Rai ya Jenerali: Waziri mkuu asiye waziri mkuu, serikali iliyobinafsishwa - hatuendi kokote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rai ya Jenerali: Waziri mkuu asiye waziri mkuu, serikali iliyobinafsishwa - hatuendi kokote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 25, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Jenerali Ulimwengu


  236
  25 Apr 2012

  NCHI inapitia kipindi tete, kipindi ambacho kinashuhudia maswali mengi yakiruka kutoka kila upande huku kukiwa hakuna majibu yanayoeleweka. Halitakuwa kosa kuieleza hali hii kama hali ya mkanganyiko wa kitaifa.


  Hivi majuzi niliandika makala katika mlolongo wa safu hii iliyosema kwamba "kupotea tulikopotea ni kupotea kukubwa." Hali tuliyo nayo leo hainipi sababu ya kudhani kwamba hali yetu ya upotevu imebadilika sana, isipokuwa tu kwamba watu wengi zaidi wametambua kupotea kwetu ama wameamua kukupigia ukunga, kusema kwamba hata wao wameuona upotevu huo.


  Hivi majuzi Rais Jakaya Kiwete ameiapisha tume yake aliyoiteua kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Napenda kuwapa pole wote walioteuliwa kwa kubebeshwa mzigo usiobebeka, kwa sababu ambazo nitazieleza leo na katika makala nyingine zijazo.


  Kimsingi, ninachokiona mimi ( na wala siko peke yangu katika hili) ni kwamba tuko katika hali ya wananchi kufurukuta wakitaka mabadiliko makubwa yafanyike na yaonekane yakifanyika, lakini wakikabiliana na utawala uliokufa ganzi na kuduwaa, usijue la kufanya. Wananchi wanaumia, wanahenya, wanalalama, wanatafuta majibu, lakini wanakutana na maswali zaidi.


  Kila mtu anajua kwamba hali ya maisha kiuchumi imekuwa ngumu sana, hususan katika maisha ya watu wa kawaida ambao wanaathirika vibaya kutokana na gharama za maisha kuzidi kupanda kutokana na bei za mafuta na chakula kupanda kila uchao. Hawaoni jitihada zo zote za serikali yao kupambana na hali hiyo, na badala yake wanashuhudia wakubwa ndani ya serikali wakizidi kujijengea ukwasi usiokuwa na maelezo.


  Taratibu, wananchi wameanza kutambua kwamba ufukara wao katika mazingira ya nchi tajiri sana unahusiana moja kwa moja na utajiri mkubwa wa watawala wao ambao wamekuwa wakitumia ofisi zao kujikusanyia mali haramu. Ofisi za serikali sasa zinajulikana kuwa ni mali binafsi za wale waliowekwa mle eti kuwatumikia wananchi. Kila anayepata nafasi hiyo ameiona kama ‘kihamba' chake binafsi bila kujali maslahi ya nchi.


  Jambo moja linajidhihirisha kila mwaka, nalo ni kwamba kila siku uozo wa watawala wetu unazidi kujidhihirisha kwa kiasi kile kile ambacho tunadhihirisha udhaifu wa jamii yetu kukabiliana nao.


  Kwa mfano, ofisi ya CAG ina maana gani kama kila mwaka inatoa taarifa inayoonyesha ubadhirifu katika idara za serikali lakini hakuna hatua yo yote inayochukuliwa kutokana na taarifa hizo?


  Hakuna shaka kwamba ofisi ya CAG inaendeshwa kwa gharama kubwa na ziara za uchunguzi zinazofanywa na ofisi hiyo ndani na nje ya nchi ni mzigo mkubwa kwa bajeti ya nchi, na gharama hizi hatimaye zinabebwa na mlipa kodi. Kama tunajua kwamba taarifa za CAG hazina umuhimu kwa sababu hakuna dhamira ya kuzifanyia kazi, ni kwa nini ofisi hiyo isifungwe ili, angalau, tupunguze matumizi katika eneo hilo finyu?


  Ofisi ya CAG ni kielelezo cha undumilakuwili wa utawala wetu. Sipati neon toshelezi la kuielezea hali hii, hivyo nalazimika kutumia neno la Kiingereza 'schizophrenia,' kwa maana ya kuwa na hulka mbili kwa wakati mmoja.


  Kwa upande mmoja, tumerithi kutoka kwa wakoloni vyombo vya udhibiti ambavyo kazi yake ni kuhakikisha kwamba fedha za serikali hazitumiki hovyo, na kwamba pale zinapothibitika kutumika hovyo, wahusika wanachukuliwa hatua.


  Lakini kwa upuuzi wetu hatuna dhamira ya kuchukua hatua pale inapobidi kwa sababu, kimsingi, ni kama tumekubaliana kwamba kila mtu atajinufaisha na ofisi yake, na kwa hiyo hakuna wa kumsema mwenzie.


  Kwa maana hiyo, ingekuwa hatua ya mantiki kuifutilia mbali ofisi ya CAG, lakini hiyo ingetusababishia matatizo na wafadhili ambao wangetusuta kwa kufuta ofisi muhimu kama hiyo.


  Hivyo, basi, tunayo ofisi ya CAG ambayo inatoa taarifa za kila mwaka ambazo hazifanyiwi kazi lakini hatuifuti kwa sababu wafadhili watatusuta. Watu wa ajabu!


  Kuna jambo ambalo inawezekana watawala wetu wamekosa kuliona kutokana na ulafi wao na uwezo mdogo wa kufikiri unaotokana na ulafi huo. Kuruhusu ofisi ya CAG kutoa taarifa hizi kila mwaka zikionyesha wizi mkubwa wa fedha za wananchi bila kuzichukulia hatua ni njia mojawapo ya kujenga chuki ya wananchi dhidi ya serikali. Serikali inayofikiri ingechagua moja: ama kuzifanyia kazi taarifa hizo, ama kuzipiga marufuku kabisa na kuifuta ofisi ya CAG. Kwa sasa serikali yetu ni 'schizophrenic.'


  Kwangu mimi ni dhahiri kwamba siku wananchi watakapochukua hatua ya kuwaadabisha watawala wao, hoja mojawapo itakayowasukuma itakuwa ni taarifa za CAG zisizofanyiwa kazi.


  Wiki iliyopita, bungeni, tumepata ushahidi mwingine kwamba watawala wetu wameshindwa kufanya kazi wanayotakiwa kuifanya. Baadhi yao wamebanwa na wabunge ambao bila shaka wamesukumwa na hasira za wananchi dhidi ya utawala wa ubadhirifu, wizi, kutokujali, na upuuzi. Katika sakata tulilolishuhudia bungeni, mojawapo ya sababu za malumbano yale ni taarifa za ubadhirifu serikalini (kutoka kwa CAG na kwingineko) ambazo serikali inaonekana kutokuwa na uwezo wa kuzishughulikia.


  Kusema kweli, sura iliyojitokeza wiki hii iliyopita ni kwamba hatuna serikali inayofanya kazi kama serikali, bali tuna mkusanyiko wa maofisa waliokabidhiwa ofisi mbalimbali ambazo wanazitumia kadri wanavyojua wao na wala hawana udhibiti wa kati (central control).


  Kila mmoja anasema anavyotaka, na katika kusema huko tunagundua kwamba katika ofisi yake anatenda anavyotaka pia, na hana ofisa mwandamizi wa kumwelekeza.


  Walichotuonyesha watawala wetu wiki iliyopita ni taswira ya mkanganyiko mkubwa na wa kutia wasiwasi kwa ye yote anayethubutu kufikiri kidogo. Nchi hii haijakabiliwa na janga kubwa la ghafla katika miaka ya karibuni. Hatujakabiliwa na vita, mafuriko makubwa wala milipuko mikubwa ya magonjwa ya kutisha. Tuthubutu kujiuliza, je, iwapo tungekabiliwa na mojawapo ya majanga kama hayo, wale tuliowaona na kuwasikia bungeni Dodoma ndio tungewaamini kwamba wangetuongoza kuishinda dharura hiyo? Wale?


  Nasema hapana. Tulichokishuhudia ni msamabaratiko ambao haujawahi kutokea katika historia ya nchi hii, serikali iliyoparaganyika, mawaziri wenye kauli za kitoto, wakuu wa serikali wasiokuwa na maamuzi, waziri mkuu kivuli asiyekuwa waziri mkuu, na mkuu wa nchi mtoro.


  Hapo juu nimewapa pole wale walioteuliwa katika tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Hii ni kwa sababu namheshimu sana Joseph Warioba, kama ninavyowaheshimu baadhi ya wajumbe wa tume yake. Ningependa Warioba, ambaye tunajua sote ni mtu makini, afanikiwe nasi tupate manufaa.


  Katika wiki zijazo nitaieleza ‘pole' yangu, lakini nianze tu kwa kusema kwamba, katika kazi ambazo zinaweza kufanywa na tume hiyo katika muda mfupi iliyopewa ni kuangalia nafasi ya waziri mkuu asiye waziri mkuu, anayefanya kazi chini ya mkuu wa nchi asiyekuwapo, na anayewasimamia mawaziri asiowasimamia na wanaofanya shughuli zao binafsi.


  Hivi tunaelezaje kwamba inafikia hatua ya wabunge (bila kujali vyama) wanachukua uamuzi wa kufanya jambo ambalo halijawahi kufanyika katika historia yetu, kama kusukuma hoja ya kutokuwa na imani na serikali kwa sababu mawaziri wachache wanaoonekana wameboronga hawataki kuondoka hata pale wanapotakiwa kufanya hivyo na chama chao bungeni, halafu waziri mkuu hana kauli na bosi wake yuko ughaibuni?


  Kama nilivyosema kuhusu ofisi ya CAG asiye CAG, hivi kuna haja gani ya kuwa na waziri mkuu asiye waziri mkuu? Niliwahi kuijadili mada hii katika safu hii yapata miaka miwili iliyopita, nikieleza ‘schizophrenia' ya ofisi hii.


  Nilieleza kwamba katika mojawapo ya mazoezi ya kuunda serikali katika miaka ya sabini, Mwalimu Nyerere alimteua Edward Sokoine kuwa waziri mkuu, na akaulizwa na waandishi wa habari kwa nini anamteua waziri mkuu wakati Katiba haitaji ofisi hiyo.


  Jibu la Mwalimu lilikuwa ni kwamba, kweli, Katiba haikusema kwamba kutakuwa na waziri mkuu, lakini pia Katiba haikutamka kwamba hakutakuwa na waziri mkuu, na kwamba waziri mkuu ni waziri kama mawaziri wengine isipokuwa yeye yuko kidogo juu ya wenziwe. ‘Schizophrenia.'


  Baadaye ikaandikwa kwenye Katiba kwamba tutakuwa na waziri mkuu atakayekuwa kiongozi mkuu wa "shughuli za serikali bungeni" lakini tunashuhudia ukweli kwamba tunaye waziri mkuu asiye waziri mkuu.


  Ndiyo maana hawezi kuwaambia mawaziri wanaotoa kauli za kijinga "Shut up!," hawezi kumwambia bosi wake awaondoe, na imedhihirika kwamba huko maofisini mwao wanafanya wanavyotaka. Waziri anaweza akasema hadharani kwamba naibu wake anafanya mambo bila kumwambia, anakwenda kutafuta wakandarasi wake bila kumpa taarifa, na kadhalika, hali inayodhihirisha ubinafsishaji wa ofisi za serikali yetu.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ubepari wetu ni tofauti na ubepari wa nchi za magharibi, wetu tunawapa wachache wa nje watumalize, hatuna sauti yoyote kuhusu Uchumi wetu, Usalama wetu uhuru wetu... tumeuza vyote
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Ulimwengu in top form.Tunahitaji wakongwe hawa waseme hivi isije kuonekana ni maneno ya vijana wasioijua nchi tu haya na "yatapita kama upepo".
   
 4. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
   
 5. O

  Olecranon JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,371
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Ulimwengu umenena
   
 6. k

  kindafu JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
   
 7. T

  TUMY JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jenerali Ulimwengu moja kati ya watu ninao waheshimu sana.
   
 8. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,078
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Makala nzuri sana hii Mzee Ulimwengu na ni kweli kabisa kuwa waziri mkuu kibogoyo na mkuu wake mtoro. Du kazi tunayo.

  - Asante nngu007 kwa kutubandikia
   
 9. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  that is a recipe for disaster!!!
   
 10. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mzee Jenerali ni muda sasa ujitokeze jamvini hapa JF!
  Nasubiri hyo "pole" uliyowapa wakina Warioba.
  "nchi ya ajabu" ndio ninachoweza kusema pia.
   
 11. w

  wakijiwe Member

  #11
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makala imejitosheleza vilivyo na mwandish kaonesha uwezo mkubwa wa uchambuzi.
  Huu ndo uandish unaohitajika umejaa critical thinking na una sense..
   
 12. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini, Usije kukuta Pinda nae haelewi majukumu yake kama Waziri Mkuu kama mimi nisivyoyaelewa vile! Zamani nilikuwa nadhani, Waziri Mkuu ni kama Kiranja wa Mawaziri wote na kwamba pamoja na Mawaziri kuteuliwa na "Mtoro" lakini Waziri Mkuu anaweza kuwakemea, lakini yanayojitokeza sasa, ukiacha tofauti ya Majina ya Ki-Cheo, sijaona tofauti ya Kiutendaji kati ya Waziri Mkuu, Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu.
   
 13. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Tukikosea kidogo huko siku za mbele huyu Jenerali twaweza mwita "Shehe Yahya" wakati sio kweli bali anaona mbali na kutahadhalisha mapema lakini wenye inchi hawaoni wala kusikia na huishia kubeza, Serikali yetu ni kama Kenge fulani kwani "Kenge haachi mila zake mpaka atokwe na damu masikioni"
   
 14. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Dah,rais mtoro
  kama darasan itakua hivi.
  MWALIM:JEI KEI
  WANAFUNZI:HAYUPO JANA NA LEO.
  Mwalim:halafu huyu jei kei mtoro.
  WANAFUNZI:NDO KAWAIDA YAKE
   
 15. S

  Saas JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rais “Mtoro”
   
 16. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2012
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Asante na pongezi Jenerari- We cant all stand in the political ''pulpit'' and preach, umefanya kwa sehemu yako
   
 17. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sishangai Baada ya siku kadhaa ikaibuka tena ile Kesi ya Uraia wa Ulimwengu.

  Ni nani mwingine mwenye guts ya kuutamka ukweli huu?

  quote my words, msishangae statement kutoka ikulu ikihoja ukweli huu uliondikwa hapa. Mark my words please.

  Take five Jenerali!!
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kwamba waziri mkuu hajawahi kufanya kazi yoyote ya kishujaa zaidi ya kumsikia akiwa Bungeni kunyamazisha vuguvugu za mabadiliko. Na hili kafanikiwa sana. Nadhani ndio kazi pekee aliyoteuliwa kwayo
   
 19. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #19
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,991
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
   
 20. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  I can only add my thanks to Ulimwengu's majestic article. Bravo!
   
Loading...