Rai yangu kwa watanzania kupitia JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rai yangu kwa watanzania kupitia JF

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Jul 7, 2011.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wapendwa,

  Ninaomba mnisaidie kidogo maana naona kama nimepotea sielewi.

  Kwa kipindi kirefu nimepotea kuchangia kwenye Jukwaa japo nachungulia kusoma pale nipatapo wasaa. Nimekuwa naona hasa baada ya uchaguzi kumezuka mtindo/trend za "ajabu ajabu"( na haya ni maoni yangu binafsi) watu kujikita zaidi kugeuza JF kuleta hoja za kujaribu kuonyesha ni chama gani zaidi ya kingine na hata pale pasipokuwa na sababu.

  Utaona mtu anamvamia kiongozi wa chama fulani na kumshambulia hata pasipo sababu just because ni wa chama asichokipenda.

  Pia kuna kundi lingine nalo limejikita zaidi katika kushambulia dini za watu na hasa kuchochea uhasama baina ya dini ya kikristo na kiislam. Kundi hili ni tofauti kabisa na lile kundi la kwenye jukwaa la kidini kwa maana wao wanatumia siasa kuchanganya na dini. Kwa mtizamo wangu kundi hil ni hatari zaidi.

  Sumu wanayomwaga ni sawasawa na kumwaga sumu kwenye chanzo cha mto maana hujui itakuua hata wewe mwenyewe maana huwezi kuishi bila kunywa maji na chanzo ni hicho tu hakuna kingine!

  Mimi binafsi nadhani new media ni njia nzuri ya mawasiliano na upashanaji habari. Kiwango cha uzuri wake pale inapotumiwa vizuri ni sawasawa na kiwango cha ubaya pale inapotumiwa vibaya.Ni kama upanga wenye makali pande zote unaporushwa hewani!

  Tuliobahatika kuweza kutumia mitandao basi tungeweza kuleta faida kwa umma mpana zaidi kama tungetumia fursa hii kuibua maswala ya msingi ambayo serikali na hata jamii pana ingeyatumia kwa faida ya umma wa Watanzania, badala ya kutumia nguvu kubwa sana kujaribu kurusha matusi na shutuma zisizo na msingi au mashiko yoyote.

  Najua kuna watakaosema wana haki na uhuru kutumia mtandao huu wapendavyo. Ni sawa kabisa halina ubishi hilo. Lakini ninatoa rai/ombi tujaribu kupunguza hasira na jazba zetu ili tujikite zaidi kwenye majadiliano yenye kulenga kutuletea mabadiliko ya maendeleo.

  Nimeileta kwenye Jukwaa la siasa kwa sababu ni zaidi ya hoja au tangazo. Tatizo ni la kisiasa kwa sababu limejikita zaidi kisiasa na liko zaidi kwenye jukwaa la kisiasa.Kwani siasa za ushindani ni lazima kutumia matusi?......tujadili.

  Asanteni.
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 584
  Trophy Points: 280
  tangu kikao cha kujivua gamba ndipo na JF ikaonekana km jukwaa la udaku, tatizo ni kile kikao cha kujivua gamba pale makao makuu dodoma, vijana wapo wengi kikazi hapa JF, hata yule mstaarabu uliyemzoea naye amegeuka kuwa mdaku kutokana na hiyo sumu iliyomwagwa kwenye mto. mods sasa wana kazi ya kuwapiga ban members ili kupunguza hiyo sumu lakini bado sio dawa, maana km mtu analipwa ili avuruge, hata ukimpiga ban atarudi tu, ajabu sasa hivi kila siku kuna members wapya wengi wanaojiunga, naamini km kwa siku wanajiunga members wapya 10, mmoja tu ndo mpya kwenye hili jukwaa.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  asante wos

  kuna matatizo mengi hapa jf

  la kwanza ni baadhi ya mods....
  kuna thread ilianzishwa juzi kumhusu mzee malecela cha ajabu
  alieanzisha aliweka title ya kiungwana,but sijui ni moderator yupi akaibadilisha
  title akaweka title ya kumvunjia heshima mzee malecela
  nilipo complain,tilte ikabadilishwa..

  huo ni mfano mmoja.
  jiulize kama mods wanaweza shiriki,je watu wengine??????


  kuna watu wa aina mbili hapa,wanaokosoa kwa lengo la kufahamishana
  na wanaokosoa kwa lengo la kutukanana

  mimi nafikiri wanaeleweka so far....
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  halafu kuna mambo now ni very serious kwa future ya taifa

  mfano hii eat africa unification inayokuja...
  but ukikuta thread zinazohusu east safrica issues,huoni kabisa watu wakichangia sana
  itatu cost nionavyo mimi
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Na wale mashabiki wa kutupwa kama MS.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  huyo ms anaeleweka
  na mimi naona anapewa nguvu na umaarufu bure humu ndani....
  sasa kama anaanzisha thread mnaona haina logic
  kwa nini mnachangia???/hamuwezi kuichunia?????/
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kama kinachosemwa ni kweli basi tuna tatizo kubwa zaidi ya linavyoonekana!
  PESA NI SABUNI YA ROHO....PESA INAWEZA KUPOTEZA ROHO! KATIKA JAMII MASKINI PESA/KITU HUWEKWA MBELE KULIKO UTU!
  Ikiwa ni kweli, mbona nchi itafikishwa pabaya!

  Boss,
  Ninakubaliana nawe kwenye bold ya hudhurungi. wenye kutukana Mods pls wasitishieni uanachama
  sitisho la kudumu ikiwezekana server ban.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  halafu na member wote nafikiri tunapaswa jifunza
  culture ya kubishana kwa lengo la kufahamishana na kujenga hoja

  sio mtu akitofautiana nawewe moja kwa moja unmpa label...na matusi....

  sio kila mtu akikosoa chadema kwa mfano,basi anaunga mkono ccm.....

  naweza kuwa sio ccm,na bado nikawa sio convinced na chadema
  tujifunze ku agreee to disagree kiungwana na kwa hoja....

  au naweza mkosoa nyerere but still namheshimu kama baba wa taifa...
  naweza kukubaliana na jk kwa jambo moja,but still nikampinga kwa mengi mengine\
  sio kila kitu ni black or white
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Dada WoS,

  Heshima yako dada angu. Katika wanajamvi ninao waheshimu sana basi mmoja wapo ni wewe. Sijawahi kuona ukianzisha thread mbovu wala kutoa post mbovu. SIku zote maneno yako unayo sema yana mshiko na leo hakuna tofauti.

  WoS, sitopenda kutetea hayo maovu uliyo ya ainisha ila nitataka kukupa sababu ya kwa nini yanatokea ili uweze kuelewa. Hapa namaanisha naomba niwe "The devil's advocate" na nionyeshe upande wa pili wa shilingi.

  Unajua kwa nini hili linatokea dada? Kwa sababu viongozi wengi wa chama na wao hawapendi compromise. Wewe angalia hata Bungeni. Unakuta kiongozi anasifia upumbavu wowote unaotaka kwenye chama chake na kupinga hata kizuri kinacho toka chama tofauti. Wao wamesha jenga tabia ya "You are either with us 100% or against us 100%". Sasa unakuta hata wafuasi wa vyama inabidi wafuate hiyo principle. Kwa nini ujaribu kucompromise na asiyetaka kufanya hivyo? Kwa nini nisifia mazuri yako wakati mazuri yangu utayapinga tu? Kwa hiyo it's a trickle down effect. Viongozi wakianza kuonyesha kuwa wapo tayari kuacknowledge mazuri ya upande wa pili basi na wananchi wa kawaida wata yaona hayo na kuiga mfano.

  Dada angu tunajua na ipo wazi kuna chama fulani kilitumia "udini" usiokuwepo kujaribu kukipaka chama kingine. Chama hiki kilitaka kuonyesha kwamba mgombea wao anapingwa sababu ya dini yake. Hii ilikua campaign strategy. Kwa ajili ya kuendeleza strategy hii from the ground up kuna watu walitumwa humu JF makusudi wapromoste strategy hiyo ya chama hicho kwa maana walituma watu wao na wao waingie humu na wapandikize hoja za kidini. Hawa watu humu ndani ni wachache sana lakini wanakelele nyingi mpaka unaweza kujichanganya na kudhani kwamba udini umeenea JF kumbe sivyo.

  Kwa hiyo dada angu binafsi naona uliangalia zaidi "what" is happening bila kuangalia pia na "why" it is happening. Najua yanayo tokea si mazuri lakini pia si bahati mbaya. Kuna sababu zake. Ila maadam kuna watu kama wewe ndani ya JF na jamii kwa ujumla naamini tuta piga vita hizi siasa chafu.

  Asante....
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  mkuu umeongea ukweli mtupu.....
  naogopa kuigeuza hii thread kuwa thread nyingine ya watu kubishana kwa kuwa muwazi zaidi
  si nitajizuia kutaja majina

  inafahamika mno kuwa humu ndani ukiikosoa chadema tu
  unaanzisha ugomvi,wakati wengi tunaokosoa chadema tuna matumaini kuwa
  kitashika nchi soon.so tunataka wawe perfect na wajirekebishe now....

  hilo la ccm kujifanya kuna udini,linafahamika sana.....
  actually ni kila uchaguzi wanafanya hivyo....
  uliza historia yao...
  wakati wa mrema,walitumia sana misikiti kumpinga mrema.
  kila uchaguzi ccm,wanakuwa na stategy za siri na za ajabu mno...
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Tujifunze kukosoa kistaarabu.

  Kama viongozi wetu tuliowachagua watatugawa kwa dini zetu basi watafanikiwa sana kuivuruga amani iliyojengwa kwa miaka 50!! Ni dhambi itakayowatafuna wao na vizazi vyao vyote na tutamuomba Mungu kama hili litatokea basi awapatilize wao na vizazi vyao vyote!
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  sio tu tuendako
  ila mimi naona tulipofika ni pabaya mno tayari......

  waziri anaboronga,akifika bungeni anawa mobilise wabunge wa dini yake wamlinde
  wanaofahamu vizuri nchi ya nigeria,wanajua haya yote ni marudio ya mambo ya nigeria....

  tuna mgao wa umeme,waziri anawahonga wabunge,wabunge watamsifia bungeni...
  atakae pinga ataitwa mpinzani,au ana udini,au sio mwenzetu
  ni pabaya mno hapa tulipo....
   
 13. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #13
  Jul 7, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 584
  Trophy Points: 280

  umewashtukia ee? wapo humu, wala hata hii thread yako haijawashtua kabisa.
   
 14. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Majibu y ako ni yamejitosheleza

  esp the below part ndipo panapo wafanya watu kukinzana kwa hoja na majibu

   
 15. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  May be sasa umefika wakati JF iwe katika pande mbili au kuwe na members wa aina mbili, yaani wale wa kuchangia kutokana na weledi na uelewa bila kuweka ushabiki, kejeli, ujinga n.k. kama JF ya kabla ya 2010 (wawe na jukwaa lao na Mods wawe wanamoderate nani wa kuwa jukwaa hilo) na pia kuwa na jukwaa hili la jamaa zetu wa majungu, udini, ushabiki wa vyama n.k.
   
 16. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Seriously you hit the nail on the head. Tuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu mustakabali wa nchi yetu. Tunakwenda wapi, nani atatufikisha hapo tunapotaka kufika. Kwa kweli kinachoonekana siku hizi hapa JF ni kama kijiwe cha mtaani kabisa.

  Inaweza kuwekwa thread ya msingi kabisa lakini hakuna cha maana kitakachojadiliwa badala yake yataingizwa matusi na unnecessary attacks kwa viongozi wa vyama au vyama fulani. Ni tatizo hili hili lililotufikisha hapa tulipo. Ushabiki wa kutofikiria. Wana jf wengi sana siku hizi ni sawa kabisa na wanajeshi wa kinjekitile. Wakiambiwa ukisikia "pu" sema "maji".

  Ni kitu cha ajabu sana, mtu anawezaje kutumwa kuharibu mtandoa ambao unatoa mawazo ya namna tunaweza kufikia malengo ya kitaifa? Unawezaje kuvuruga, mijadala yenye mantiki kwa ajili ya faida yako na jamii yako?

  Tunaona ulimbukeni mkubwa sana katika nchi hii. Binafsi naipenda sana jf na I am addicted! Lakini siku za karibuni, nimeichukia kwa sababu ya namna mambo yanavyojadiliwa. Jambo la msingi linaweza kufanywa jambo la chama, jambo linalohusu jamii kwa ujumla linaingizwa katika dini. Mtu anatetea uovu tena kwa matusi. Hakuna ustaarabu kabisa.

  Rai yangu ni kuwaomba watu wote wenye mapenzi mema na chini hii, tujadili mambo kwa ustaarabu. Mimi naanza naomba na wewe useme naanza. Mchana mwema.
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Limbani nimeikubali hii!
  Kwa kuongezea, ningeshauri Mods waweke a mini jukwaa kwenye siasa la "cheap politics'.Hapa wajimwage wale wote wenye michango hafifu ya rejareja na ushabiki-mbuzi. Mods watakuwa na kazi ya kuhamishia kila "trash" ya siasa huko.Jukwaa la siasa litabaki kwa mambo serious.Nadhani wale waliomwagwa kuchafua hali ya hewa kama kweli wapo baada ya muda watajisikia redundant maana hawatapata mwanya tena wa kuchafua michango makini. Kila kitu chao kitaishia kwenye "trash bin"
   
 18. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  tuendeleeni na mada yetu.....
   
 20. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #20
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ya Mini-jukwaa inafurahisha lkn end of the day bado watu watapatumia vibaya. Kifupi tutakuwa strict kwenye jukwaa hili, tunalifanyia kazi.

  We'll be releasing the mobile app soon hopefully baada ya hapo tutapata muda wa kui-manage JF vema.

  Tusaidieni kutuarifu hoja zenye kuichafua JF na jamii kwa ujumla kwa kubonyeza ICON HII juu ya post husika:

  [​IMG]
   
Loading...