Rai tume ya uchaguzi itangaze mapema kuhairisha uchaguzi wa udiwani katika kata zote za arusha mjini

Mr Emmy

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,219
550
Kwanza natoa pole kwa watanzania wote wapenda amni nchini Tanzania kwa tukio baya kabisa lililotokea jana katika Jiji la Arusha.

Natoa pole za dhati kwa wafiwa na majeruhi wote wa tukio la bomu na pole nyingi kwa Chadema kwani huu ni msiba mkubwa sana kwao.

Kutokana na tukio baya kama hili napenda kuishauri tume ya uchaguzi kuhairisha chaguzi zote ndogo za udiwani katika kata zote za jiji la arusha ili kuwawezesha wanachi wote kushiriki kwa amani katika maombolezo ya vifo vilivyotokea kutokana na tukio la ugaidi lilofanywa na watu wapuuzi kabisa.

Mwisho watu wote ambao wanatiliwa mashaka na wananchi kuhusika na tukio hili ni bora police ikaanza kuwajamata na kuwahoji kwa upelelezi hata kama ni viongozi wakubwa wa vyama vya siasa

no way out kwa hili la kumwaga damu zisizo na hatia watanzania tutaungana na kupambana na wote wasioitakia mema nchi yetu bila kujali itikadi zetu za kisiasa.

Shimeshime Police na Tume ya taifa ya uchaguzi futeni maramoja uchaguzi wa leo ili kuwawezsha wana arusha kuomboleza kwa amani


Poleni tena wafiwa, majeruhi na wanachadema wote kwa yote yaliyowatokea hakika mimi kama mwana ccm mpenda amani naungana na watu wote kulaani tukio hili nanataka wote waliohusika wakamatwe mara mojo pasipo kujali uraia wao, ukabila wao, udini wao, rangi yao, umaarufu wao na vyama vyao vya siasa.
 
Kwahiyo mlijipanga kwa ajili ya hilo sio?! Shame on you ccm..
Hakuna cha uchaguzi kusitishwa wala nini?. Kesho asubuhi tunakwenda kupiga kura na tutawazika ndg zetu.
 
Natarajia tume ya uchaguzi kuhairisha chaguzi zote zilizokua zifanyike kesho kwasababu mshiriki mmoja muhimu yupo ktk msiba wa kiongozi na wanachama wake walio jeruhiwa!
 
Hakuna kuahirisha uchaguzi wa madiwani arusha???????????????????? Ulikuwa mpango mzima wa wapinzani nzetu akina Nepi na Mguu Chemba.
Poleni sana wafiwa, katika kipindI ihiki kigumu, lakini damu ya walio uwawa iko juu yenu nyie mlio panga mauaji hayo. Via chadema viva!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wajo hilo siyo muafaka hata kidogo,kwa kuwa upo uwezekano mkubwa kuwa huo mkasa,ukawa umepangwa na magamba,baada ya kufanya tathmini,na kugundua kuwa hawana uwezekano,hata wa kuambulia kata moja!!

Kwa hiyo kinachopaswa kufanywa na wana Arusha,ni kujitokeza kwa wingi mno kupiga kura na kuwapa adhabu hao waliopanga njama hizo,za kukataa kushindwa kwa kutumia sanduku la kura.

Vile vile,hilo lililotokea Arusha linaweza kuwa ushahidi mwingine wa mazingira,wa kauli zinazotolewa mara kwa mara,na viongozi waandamizi wa chama tawala kuwa CCM itatawala milele!!

Vile vile siafikiani na wazo lako kuwa jeshi letu la polisi ndilo lipewe jukumu la kufanya upelelezi wa tukio hilo,kwa kuwa kama ilivyotokea kwenye matukio ya nyuma,usije ukashangaa,jeshi letu hilo,likatoa taarifa ya kuwa ,Chadema ndiyo wamehusika moja kwa moja,na kadhia hiyo,kwa kuwa viongozi wake,wamewahi kutamka kuwa kama watawala wa nchi hii,hawatarekebisha mwenendo wao wa kuwagandamiza raia wake,upo uwezekano wa kufika mahali,nchi itashindwa kutawalika!!

Hebu pia tujiulize jeshi hilo la polisi,kama huko siku za nyuma lilifanya juhudi zozote za kuwakamata watuhumiwa,kama vile la utekaji nyara wa Ulimboka na Kibanda,mauaji ya mwandishi Mwangosi huko Iringa na hata hili tukio la hivi karibuni la kutupwa kwa bomu kanisani,ambapo,kulisababisha mauaji ya raia kafhaa,wasio na hatia,ambapo hadi sasa aliyeburuzwa,mahakamani ni kijana mmoja tu,dereva wa boda boda,ambaye inasemekana,ndiye aliyembeba abiria aliyetupa bomu kanisani!!

Kwa mazingira hayo,ambapo mkuu wa nchi anaendelea kuwapandisha vyeo makamanda wa mikoa,ambao wamesababisha vifo vya raia,katika mikusanyiko ya vyama vya siasa vya upinzani,ni vigumu mno kwa mkuu wetu huyo wa nchi,kukana kuwa,halitumiii,jeshi hilo,kwa manufaa ya chama chake tawala,ambacho siku zote,viongozi wake waandamizi,wamekuwa,wakijigamba kuwa chama chao,kitatawala nchi hii milele!!

Kwa wana Arusha,kazi ya kufanya ni moja tu,kujitokeza kwa wingi sana na kupiga kura za kukitaa chama,ambacho kinataka kidumu madarakani,hata kwa kutumia njia za maafa ya wananchi!!!
 
Maccm lengo lao kuua kama jana ili uchaguzi uahirishwe,hakuna hiyo kitu.NAJITOKEZA MAPEMA KWENDA KWENDA KUPIGA KURA.
 
Hatimaye taarifa zilizotoka asubuhi hii ni kuwa uchaguzi wa madiwani kata zote za arusha umeahirishwa hadi tarehe 30/6/2013. Poleni wafiwa wote, mungu awatangulie.
 
Back
Top Bottom