na kadhalika.

Watu wanapoanza kudharau dini nyingine na kuiona yao bora zaidi hata kama hakuna ukweli basi huo ndio UDINI kwa sababu ubaguzi wowote unatokana na tuhuma sizizo za kweli kutumika kama sababu ya kudharau au kuwanyanyasa kundi jingine. Wazungu walipokuwa wakitumia Ubaguzi wao kwa watu weusi kulitokana na sababu zisizo za kweli, kwamba sisi tulikuwa sawa na wanyama, tunaluka watu, wachafu, tunalala mitini kama nyani na kadhalika.. Hivyo UDNI mkuu wangu ni maandishi yanayodhihaki dini nyingine ili mradi dini yako ionekane bora zaidi wakati dini ni swala la kiimani ambalo hakuna kati yetu anayeweza kumhukumu binadamu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu..

Na nikirudi kwa bibie, WomanofSubstance namjulisha tu kwamba anachokiona hapa ndio hali halisi ya UDINI nchini, hawa watu hawaandiki vitu pasipo bongo zao kufikiria vitu hivyo hata kama watafanya matani lakini dhumuni lake linabakia palepale. Ndivyo wanavyoamini na ndivyo wanavyotaka watu wengine wafahamu ili kujenga chuki baina ya watu wa madhehebu.

Kweli ni hatari kubwa lakini huwezi kumkanya mtu alokusudia kufanya hivyo ukifikira kwamba ni hatari kumwaga sumu ktk mto ili hali anayemwaga anatambua jinsi gani sumu hiyo itaweza kuathiri upande unaotegemea maji haya. Kwa kila anayeandika Udini hapa JF yeye nafikiria yupo juu kilimani na suimu anayomwaga haitapata isipokuwa wale walioko chini ya mkondo wa maji hayo.

Hivyo bibie, nakutaarifu tu kwamba UDINI nchini UPO na hizi ndizo dalili za kwanza za udini unapowasoma watu wenye akili zao wakiandika madudu yenye kujaa chuki wakidai ni dhihaka! - matter of fact, they mean what they write!
 
Najua kuna watakaosema wana haki na uhuru kutumia mtandao huu wapendavyo.Ni sawa kabisa halina ubishi hilo.
Kama unatuambia ni "sawa kabisa na halina ubishi" katika haki na uhuru wa kutumia mtandao upendavyo, sasa issue yako nini, au ni tatizo la Watanzania kutojua kujieleza?
 
WOS,

Nakushukuru sana kwa kuianzisha but kuna some serious note needs to be clarify in detail kwako na MOD. Kitu kinachoitwa udini kimekuwa maarufu hapa JF ila udini hauzungumzwi ni udini upi.

Ndugu yangu Mdondoaji, kwanza nashukuru sana kukuona baada ya kipindi maana tuliwahi kushirikiana vizuri sana kwenye mjadala mmoja tete/tata hapo nyuma na nadhani tulipeleka vizuri ule mjadala na hata ulipofikia tamati "hakukuwa na majeruhi".Udini ninaoouzungumzia hapa ni ile hali ya kujaribu kupindishapinidisha maneno kwa kutumia kivuli cha dini, iwe ya kikristo au ya kiislamu kujaribu kuhusisha kila ovu lililoko TZ na dini hata kama haiingii akilini mwa mtu mwenye uelewa wa kawaida.Tanzania ni nchi iliyotulea na kutukuza tukiamini kabisa kuwa sote ni ndugu na kitu kimoja.Iweje leo tuanze kuchonganishwa kwa sababu ya dini zetu?. Wayafanyayo viongozi wetu au waumini wa dini zetu ni yao binafsi na wala hayatafsiri walivyo waumini wa dini hizo.

Pia naunga mkono hoja kufutwa kwa thread za kipuuzi kwani zinapoteza mwelekeo na kutia uvivu hata wa kuzisoma. Mie nashauri MOD wawe na wasaidizi wao wanaofuatilia mada zisizo na msingi. Wasaidizi watoke katika members wenye ufahamu mzuri kwenye mada husika. Hilo litasaidia kuweka majadiliano katika mistari husika.
Tena MODS walifanyie kazi mapema kabisa. Nadhani baada ya kikao cha MODs leo tutaona mabadiliko na hata ikibidi wenye Jamvi watafute nguvu ya ziada ila wajihadhari wasiwape nafasi watu wasioitakia mema JF na kuwapa rungu la moderation maana itakuwa ni sawa na kichaa kupewa rungu!

Kuhusu watu waliotuma na CCM kuja kuchafua hali ya hewa sioni ni kikwazo kwani watakaokuja humu watashughulikiwa na wasaidizi wa MOD. watakaopewa Ban na MOD watakuwa ni wale ambao wasaidizi wa MOD watashauri wapewe BAN. MOD watapima uzito wa ushauri wenyewe (judges) ikisha watoe ban hilo litasaidia kupunguza baadhi ya MOD kutoa Ban kwa hisia au emotional zao
.

Hapa nami nakuunga mkono kuwa busara itumike zaidi ya "mamlaka" na nguvu ya mod.

Mie nilipojiunga na JF niliamini kuwa hili lilikuwa jukwaa kwa ajili ya great thinkers ili kujadili mambo magumu yahusuyo mstakabali wa nchi yetu;

Hujakosea hata kidogo ndugu yangu.Wengi tulivutiwa na ustadi na umakini wa uchambuzi wa maswala JF.lakini bahati mbaya sana siku za karibuni kiwango kimeshuka sana.

sasa hawa great sinkers nao wametokea wapi?. Sasa tunaanza kupoteza maana. Utakuta hata matusi ya ajabu humu ndani nk. Tunaomba jukwaa hili lilindwe kwa manufaa ya umma.
Niliwahi kusema hapa hapa kuwa great thinkers hujadili hoja na si vioja
!
Hii ndiyo JF ilivyokuwa na kama hatua za makusudi zitachukuliwa basi ubora huu utarudi na kuvutia watu makini kama mwanzo.

nafikiri ni ngumu sana kusema mambo yote yasichanganywe,dini na matusi na ubinafsi,tujei nchi yetu imekaa vibaya sana kiutawala,kama viongozi wa nchi wenyewe wanaongea sana mambo ya dini hapa itakuwaje?

Rosemarie ume note sawa kabisa.Lakini sidhani binadamu tuliojaaliwa utashi tutashindwa kupambanua tuchanganye nini au tusichanganye nini. Kila kitu chaweza kuchanganywa lakini utashi wetu utatusaidia kutuongoza kwenye hili.Viongozi wetu wakiongea sana dini basi tuone ni kwa vipi nao tutawakosoa kwa lugha ya kistaha badala ya kuwavurumishia matusi. Viongozi wetu nao siyo Mungu kiasi tuwaogope kuwaambia kuwa siyo sahihi kutumia mwavuli wa dini kuweka chuki na mgawanyiko kwa wananchi wanaowaongoza.

kama ni msimu nafikiri hii itapita na hali itarudi kama ilivyokuwa,vilevile tukumbuke tumetoka kwenye uchaguzi mkuu naona watu bado wana hasira na mambo jinsi yalivyokwenda,tuvute pumzi kidogo tuone itakuwaje,lakini mimi binafsi nafaidika mno na jf.

Hujakosea hata kidogo.

WomanOfSubstance umena jambo la busara lakini ukiona hivyo wameruhusiwa na MODS au uwezo wa Mods ni mdogo kugundua wanaobadili mada.

Asante.
Tuwaachie Mods kazi nadhani baada ya leo watatuhudumia vizuri zaidi.
 
Kama unatuambia ni "sawa kabisa na halina ubishi" katika haki na uhuru wa kutumia mtandao upendavyo, sasa issue yako nini, au ni tatizo la Watanzania kutojua kujieleza?

Ndugu yangu,
Maana yangu ni nyepesi tu wala haihitaji kamusi kujua nilimaanisha nini.Niliposema "ni sawa" sikumaanisha ni sawa wafanye vile bali nilimaanisha watakuwa sahihi kujibu kuwa wanaweza kufanya wapendavyo... kwani si kila mtu anayo haki ya maoni yake?
 
Wabongo hatutaki kuumiza vichwa kujadili vitu vingumu. Tunapenda vitu simple simple: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/51791-watanzania-tunapenda-mepesi-mepesi.html

Au unaweza kusema wengi tuko reactive na sio procative. Ingawa sio mbaya lakini inabidi tuwe na mixture of proactive and reactive. comments an threads.

Mfano japo wengi tunaweza na ni wepesi wa kukosoa sio wengi wanaweza kusema wangekuwa wao wangefanya nini. Nimewai kuja na uzi huu
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/129146-ungekuwa-wewe-ungefanya-nini.html.

BTN
Nice observation and advice by WoS
 
Niliposema "ni sawa" sikumaanisha ni sawa wafanye vile bali nilimaanisha watakuwa sahihi kujibu kuwa wanaweza kufanya wapendavyo... kwani si kila mtu anayo haki ya maoni yake?
Kama wako sahihi kuwa "wanaweza kufanya wapendavyo," sasa bifu yako nini? Kwa nini Wabongo hatujui kujieleza masikini?
 
Kama wako sahihi kuwa "wanaweza kufanya wapendavyo," sasa bifu yako nini? Kwa nini Wabongo hatujui kujieleza masikini?

Hivi una nini wewe? Au wewe ndio hao mnaofikiri hapa ni kijiwe cha kutafuta Biff?? Poleee!!

And by the way, mada zako mbili ulizoanzisha tangia ujiunge JF nimeshangaa hazikuwahi kuchangiwa hata na mtu mmoja ina maana ulijieleza saaaaaana kiasi ambacho watanzania ambao hawajui kujieleza wakashindwa hata kukujibu?!
 
And by the way, mada zako mbili ulizoanzisha tangia ujiunge JF nimeshangaa hazikuwahi kuchangiwa hata na mtu mmoja...
Unaanza kurusha vijembe na mipasho na mada hasi ambazo nilidhani unazipinga kwenye hii thread, see what the problem is? Unaona jinsi wewe mwenyewe ulivyo sehemu ya tatizo unalotaka kutatua hapa JF?

Hizo thread zangu mbili za kuomba unlock keys si ajabu hakuna aliyekuwa nazo, ndio maana sikupewa, wala sina kinyongo, lakini hiyo sio mada yetu hapa.

Nilichochangia ni kwamba hoja ilivyoletwaletwa ina mushkeli, umesema mwenyewe kwamba atakaetaka kufanya apendavyo hapa "ni sawa kabisa na halina ubishi," sasa issue yako ni nini? Umeshasema ni sawa.
 
when the dove cry
 
Back
Top Bottom