Rai yangu kuhusu kauli ya Rais juu ya mitandao ya kijamii

Oct 5, 2015
88
476
Nimesikia 'mitandaoni' kauli ya Mh. Rais kwamba anatamani malaika washuke wazime hiyo mitandao. Kupitia kauli hii, tunagundua mambo makubwa matatu na mengine madogodogo.

1. Rais anafuatilia sana yaliyomo mitandaoni.
2. Rais anaamini mitandao ni kikwazo katika kutekeleza majukumu yake ya kiuongozi.
3. Kauli ya Rais ni kielelezo cha nguvu ya mitandao ya kijamii katika kuleta mabadiliko chanya, au hasi.

Ningependa kujadili zaidi hili la tatu.
Mh. Rais, Pamoja na kwamba umewataja malaika lakini dhamira yako hasa Inaonekana hupendi mitandao ya kijamii.

Mh. Rais, hakuna nchi duniani iliyothubutu kuzima mitandao ya kijamii isipokuwa tu Uturuki ambayo iliizima mitandao kwa muda baada ya jaribio la kupindua serikali. Katika Uchina hakuna mitandao hii tunayoijua huku, lakini wana mitandao yao, kama Weibo, RenRen, Youku nk. Huku Tanzania bado hatuwezi kuwa na mitandao yetu.

Mitandaoni ndio mahali ambapo taarifa husambaa kwa haraka kuliko mahalai popote. Katika uchaguzi wa uraisi, wabunge na madiwani, wa Oktoba 2015, kampeni zilipigwa mitandaoni. Sera zako tukizisikia mitandoani. Mitandao ndio iliyotuwezesha tukuone ukiahidi kufungua mahakama za mafisadi. Mitandao ndio iliyotuonesha ukipiga push-up kuonesha ukakamavu wako. Mitandao ndio iliyotuwezesha tujue mapema kwamba 'umetangazwa' kuwa Rais.

Ahadi zako kuhusu kununua ndege, mitandaoni. Ndege zimekuja tumeziona mitandaoni. Umeenda kuzindua, tunakuona mitandaoni. Taarifa za kutumbua majipu tunazipata mitandaoni. Hata Falsafa zako ya kubana matumizi na ile ya Hapa Kazi tu, zina'bamba' kwa sababu ya mitandao.

Lakini kwanini Mh. Rais unatamani mitandao izimwe? Bila shaka umepima na kuona kuwa upande usiokufurahisha una nguvu kubwa kuliko upande unaokufurahisha. Pengine, hoja za watetezi wako ni nyepesi kulinganisha na hoja za 'wachokozi' wako. Lakini yafaa nini kwako kama Rais wa watanzania wote kujali kufurahishwa na kutokufurahishwa mitandaoni? La! Haifai.

Lakini pia, si kweli kwamba vijana wengi wanaotajwa kukukashifu mitandaoni wamekamatwa, kupigwa na kufunguliwa mahstaka kisha kufungwa na kupigwa faini kubwa? Je! Kauli yako ni ujumbe kuwa jitihada za kuwanyamazisha kwa vitisho wakosoaji wa serikali yako kupitia mitandao, zimegonga mwamba?

Nadhani Mh. Rais ungewekeza nguvu zaidi katika kujenga nchi huku wananchi wakaachwa huru watoe maoni yao kwa uhuru. Kama unafanya kazi nzuri hutakuwa na wakati mgumu kuwajibu wakosoaji wako. Lakini kama unafanya kazi mbovu bila shaka wakosoaji wako watakuzidi kwa hoja, na ukijali sana hoja hizo kinzani, lakini usiwe na majibu ya kuzishinda, utaishi kwa hasira. Hasira huzaa maradhi ya kichwa, tumbo na moyo. Hakuna raia mwema anayependa Rais augue maradhi ya kichwa, tumbo na moyo.

Kwa kumalizia tu; Mh. Rais, usiogope wananchi wako kisa tu wana mawazo tofauti na wewe au kisa wanaikosoa serikali. Ni haki ya asili kuwaza tofauti, hata ukiweka sheria ya kuzuia watu wasiwaze tofauti utakuta na wewe unaingia hatiani, Leo unawaza hivi kesho unabadili mawazo. Kwani haijawahi kutokea? Ndivyo ilivyo. Na ukitaka kusikiliza unayopenda tu, akili hudumaa. Lakini kujifunza na kukua kifikra kunakuja kwa Kusikiliza hoja kinzani, na si lazima uzikubali. Ni haki yako pia kuzipinga kama wewe unavyopingwa.

Jenga nchi, utuache na Uhuru wetu! Umezima bunge, umeendelea kuzitumia sheria kandamizi za kudhibiti sauti za watu mitandaoni, haitoshi unatamani na kuzima mitandao? Tafadhali.
Wewe ni Rais, tutake tusitake.
Na sisi ni watanzania, tutakupongeza kwa kazi njema, na kukukosoa kwa kazi mbovu, Utake usitake.
Asante.
 
Moja; Rais anafuatilia sana yaliyomo mitandaoni.
Pili; Rais anaamini mitandao ni kikwazo katika kutekeleza majukumu yake ya kiuongozi.
Tatu; Kauli ya Rais ni kielelezo cha nguvu ya mitandao ya kijamii katika kuleta mabadiliko chanya, au hasi.

Mkuu Chris, naunga mkono hoja.
Pasco
 
anakera ajifunze kukaa kimya...Mungu alipotuumba na masikio mawili na mdomo mmoja alikuwa na sababu, kwamba we should listen twice as much as we speak...sasa yeye anavuvuzelika tuuuuu, aargh!
 
Magu [sitashangaa siku tukija kukatazwa kumwita Magu ] tayari keshaonyesha kuwa ana ngozi nyembamba ya kutoweza kuvumilia na kupuuza maneno ya watu dhidi yake ambayo kwa kiasi kikibwa yanakuja na nafasi pekee aliyonayo kwenye nchi hii.

Ukiwa rais utasemwa tu. Na utasemwa kwa yote, mazuri, mabaya, ya kipuuzi, ya kizushi, na kadhalika.

Sasa yeye sijui halielewi hilo au analielewa fika lakini hana uvumilivu wa kuyapuuza....ukweli anaujua mwenyewe.

Ila mimi binafsi naamini yeye ni mdau wa siku nyingi tu humu JF.
 
Nyie endeleeni tu....
Wala usiwe na wasi wasi, tunaendelea kama kazi...mnavyozidi kutuwekea vikwazo ndivyo na sisi tutaongeza moto. Ningependa kuchukua nafasi hii kumshauri kwamba ni ukosoaji wetu ndio utamsaidia na si kumlamba viatu. Hivi leo akiamua kufungia mtandao sawa ila ajue atakuwa amewasha moto ambao hana uwezo tena wa kuuzima.
 
Kuna mahali alisema eti wakosoaji ilifika mahali wakamfanya ahisi amefanya uamuzi usio sahihi!!

Jamaa anaonekana weak mno in thinking and reasoning kiasi kwamba hajiamini!!

Yupo too emotional!!!
 
Ushauri rais yeye afanye kazi kama vile mikakati yake alivyopanga huku mitandaoni ni kelele za chura ( kwa sisi wa Tz ni waoga mnooooo ) hakuna anayeweza kuja magogoni kukutunishia msuli anayetaka uongozi uwe sahihi 100% angoje 2020 agombee fanya yako wacha sie tufurahishe genge huku whatsApp Fb IG Twitter na kwingineko
 
Na hisi mh Rais wetu ana taka awe anasifiwa kwa kila jambo ni mtu asiyetaka kuona mtu yeyote akimkosoa,baada ya kufanikiwa kuwabana watu ambao wangeweza kumkosoa bungeni na kwenye mikutano ya hadhara,mahali peke ambapo mh Rais anapo paona panakwenda kinyume na matakwa yake ni kwenye mitandao ya kijamii.

Na usije ukashangaa mitandao ya kijamii ikapigwa mkwara Kama siyo kufungiwa kabisa kwa kuwa watendaji wa Rais wataichukulia kauli ya Rais kuwa Wao ndio malaika ambao Rais alitamani watokee waifungie mitandao ya kijamii japo kwa mwaka mmoja tu,
 
Watanzania wana akili siku hizi.
Hivi yule mtetezi wa wanyonge watu wa chini kabisa amewatetea watanzania ktk hali za maisha huko Tz?Hivi bunge lipo live siku hizi?
Nijulisheni nirudi Tz.
 
Nimesikia 'mitandaoni' kauli ya Mh. Rais kwamba anatamani malaika washuke wazime hiyo mitandao. Kupitia kauli hii, tunagundua mambo makubwa matatu na mengine madogodogo.

1. Rais anafuatilia sana yaliyomo mitandaoni.
2. Rais anaamini mitandao ni kikwazo katika kutekeleza majukumu yake ya kiuongozi.
3. Kauli ya Rais ni kielelezo cha nguvu ya mitandao ya kijamii katika kuleta mabadiliko chanya, au hasi.

Ningependa kujadili zaidi hili la tatu.
Mh. Rais, Pamoja na kwamba umewataja malaika lakini dhamira yako hasa Inaonekana hupendi mitandao ya kijamii.

Mh. Rais, hakuna nchi duniani iliyothubutu kuzima mitandao ya kijamii isipokuwa tu Uturuki ambayo iliizima mitandao kwa muda baada ya jaribio la kupindua serikali. Katika Uchina hakuna mitandao hii tunayoijua huku, lakini wana mitandao yao, kama Weibo, RenRen, Youku nk. Huku Tanzania bado hatuwezi kuwa na mitandao yetu.

Mitandaoni ndio mahali ambapo taarifa husambaa kwa haraka kuliko mahalai popote. Katika uchaguzi wa uraisi, wabunge na madiwani, wa Oktoba 2015, kampeni zilipigwa mitandaoni. Sera zako tukizisikia mitandoani. Mitandao ndio iliyotuwezesha tukuone ukiahidi kufungua mahakama za mafisadi. Mitandao ndio iliyotuonesha ukipiga push-up kuonesha ukakamavu wako. Mitandao ndio iliyotuwezesha tujue mapema kwamba 'umetangazwa' kuwa Rais.

Ahadi zako kuhusu kununua ndege, mitandaoni. Ndege zimekuja tumeziona mitandaoni. Umeenda kuzindua, tunakuona mitandaoni. Taarifa za kutumbua majipu tunazipata mitandaoni. Hata Falsafa zako ya kubana matumizi na ile ya Hapa Kazi tu, zina'bamba' kwa sababu ya mitandao.

Lakini kwanini Mh. Rais unatamani mitandao izimwe? Bila shaka umepima na kuona kuwa upande usiokufurahisha una nguvu kubwa kuliko upande unaokufurahisha. Pengine, hoja za watetezi wako ni nyepesi kulinganisha na hoja za 'wachokozi' wako. Lakini yafaa nini kwako kama Rais wa watanzania wote kujali kufurahishwa na kutokufurahishwa mitandaoni? La! Haifai.

Lakini pia, si kweli kwamba vijana wengi wanaotajwa kukukashifu mitandaoni wamekamatwa, kupigwa na kufunguliwa mahstaka kisha kufungwa na kupigwa faini kubwa? Je! Kauli yako ni ujumbe kuwa jitihada za kuwanyamazisha kwa vitisho wakosoaji wa serikali yako kupitia mitandao, zimegonga mwamba?

Nadhani Mh. Rais ungewekeza nguvu zaidi katika kujenga nchi huku wananchi wakaachwa huru watoe maoni yao kwa uhuru. Kama unafanya kazi nzuri hutakuwa na wakati mgumu kuwajibu wakosoaji wako. Lakini kama unafanya kazi mbovu bila shaka wakosoaji wako watakuzidi kwa hoja, na ukijali sana hoja hizo kinzani, lakini usiwe na majibu ya kuzishinda, utaishi kwa hasira. Hasira huzaa maradhi ya kichwa, tumbo na moyo. Hakuna raia mwema anayependa Rais augue maradhi ya kichwa, tumbo na moyo.

Kwa kumalizia tu; Mh. Rais, usiogope wananchi wako kisa tu wana mawazo tofauti na wewe au kisa wanaikosoa serikali. Ni haki ya asili kuwaza tofauti, hata ukiweka sheria ya kuzuia watu wasiwaze tofauti utakuta na wewe unaingia hatiani, Leo unawaza hivi kesho unabadili mawazo. Kwani haijawahi kutokea? Ndivyo ilivyo. Na ukitaka kusikiliza unayopenda tu, akili hudumaa. Lakini kujifunza na kukua kifikra kunakuja kwa Kusikiliza hoja kinzani, na si lazima uzikubali. Ni haki yako pia kuzipinga kama wewe unavyopingwa.

Jenga nchi, utuache na Uhuru wetu! Umezima bunge, umeendelea kuzitumia sheria kandamizi za kudhibiti sauti za watu mitandaoni, haitoshi unatamani na kuzima mitandao? Tafadhali.
Wewe ni Rais, tutake tusitake.
Na sisi ni watanzania, tutakupongeza kwa kazi njema, na kukukosoa kwa kazi mbovu, Utake usitake.
Asante.
Hoja zenye ujazo akili kubwa pekee ndo zitaelewa vizur uzi huu..

Hata kama Mh. Sana akisoma atakuwa anajifunza taratib taratib mpaka kukurupuka kutakapo isha..

Salute sana bro kwa andiko hili

ndo napaa ivo..
 
Back
Top Bottom