RAI:Waslamu wote unganeni kupinga mashambulizi ya kigaidi yanayotumia mgongo wa dini

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,318
50,532
Asalam alyeukum,
Ni muda mrefu sasa dini ya kislaamu imekuwa ikishtumiwa kujirusha na matendo mabovu na ya kinyama. Baadhi wamepinga madai hayo Kwa hoja nzuri tu kuwa uislamu ni dini safi dini inayopenda amani na hivyo kwa msingi huo basi wale magaidi wanaotuua wanakosea, lakini jambo hili linaendelea kuchafua sana hii dini.. Swali la kujiuliza ni kwanini Waslamu hamkemei matendo hayo na badala yake baadhi wanayaunga mkono kisa wanaouliwa ni wa dini tofauti na wengi wanayapinga mashambulizi wanayofanyiwa na mataifa ya magharibi pamoja na kuwa operesheni hizo zina walakini kidogo (propaganda).. Lengo langu sio kubomoa bali kujenga na staki tubishane. Kwa heshima na taadhima naomba Kutoa wito kwa ndugu zetu waislam kama kweli mnachukizwa na mauaji yanayopewa jina jihad na kwamba Mwenyezi anapenda tuish kwa amani basi anzeni kuhamasishana misikitini na kwenye jumuiya zenu mfanye maandamano ya amani na kampeni endelevu ya kuifanya dunia salama kwa kupinga mashambulizi ya vikundi vya kigaidi kutumia vifungu vya dini hii kutekeleza mauaji yao.hilo litasaidia sana kwani litawafanya vikosi hivo kubaki bila Sapoti yoyote..najua mwanzo ni ngumu lakini kama mna nia ishallah mtafanikiwa na Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi
 
Back
Top Bottom