Rai: Vyombo vya Habari VISUSIE Habari za mkuu wa mkoa Dar kuanzia Leo

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
812
Kutokana na Mkuu wa Nchi hii kukataa kuchukua hatua kwa matendo yanayomhusisha Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaama juu ya tuhuma kibao zinazomkabili ikiwemo Uhalali wa Majina na Vyeti Vyake, Kutumia Magari au Mali za Wauza Madawa ya Kulevya aliowataja yeye Mwenyewe (Matumizi mabaya ya Ofisi na Ufisadi), NA KUBWA ZAIDI kuvamia chombo cha habari kwa Mitutu ya Bunduki na kuchukua FlashDisk na kusambaza recording kinyume cha sheria, nawaomba wanajf ambao sisi ni pia ni sehemu ya wadau wa vyombo vya habari tuazimie kushauri yafuatayo:-

1. Vyombo vya Habari vyote ambao ni mhimili wa NNE i.e Radio, Magazeti na Television VISUSIE kutangaza habari zozote zinazomhusu au zinazomhusisha mkuu wa mkoa aidha za kwake mwenyewe au za kushirikishwa mpaka pale atakapojiuzulu.

2. Vyombo vya Habari, vimpeleke Mahakamani kulingana na uvunjaji mkubwa wa haki za wanahabari, uhuru wa vyombo vya habari na maadili ya kiuongozi kutokana na uvamizi alioufanya (maana hana kinga yoyote kisheria).

3. Mwendesha Mashtaka Binafsi (ambaye ameshapatika, Boniface Jacob) aendelee kufungua kesi kuhusiana na tukio la Makonda kughushi identity na vyeti. (maana hana kinga yoyote kisheria).

4. Wananchi wasimpe ushirikiano popote atakapokuwepo na ikiwezekana wamzomee kwa kutaja jina lake halisi la Bashite kumshinikiza ajiuzulu. Hii mbinu inatumika na inakubalika katika nchi yenye demokrasia kama Tanzania.

5. Vyama vya Siasa au NGOs zianzishe vuguvugu la maandamano kupinga BOND hii isiyosikiliza haki za Binadamu katika utendaji wake (refer.. kutaja majina watu hadharani bila ushaidi na kusababisha defamation, kudharau wafanyakazi wa serikali na kuwaita vichaa, kuvamia kituo cha habari na kupiga waandishi wa habari etc etc)

6. Viongozi wa Dini zote, kwa Pamoja wakemee na kulaani kitendo cha uvamizi kwa vyombo vya habari na kumtaka Mkuu wa Mkoa aombe radhi.


Wakuu salam. Sitakuwa na mengi ya kuzungumza kwani naamini kila mmoja atakuwa anafahamu mambo yanayoendelea nchini kuhusu huyu bwana mdogo Bashite majuzi alichokifanya Mawingu FM, kauli aliyoitoa Waziri Nape leo hii, na majibu ya shombo aliyoyatoa faru joni mchana huu ambayo yameacha sintofahamu kubwa kwa wanaopenda na kuheshimu utawala wa sheria nchini.

My take
Mimi naamini kupitia vyama vyenu, waandishi wa habari mkiamua kuwa kitu kimoja na kuamua kutoripoti habari yoyote ile inayomuhusu huyu dogo mwenye kiburi DSM itakuwa ni 'psychological torturer' kwake kwani bila media huyu dogo hawezi ku survive.

UPDATE: 22/MARCH/2017 - TEC NA KLABU YA WAANDISHI VYAMFUGIA VIOO MAKONDA

 

Attachments

  • WhatsApp Image 2017-03-22 at 11.00.33.jpeg
    WhatsApp Image 2017-03-22 at 11.00.33.jpeg
    84.2 KB · Views: 72
Siyo za Makonda tu bali na za malaika mkuu ndani ya nchi na nje ya nchi. Maana anamlinda huyu jambazi.

Well spoken brother. Vyombo vya habari vianze na huyu, maana Raisi anayo kinga ya kutoshtakiwa akiwa madarakani. Kinachowezekana kwa sasa ni huyu 'mungu' wa darisalama aliyethibitishwa leo pale ubungo. HANA KINGA YOYOTE... Asusiwe habari zake na tumburute mahakamani
 
Mkuu kwa maoni yangu na huyu anayelinda huu ujambazi wa huyu mhuni naye pia wamtenge. Yeye ndiye aliyemteua na kuna taratibu za sheria za kazi nchini na pale zinapokiukwa mhusika ni lazima aadhibiwe ikiwemo kuondolewa madarakani. Kafoji vyeti vya elimu malaika mkuu kimyaaaa, kavamia chombo cha habari malaika mkuu kimyaaa! Ina maana anaunga mkono uvunjwaji wa sharia za nchi huyu! Ni lazima vyombo vya habari nchini viamue kumtenga mpaka atakapomuondoa huyo mhuni.

Well spoken brother. Vyombo vya habari vianze na huyu, maana Raisi anayo kinga ya kutoshtakiwa akiwa madarakani. Kinachowezekana kwa sasa ni huyu 'mungu' wa darisalama aliyethibitishwa leo pale ubungo. HANA KINGA YOYOTE... Asusiwe habari zake na tumburute mahakamani
 
Y'all just don't get it. At this point, Makonda is only another villain behind the villain. I can't help but believe Makonda is only acting on Joker's interests. We should all go for the main villain.

In the course of going for the Main Villain, we should get down this younger villain...and then focusing on the Main. Believe Me. Makonda should go down first
 
Back
Top Bottom