Rai ya Jenerali Ulimwengu shambulizi kwa Kikwete?

asante mkuu jounegwelu mbona jina langu umeliweka kwenye inverted commas?.....mimi ni kayagila mzee
 
Nimeipenda "si wavivu wa kufikiri tu, kusoma si magazeti bali hata katiba walioitumia kuapa mara mia hawaifahamu kwa maandishi bali kwa rangi? inawezekana hata rangi hawaijui? NDIO SABABU NEBUKADNEZA ANAISHI KWA KUTOA MAAGIZO AMBAYO YANAPINGANA NA KATIBA NA SHERIA.
 
Kumi, Danieli anasoma ukutani bila shida kwamba nchi sasa inahitaji wazalendo wanaoweza kuongoza mjadala kuhusu masuala ya utawala katika mapana na marefu yake yote, wakati Nabukadneza anakodoa macho, haoni kitu, anawatuma wajumbe wake wakawatangazie raia zake kwamba anaandaa karamu ya kucheza nachi. Raia wanamwambia enzi za nachi zimepita, lakini hang'amui.

Kumi na mosi, imeandikwa kwamba ama Nebukadneza akubali maono aliyopewa na Danieli ama yatokee mabadiliko makubwa ambayo hata Danieli hakuyataraji, lakini hayo mabadilko makubwa yaambatane na vurugu na vilio na kusaga meno.

Kumi na pili, haya yote yameandikwa bayana, na ukuta yalipoandikwa hauko ndani ya kasri ya Nebukadneza; bali umesimama njia panda kuu ya mji, na atakaye kuona ataona, bali asiyetaka kuona hajajaliwa kipawa cha kuona.

JK, Serikali na CCM kwa kwa jumla; Wamepoteza uwezo wa kuona, wamepoteza uwezo wa kusoma,wamepoteza uwezo wa kutafakari na kunusa.

Hizo nilizo zitaja hapo juu ni moja ya njia kuu ambazo binaadamu mwenye akili timamu anaweza kupata ujumbe, ambapo kwa bahati mbaya JK,Serikali na chama tawala wamezipoteza.

Sasa inabaki njia moja kuhisi.Kuhisi kwa kupitia ngozi kwa kupapaswa,kufinywa Kwa bahati mbaya ndiyo njia pekee iliyobakia kuwafikishia ujumbe wetu JK,serikali na Chama tawala bahati mbaya njia hii uambatana na vurugu na vilio vya kusaga meno maandamano migomo kuzomea n.k upande mmoja na kwa upande mwingine serekali na vyombo vya dola mabomu ya kutoa machozi,maji ya kuwasha na hata risasi za moto hapa mauaji majeruhi na vurugu kwa ujumla.

Kwa bahati mbaya gharama ya kutumia njia hii kufikisha ujumbe ni kubwa.

Adha zake tumeisha ziona mauaji na mjeruhi tayari tunao. Kwa Salva itakua vigumu kufikisha ujumbe kwa kipofu na kiziwi (JK} Kwa kumnongo'neza.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Andiko murua. :dance:
"tujipe uwezo wa kusoma maandishi yaliyo ukutani ambayo Danieli anayaona lakini mfalme Nebukadneza hayaoni. Nini kimeandikwa ukutani ambacho watawala wetu wanashindwa kukisoma?"
Niaonavyo mimi ni kwamba mfalme Nebu ameyasoma hayo maandishi. Tatizo lake ni kwamba bado anafikiri himaya yake inaweza kuendelea kushangilia usanii. Rejea ngano ya hivi karibuni ya 'kujivua magamba'!!!!
 
Nafikiri katika tafsiri yangu hii nachi anayotaka kuandaa mkubwa ni hizo sheree kubwa za uhuru akisaidiwa na akina Lukuvi!!!! lakini Daniel amesoma na ni kweli kwamba hatuitaji sheree hizi wakati maisha yanazidi kuwa magumu kila kukicha. Hakika hii ni falsafa nzito sana.
 
Nafikiri katika tafsiri yangu hii nachi anayotaka kuandaa mkubwa ni hizo sheree kubwa za uhuru akisaidiwa na akina Lukuvi!!!! lakini Daniel amesoma na ni kweli kwamba hatuitaji sheree hizi wakati maisha yanazidi kuwa magumu kila kukicha. Hakika hii ni falsafa nzito sana.

Hapa umenifumbua kitu, naenda mapumziko nikirudi naangalia ufumbuzi mwingine kutoka kwa GreaT ThinkerS.
 
rai ya jenerali

maandiko 12 ukutani, nasi twacheza nachi

jenerali ulimwengu
mei 25, 2011


katika makala yangu iliyopita nilisema kwamba tunatakiwa kuacha kupiga chenga masuala muhimu ambayo tunatakiwa tukabiliane nayo na tuyatatue. Nilisema pia kwamba kazi ya kujadili na hatimaye kuandika katiba mpya si kazi ya mzaha wala si kazi rahisi, kwani ni kazi muhimu na nzito na inahitaji utashi mkubwa zaidi kuliko ule unaojidhihirisha miongoni mwetu.

Pia nilisema kwamba katika mjadala huu kila jambo linazungumzika, ispokuwa tu yale yaliyowekewa mizingo na itikadi zenye miiko yake ambayo tunaielewa. Kwa mfano, bila kujali imani ya huyu au yule, sidhani kwamba tutaweza kujadili jambo lo lote linalohusu imani za kidini zinazohusu madhehebu mbali mbali kwa lengo la kukubaliana ni dini gani au madhehebu yapi yakubaliwe na kila raia.


wala hatuwezi kujadili iwapo watoto wanaozaliwa nchini wawe ni wa baba na mama zao au wawe ni wa kijiji au mtaa. Mwanafalsafa wa kiyunani, plato, alijaribu kuonyesha ni jinsi gani mpangilio kama huo ungekuwa na manufaa katika jamuhuri yake, lakini siamini kwamba tutafikia huko katika karne hizi mbili au tatu zijazo.


nadhani pia kwamba hatuwezi kujaribu kujadili kama ni vyema tukawa na utaratibu wa watoto wapendanao kuoana katika umri wa miaka saba alimradi wazazi wao wameridhia, au kwamba ndoa halali zisiendelee kwa zaidi ya miaka 10 kwa kuhofia uchovu wa wanandoa!


nasema, hatuwezi kuyajadili masuala haya kwa sasa kwa kuielewa jamii yetu ilivyoundwa na jinsi mapokeo yanavyotuelekeza katika maisha yetu. Mifano yote niliyoitoa hapo juu haihusu maumbile ya binadamu, bali inahusu utaratibu uliowekwa na jamii na ambao kwa sasa, kwa hali ilivyo, haujadiliki kwa sababu jamii haiko tayari kuujadili, achilia mbali kama ni sahihi au sio sahihi. Na hapa, ikumbukwe, sijazungumzia mjadala tunaoweza kuutamani wa kutaka kubadili utaratibu ili jua lichomoze magharibi na litue mashariki.


jamii ya binadamu siku zote inaendeshwa na taratibu zilizowekwa, na hizi hutokana na historia, desturi, mapokeo na mahitaji ya sasa ya jamii hizo. Hutokea kwamba mahitaji hayo ya sasa yakawa na nguvu kubwa zaidi au ushawishi mkubwa zaidi kuliko mapokeo na desturi, na msuguano unaotokea ukasababisha mtafaruku, lakini baada ya muda mambo yakatulia na jamii ikaendelea kama vile halijawa jambo ingawaje mambo yamebadilika. Mambo mengi hubadilika na yakachukua sura mpya kimya kimya kwa sababu hayatangazwi kwa baragumu ila wenye uwezo wa kuyabaini watayabaini.


aghalabu, hali mpya inayotokana na msuguano huo hujichimbia hadi nayo ikaja kukubalika kama sehemu ya mapokeo na desturi, hadi nayo ikawa ni kikwazo kwa mawazo mapya yanayotafuta njia ya kusonga mbele zaidi. Kwa jinsi hii, jamii nyingi duniani zimesonga mbele karne hata karne, muongo hadi muongo, mwaka hadi mwaka, mwezi hadi mwezi, wiki hadi wiki, siku hadi siku, saa hadi saa, dakika hadi dakika, sekunde hadi sekunde.... Hata kama hatutambui mara moja.


utambuzi huu ni mgumu kwa watu wote ila kwa wale waliojenga uwezo mkubwa wa kubaini linalokuja kabla halijawasili mlangoni na kubisha hodi. Dunia inao watu wengi wanaoweza kubaini mambo haya, mpaka wakakaribiana na hayawani kama mbwa, ngombe, mbuzi, aina fulani ya ndege, na wanyama wengine walio na kipawa cha kunusa mabadiliko katika sayari na kutoa ishara mahsusi ambazo kwa wajuzi ni ishara za tanbihi zinazowafanya wachukue hadhari dhidi ya hatari kama vile tetemeko la ardhi, gharika na maporomoko.


vipawa kama hivi ni nadra na si kila mnyama kapewa. Pia, katika shughuli zinazowahusu binadamu, si kila binadamu anaweza kuwa na vipawa kama hivyo. Kwa kuwa si rahisi kwa kila binadamu kuwa na hivyo vipawa kwa njia za maumbile tu, kama vile hayawani niliowataja hapo juu, binadamu wamelazimika kujifunza kuvijenga vipawa hivyo kwa kuzichunguza jamii waishimo.


sasa, basi, hebu tujaribu kujijengea vipawa kama vile vya wanyama niliowataja hapo juu, vya kuweza kubaini ujio wa mambo ambayo ndiyo yameanza safari kuelekea kwetu, tujipe uwezo wa kusoma maandishi yaliyo ukutani ambayo danieli anayaona lakini mfalme nebukadneza hayaoni. Nini kimeandikwa ukutani ambacho watawala wetu wanashindwa kukisoma?


mosi, imeandikwa kwamba mwaka huu ni 2011, miaka 50 baada ya uhuru wa tanganyika na miaka 47 baada ya mapinduzi ya zanzibar na muungano uliozaa tanzania. Hiyo ni nusu karne katika maisha ya taifa, muda mrefu wa kutosha kwa watu kujiuliza maswali mengi juu ya maisha yao.


pili, ukutani imeandikwa kwamba watoto waliozaliwa mara tu baada ya tanganyika kupata uhuru, mwaka huu wanatimiza miaka 50. Ni watu wazima wanaoelekea uzeeni. Wale waliozaliwa mara tu baada ya mapinduzi ya zanzibar na muungano na wao pia ni wa rika hilo hilo.


tatu, imeandikwa kwamba vijana ndiyo sehemu kubwa ya marika ya nchi hii na hao vijana wana matumaini ambayo hayajawahi kuwakuta wazee wao, na vijana hao wanahamanika kutokana na kuishi katika hali iliyojaa maswali lukuki na majibu karibu na sufuri.


nne, imeandikwa kwamba matumaini ya vijana na matatizo yanayotokana na kutopata majibu kwa maswali yao ni mambo ambayo yanaonekana kuwashinda wakubwa wa siasa na dola, hata angalau kuyafikiria na kuyaelewa. Yanaonekana kama matatizo yenye siri kubwa na ambayo yanahitaji uwezo ambao wakuu wetu hawanao.


tano, ni dhahiri kutokana na maandishi yaliyo ukutani kwamba vijana wanaamini kwamba matataizo yao yana utatuzi, lakini wakuu wa siasa na dola hawana uwezo wa kuuona utatuzi huo kwa sababu hiyo si azma yao; kwani wamezama katika shughuli nyingine ambazo hazihusiani na utafiti wa utatuzi huo.


sita, imeandikwa kwa herufi za moto kwamba nchi imepoteza mwelekeo na imekuwa ikielea kwa muda mrefu, imeacha misingi yake ya awali iliyoijengea mshikamano, umoja, upendo na amani na badala yake tunavuna ubinafsi, ubaguzi, utengano, dhuluma na migawanyiko inayotishia amani kwa kiwango cha kutisha sasa.


saba, imeandikwa bayana kwamba iwapo mabadiliko makubwa, ya haraka na ya kina hayatafanywa katika kipindi kifupi kijacho , na kama hali ya kuelea itaendelea kutusogeza mbali na pwani yetu, kuna hatari ya kweli ya kupatwa na hasara kufa na maafa tusiyotarajia, hususan kutokana na wanasiasa na wenzi wao (pamoja na familia zao) wenye uchu wa madaraka na mali.


nane, inasomeka ukutani kwamba kinachoweza kulinusuru taifa kwa sasa ni mkusanyiko wa wazalendo walio tayari kujiunga kwa lengo la kuisaidia nchi yao ili kuirejesha katika misingi ya awali iliyotajwa hapo juu kwa kupambana dhidi ya kutojali, upuuzi, ufisadi, wizi, ubadhirifu, ulaghai, ubazazi, udanganyifu, uonevu, woga, ubarakala, unafiki, uzandiki, na u-mimi-na-familia-yangu.


tisa, ukuta umebeba bango linalosema kwamba haya yote yanatokea kwa sababu nchi imekosa uongozi na hilo limetokea kwa sababu ya mifumo ya hovyo, iliyochoka na ambayo haitoshelezi matakwa ya kiuongozi na ya kiutawala inayolingana na mahitaji ya karne hii.


kumi, danieli anasoma ukutani bila shida kwamba nchi sasa inahitaji wazalendo wanaoweza kuongoza mjadala kuhusu masuala ya utawala katika mapana na marefu yake yote, wakati nabukadneza anakodoa macho, haoni kitu, anawatuma wajumbe wake wakawatangazie raia zake kwamba anaandaa karamu ya kucheza nachi. Raia wanamwambia enzi za nachi zimepita, lakini hangamui.


kumi na mosi, imeandikwa kwamba ama nebukadneza akubali maono aliyopewa na danieli ama yatokee mabadiliko makubwa ambayo hata danieli hakuyataraji, lakini hayo mabadilko makubwa yaambatane na vurugu na vilio na kusaga meno.


kumi na pili, haya yote yameandikwa bayana, na ukuta yalipoandikwa hauko ndani ya kasri ya nebukadneza; bali umesimama njia panda kuu ya mji, na atakaye kuona ataona, bali asiyetaka kuona hajajaliwa kipawa cha kuona.


Nkosi Sikelelii i Tanzaniaaaaa.........!!!!! Mooja, Mbilii, Tatu...!
 
mhhh uyu mzee anajua kuandika na yuko very reflective kwenye issues zake...naprinti hii niweke kwenye archive zangu kwa ajili ya reference siku zijazo akina gaude waje kusoma maandiko haya
 
Mkulu anapaswa kujaribu kubadilika kwasababu hali ni mbaya wanajamvi kuliko tunavyofikiri maana huwa najiuliza sisi tunaopata net za more than million hali iko hivi je kwa wale wanaopata eighty plus wanaishijemungu tusaidie!
 
Kazi nzuri sana. Nani atakaetafsiri haya maandiko kwa rais? Atleast awe hata na huruma, ajaribu kuthubutu kutatua matatizo ya Watanzania. Mheshimiwa rais, chonde chonde, waonee huruma watanzania wanaoteseka mahospitalin, waangalie na watoto wanaosoma shule ambazo kufanikiwa kwao ni ndoto kutokana na ukosefu wa vitendea kazi. Historia itatuhukumu ikiwa tunaishi nchi iliyobarikiwa maziwa na asali lakin leo hii ni miaka 50 ya uhuru lakini hakuna ahueni yoyote. Tunasema Mungu aibariki Tanzania kwa lipi tena, wakati alishatubariki tukashindwa kuzitumia baraka zake? Inavyoonekana ni sawa na mtu anaemwomba Mungu asipate ajali ili hali anaendesha gari rafu barabarani. Je ukipata ajali utamlaum Mungu au wewe mwenyewe? Viongozi wetu acheni kuweka pamba masikioni, watanzania tumechoshwa, hatuwezi tena! Tafadhali someni alama za nyakati. Wadau wamesema wamechoka, kuhusu mwenendo wa Nchi yao, kilichobaki ni kuwa "Sikio la kufa halisikii dawa", au "Asiyesikia la mguu huvunjika guu". . Nampongeza Ulimwengu kwa kazi zake nzuri za kifasihi ambapo mbali na kuelimisha zinatufumbua macho na kutambua uovu wa viongozi wetu. Long live Ulimwengu.
 
tanzania miaka 50 ya uhuru 2011.jpg

Kwa waandaji wa sherehe za miaka 50 ya uhuru: je na hii itakuwa mojawapo ya picha zitakazopamba MABANGO ya DAR. Hatuna budi tujivunie matunda ya miaka 50 ya uhuru - angaa watoto wetu (taifa la kesho) tumeweza kuwapeleka shule!!!!!!:dance:
 
RAI YA JENERALI

Maandiko 12 ukutani, nasi twacheza nachi

Jenerali Ulimwengu
Mei 25, 2011


KATIKA makala yangu iliyopita nilisema kwamba tunatakiwa kuacha kupiga chenga masuala muhimu ambayo tunatakiwa tukabiliane nayo na tuyatatue...
haya yote yameandikwa bayana, na ukuta yalipoandikwa hauko ndani ya kasri ya Nebukadneza; bali umesimama njia panda kuu ya mji, na atakaye kuona ataona, bali asiyetaka kuona hajajaliwa kipawa cha kuona.

1. Sasa Jenerali anafanya ile kitu ambayo nilitamani aifanye huko nyuma 1995, pale alipoamua kumpigia kampeni Ben Mkapa. kwa mawazo yangu, Jenarali alitakiwa kukaa katikati na kumwaga falsafa ambazo zingewasaidia wote: CCM na vyama vingine, na sisi wengine, kuelewa mchezo unavyokwenda na kuchagua kete ya kucheza. kuelewa au kuusoma mchezo ni kazi kubwa sana wanahitajika watu wenye vipawa kama Jenerali kuonesha njia. sasa wakati ule alijitoma kumbeba Ben Mkapa, na kilichofuatia ni historia.

2. "...tunatakiwa tukabiliane nayo na tuyatatue..." baada ya kusoma hayo maandishi 12 yaliyoandikwa katika ukuta ambao wala haujafichika, upo njia panda kila mtu anaona, sasa tufanye uamuzi. binafsi naangalia matukio yanayoendelea kule Uganda, ambapo Museveni ameamua kutumia nguvu kubwa ya dola kuzima moto wa Besigye. inaonekana watawala wetu nao wameamua kuazima mbinu hizo, hivyo badala ya kuruhusu mazishi ya Tarime yafanyike kwa uongozi wa CHADEMA, ambayo ingekuwa repeat performance ya Arusha, na CHADEMA wakapata political gain, waliamua kutumia maguvu ya dola na kusambaratisha ile kitu yote. binafsi naamini hapakuwa na haja ya dola kutumika pale. ni CCM ndio walitakiwa kutoa jibu la kisiasa kwa goli ambalo walishafungwa na CHADEMA, pale ambapo wanasheria wake waliwezesha kufanyika post mortem ambayo ni very damaging kwa serikali ya CCM. ubabe ulikamilishwa kwa kuwadhalilisha na kuwasweka ndani vigogo kadhaa wa CHADEMA, akiwemo mpambanaji wa siku nyingi: Tundu Lissu

3. Nimechukua mfano huu wa Tarime kuonesha kwamba bila ya watanzania kukubali kukabiliana na uongozi wa kibabe wa watawala wetu, BILA WOGA, wote tutakuwa tunaishia kucheza nachi, pamoja na kusoma maandiko hayo. akina Tundu Lissu wamelala ndani kwa niaba yetu sote tunaoitakia mema nchi yetu. pale ambapo Polisi wamefanya mauaji, na polisi hao hao wanatumia dhamana waliyonayo kufunika madhambi yao, na wanatumia dhamana hiyo pia kupambana na wale ambao wanajaribu kufichua madhambi ya polisi - kama tutameza yote hiyo na kujidai tumeelewa hayo maandiko, huo ni mchezo wa nachi, tena mzuri tu.

4. Katika nchi ambayo dhahabu imepanda bei duniani, na sisi bado tunalalama katika lindi la umaskini, huku tukiruhusu dhahabu yetu inaporwa mchana kweupe. eti mradi mimi nina ka kazi kanakonipa mshahara, basi mwingine alie tu. au mimi ninafaidika kidogo na makombo wanayodondosha wakubwa, wengine walie tu. nadhani tufike mahali tuseme No! tuungane na wale ambao wapo tayari kutoa muda wao na hata kujitia katika hatari, tuwaunge mkono kwa njia mbalimbali, kuonesha kwamba angalau tunaelewa uzito wa maandishi hayo, na kwamba tumeshachoka kucheza hiyo nachi
 
He! Huyu anamzodoa muislamu mwenzake

Hakika maneno yenye kuwapanga watu kwa makundi ya udini yanakera. Hivi kweli Mkuu unashindwa kujadili hoja zilizotolewa kwa mtiririko wa hadithi bila kufikiria dini ya Mwandishi,Mwanzisha thread au anayepewa ujumbe? Kuwa taifa kwanza acha mambo ya udini...
 
Raiamwema sasa linarudi kwa enzi yake ya uchambuzi makini na wenye tija kwa wasomaji na watawala..watake wasitake!!!isingekuwa mafisadi leo wangekuwa mbali sana bahati mbaya walivurugwa sana na mafisadi
 
Back
Top Bottom