RAI: Sangoma kutoka Kenya wakodishwe kukamata mafisadi Tanzania

Kifyatu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
3,385
2,000
Lazima tukubali Kenya ina sangoma viboko ile mbaya.

Mifano:
1. Kama mke au mume wako anachepuka basi sangoma wa Kenya wana dawa zakuwafanya hawa wachepukaji kunasiana wakati wa tendo la ndoa mpaka wewe mwenye mali uje uwanasue.

2. Hivi juzi bwana mmoja aliibiwa/alitapeliwa gari na mwizi mmoja. Mwenye gari hakwenda polisi bali alikwenda kwa sangoma. Sangoma alifanya vitu vyake na kumwambia mwenye gari atulie na kuwa huyo mwizi atalirudisha hilo gari na kujipeleka polisi mwenyewe. Kweli kabisa, baada ya siku tatu yule mwizi alishambuliwa na nyuki ndani ya lile gari la wizi na kujikuta anakimbilia polisi na funguo za gari la wizi mkononi.

WAZO
Hivi kwa nini Tanzania isiwakodi hawa sangoma kutoka Kenya kuja kufanya hizi dawa kuwakamata hawa mafisadi papa/nyangumi hapa nchini.

Fikiria kama wale wote waliokwapua hela za:
1. Eskro
2. IPTL
3. Meremeta
4. Mikataba mibovu ya madini
5. Wezi wa TRA
6. Uuzwaji haramu wa wanyamapori
7. Waliojenga majengo ya kufuru (mahekalu) kwa fedha chafu
8. n.k.

wangeng'atwa na nyuki mpaka wote wakimbilie Ikulu kurudisha visafleti vya pesa walizikwapua au kurudisha hatimiliki za mahekalu na maturbo V8 waliyoiba.

Mnaonaje, wazo langu lina mashiko?
 

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
1,998
2,000
Unataka wakuu wa nchi walostaafu wang'atwe na nyuki sio!! Si haki, katiba inawalinda.
 

dem boy

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
2,658
2,000
Nani aende akawaloge maana kila mtu fisadi nchi hii,hao mafisadi wanaeza fika ikulu na vi saflet vya pesa wakakuta mkuu nae yupo feri kule anapanda pantoni kukimbia hao nyuki

Yaani unakata tawi ulilokalia
 

mlimilwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,335
2,000
Mbona huko Kenya ndio kunamafisadi kuliko Tanzania,inamaana hawataki kufanya hivyo?
 

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,844
2,000
Hao masangoma ndio wanao walinda wana siasa na viongozi huo ugomvi utakuwa wa masangoma kwa masangoma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom