RAI - Mgogoro CCM: Siri nzito zavuja; Mgogoro wa Arusha ni urais wa 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAI - Mgogoro CCM: Siri nzito zavuja; Mgogoro wa Arusha ni urais wa 2015

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by nngu007, Jun 10, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Friday, June 10, 2011

  *Mgogoro wa Arusha ni urais wa 2015
  *Wenyeviti UVCCM 11 kumfuata Millya
  *Wenyeviti wilaya wamwandikia Mukama


  Na Waandishi Wetu

  MBIO za urais wa mwaka 2015 ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimekivuruga chama hicho katika Mkoa wa Arusha, hali inayotishia hatma yake.

  CCM wanagombana ilhali wakitambua kuwa mkoa huo ni miongoni mwa ngome madhubuti za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), hivyo mgogoro wowote utakuwa na manufaa kwa wapinzani.

  Tangu kumalizika kwa kura za maoni na Uchaguzi Mkuu, kumeibuka makovu makubwa ya kisiasa, na wachunguzi wa masuala ya kiasiasa wasema busara za Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha ndiyo inayoweza, ama kukiokoa chama, au kukiua.

  Kwa wiki kadhaa MTANZANIA imefuatilia kile kinachoitwa kuwa ni mvutano miongoni mwa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)-wenyewe kwa wenyewe- kwa upande mmoja; na viongozi wa UVCCM dhidi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda.

  Baadhi ya viongozi wa UVCCM wanaokabiliwa na hatari ya kupoteza uanachama wa CCM ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James ole Millya, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Mjini na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Ally Bananga, Fatma Ngairo, Philemon Ammo, John Nyiti ambaye ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arumeru, na Ally Majeshi.

  Hasimu wao mkuu aliyekuwa chanzo cha kuibuka kwa mtafaruku huo ni Mrisho Gambo, ambaye inatamkwa bila ushahidi kwamba alishangilia baada ya CCM kupoteza jimbo la Arusha. Chaguo lake kwenye kura za maoni, Felix Mrema, alishindwa na Dk. Batilda Burian, kwenye kura za maoni

  "Hawa vijana wana nguvu na ushawishi, huwezi kuamua kuwafukuza kienyeji tu na vijana wakaendelea kukitumikia chama.

  "Hatuwezi kuwafukuza kwa sababu kuna hatua kama nne hivi kabla ya mwanachama kufukuzwa. Kuna kupewa onyo, onyo kali, karipio na karipio kali-haya yote hayajafuatwa- itakuwa ajabu kuwafukuza wanachama kwa sababu tu wameonyesha hisia zao," amesema mmoja wa wazee waliozungumza na MTANZANIA mjini Arusha.

  Kutokana na hali ya mambo kwenda mrama, wenyeviti wa CCM wa wilaya zote za Mkoa wa Arusha wamemwandikia barua Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama.

  Taarifa kutoka Makao Makuu ya CCM zinasema kwamba barua hiyo iliandikwa Juni Mosi, mwaka huu na kusainiwa na wenyeviti hao. Maudhui makuu ni ushauri wao ambao wanasema ukizingatiwa utakiokoa chama hicho kutoka kwenye hatari ya kusambaratika.

  "Wameleta barua, ina mapendekezo kama matano hivi, wanaomba, kwa manufaa ya chama, Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda ahamishwe mara moja.

  "Wanapendekeza njia ya mazungumzo itumike kumaliza mgogoro ulioibuka baadala ya kutumia rungu la kufukuzana.

  "Wanataka Chatanda na viongozi wote wa CCM na UVCCM wapigwe marufuku kuropoka kwenye vyombo vya habari juu ya migogoro inayoendelea," amesema mmoja wa viongozi walio CCM Ofisi ndogo za Makao Makuu, Lumumba jijini Dar es Salaam.

  Kadhalika, wenyeviti hao wanasisitiza umuhimu wa vijana kukosolewa na kuonywa na viongozi wa juu wa CCM badala ya malumbano hayo kufikishwa kwenye vyombo vya habari.

  Wenyeviti hao wanakiri kwamba tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kumeibuka makundi makubwa na hatari ndani ya chama hicho.

  "Wakati wa kura za maoni Chatanda aliamua kuegemea kwenye kundi fulani lenye ushawishi wa fedha ndani ya wilaya mbili za mkoa wa Arusha, inasemekana tangu awe Katibu wa CCM katika Mkoa wa Arusha hajawahi kuhudhuria kikao chochote cha UVCCM kwa mujibu wa Katiba," kimesema chanzo kilichosoma mapendekezo ya wenyeviti hao.

  Chatanda anatuhumiwa pia kutoelewana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole, kiasi cha kutuhumiwa kutoa maneno ya kumdhalilisha.

  Anatuhumiwa kugombana na wajumbe wanne hadi sasa wa Kamati ya Siasa ya Mkoa. Miongoni mwa wanaodaiwa kugombana naye ni Mjumbe wa NEC Mkoa wa Arusha, Elishilia Kaaya, Millya, Abrahamani Konje na Majid Mwanga.

  Wenyeviti wa CCM wa Wilaya wanasema mgogoro umekuwa mkubwa kutokana na Chatanda kuamua kuingilia masuala ya UVCCM moja kwa moja, ilhali akitambua kuwa Jumuiya hiyo imepewa mamlaka ya kujiendesha, isipokuwa pale itakapohitaji ushauri au ‘kurejeshwa kwenye mstari'.

  Chatanda ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu, analaumiwa kutumia muda mwingi kwenye shughuli za ubunge badala ya shughuli za chama mkoani mwake.

  "Wanasema kwa sasa shughuli za chama na vikao muhimu vinapangwa siku za mwishoni mwa wiki kwa sababu Katibu (Chatanda) siku za katikati ya wiki anakuwa bungeni.

  Wanataka achague moja, kama hataki chama kiamue," kimesema chanzo chetu.

  Nakala ya barua ya wenyeviti hao imepelekwa kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, Mjumbe wa NEC Mkoa wa Arusha, Elishilia Kaaya na kwa Chatanda.

  Wakati Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha ikiketi leo kutoa uamuzi wa ama kuwafukuza, au kutowafukuza vijana hao, kuna habari za uhakika kwamba kundi lililodhamiria kuvunja ngome ya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, limekuwa likihaha kuhamasisha wajumbe wa kikao hicho ili waidhinishwe kutimuliwa kwa Millya na wenzake.

  Kundi hilo inasemekana linapata ufadhili mnono kutoka kwa mmoja wa mawaziri wenye dhamira ya kuamua nani awanie urais mwaka 2015; pamoja na kijana wa mmoja wa viongozi wakuu nchini ambaye kwa siku za karibuni amekuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa ndani ya UVCCM na hata CCM kwa jumla.

  Kwa mujibu wa watu walio karibu na waratibu wa kundi hilo, lengo la kumwondoa Millya na wenzake ni kuhakikisha kwamba Lowassa anapoteza uwezo wa kugombea urais mwaka 2015, au hata kama hatagombea yeye, basi atakayemuunga mkono ashindwe kufanikiwa.

  MTANZANIA imefanikiwa kupata baadhi ya vilelezo vya mawasiliano kati ya vinara wa mkakati wa kummaliza Millya na Lowassa, kwenda kwa mawakala wao mkoani Arusha.

  Kubwa linalojadiliwa na kundi hilo ni kuhakikisha unatumika ushawishi wa kila hali ili mtandao wa Lowassa umalizwe kabisa. Washiriki wa mkakati huo wanakiri kuwa Lowassa ana nguvu kubwa, kwa hiyo asipodhibitiwa sasa anaweza kuwasumbua kwenye kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015.

  Suala la urais mwaka 2015 linaonekana kuwapa kiwewe hata viongozi waandamizi ndani ya CCM. Hivi karibuni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara) Pius Msekwa, amenukuliwa akimsihi Lowassa ajitoe NEC na aache na harakati za kuwania urais.

  "Mgogoro wa Arusha ndani ya CCM ni urais mwaka 2015, waziri yule bado anataka ahakikishe Lowassa anamalizwa kabisa, wanajua wakishammaliza Arusha itakuwa kazi rahisi kuwamaliza vijana wengine wanaomuunga mkono Lowassa au ambao hawakubaliani na njama za kuchafuana ndani ya CCM.

  "Nakuhakikishia kuwa baada ya Millya anaweza kufuata Shigella (Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Martin Shigella, mmoja wa wafuasi wa Chatanda amesikika akisema wazi wazi.

  "Walianza kuwamaliza kina Bashe, wakaja kwa Masauni sasa ni Millya, lakini hawataishia hapo, watakwenda hadi kwa kina Mathayo Marwa (Mwenykiti UVCCM Mkoa wa Mara), Msomba (Mbeya), Fadhil Ngajilo (Iringa), Zainab Kawawa (Mbunge), Catherine Magige (Mbunge), Mwenyekiti UVCCM Tabora na Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Mwanza, Magembe, Tauhida (Mwenyekiti Vijana Mkoa wa Mjini Magharibi).

  "Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kigoma, Anold; Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Mtwara, na wengine wengi. Kazi hii inafanywa na mtoto (mtoto wa kigogo mwandamizi ndani ya Serikali na CCM). Utaona tu kazi ya kuwapukutisha wote wanaodhaniwa kuwa ni threat (hatari) kwa harakati za urais mwaka 2015," kimesema chanzo chetu.

  Ngajilo aliundiwa kesi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), akituhumiwa kutoa rushwa ya Sh 30,000 (elfu thelathini) kwa hoja kwamba aliwagawia watu 30. Mkakati wa kesi hiyo ulisukwa na mtoto wa kigogo katika mpango wa kumwandalia mazingira Monica Mbega ili aweze kuteuliwa na chama kugombea ubunge Jimbo la Iringa Mjini.

  Ngajilo kwa kutambua njama hizo, alimtumia ujumbe wa maandishi mtoto huyo wa kigogo. Kwa sababu hiyo, amewekwa kwenye orodha ya vijana wa UVCCM wanaopaswa kuwa nje ya umoja huo ifikapo 2012 ili wasishiriki uchaguzi ndani ya chama.

  Uchaguzi wa mwaka 2012 unachukuliwa ndiyo maandalizi mahsusi kwa ajili ya kambi mbalimbali zinazotaka kuwania urais mwaka 2015.

  Magembe ameibuliwa kesi ya utapeli. Tuhuma dhidi yake ziliibuliwa mwaka 2008, lakini ziliachwa na sasa katika mazingira ya fitna za kisiasa, zimeibuliwa baada ya kuonekana kuwa ni mfuasi wa Masauni.

  Marwa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji, mkakati madhubuti ulisukwa dhidi yake baada ya Masauni kung'olewa. Aliibuliwa tuhuma ya kuwa na umri mkubwa na ulitumika mkakati ule ule uliotumika kwa Masauni wa kusambaza ujumbe wa simu na karatasi. Tuhuma hizo zilikosa mashiko na hivyo kupuuzwa na wajumbe wengi wa UVCCM.

  Tauhida, alipigwa zengwe kwenye uchaguzi wa ubunge kupitia Vijana mwaka jana. Hoja kubwa dhidi yake ilikuwa kwamba amezidi umri na asipewe kura kwa sababu hayumo kwenye karatasi ya maelekezo. Kuhusishwa kwake na Masauni na kutokuwamo kwenye karatasi ya maelekezo kulimsaidia kushinda.

  Neema Mgaya (Mbunge) alishambuliwa kwa kutokuwamo kwenye karatasi za maelekezo na zikatengenezwa nyaraka za kughushi kwamba kaolewa Bomani na umri wake umezidi. Kwenye vikao alithibitisha kwa vielelezo kuwa aliolewa Kiislamu kwa ndoa halali.

  Anold aliibuliwa tuhuma ya umri, lakini baada ya kukosekana ushahidi, sasa katengenezewa tuhuma ya kummaliza kiuchumi kwa kumtaka ahame eneo aliloweka karakana kwa maadai kwamba ni la wazi.

  Baadhi ya viongozi wa UVCCM Mkoa wa Arusha walio kwenye orodha ya kuvuliwa uanachama wamezungumza na MTANZANIA kwa hisia kali na kuweka bayana msimamo wao.

  "Kama James (Millya) atachukuliwa hatua zisizostahili, au za kuonewa kwa ajili ya kulinda maslahi ya baadhi ya watu, sisi tutakuwa naye katika uamuzi huo.

  "Tutakuwa naye na ikibidi sisi sote tutaandamana usiku na mchana kudai haki zetu ndani ya chama hata ikibidi kutugharimu.

  "Tumeteseka chamani, tumelala nje kwa ajili ya chama, tumeshinda njaa, tumehangaikia chama kwa kila hali, lakini malipo yake ni haya…leo haya ndiyo malipo (kufukuzwa).

  "Tumepiga kelele dhidi ya Chatanda kwa ajili ya maslahi ya chama, huyu alikihujumu chama, alikuwa na mgombea wake kwenye kura za maoni, aliposhindwa akasusa kabisa mikutano ya Dk. Burian, hakukanyanga hata mkutano mmoja, baada ya Chadema kushinda alisikika akitoa maneno ya kejeli kwamba ‘alijua'.

  "Mtu huyu hatari kwa chama tunamkataa kwa maslahi ya chama, leo sisi ndiyo tunageuziwa kibao, haya yote ni kwa ajili ya urais mwaka 2015. Wanasema tunamuunga mkono Lowassa, utamuunga mkono vipi mwanachama ambaye hajatangaza kuwa atawania urais?

  "Tunatoa hoja tunatishiwa, chama hiki kinachokataza hisia za wanachama wake ni chama gani? Kitakuwa chama cha aina gani? Ipo siku tutaenda kule watakapotusikiliza," amesema mmoja wa ‘watuhumiwa'.

  Vijana hao wanatoa mapendekezo yao. Mosi, wanashauri Chatanda ahojiwe kwa sababu hata Kamati ya Maadili iliyotumwa Arusha imekataa kumhoji; na pili, hisia za vijana zisitafsiriwe kuwa ni usaliti.

  "Tuhuma tunazoelekeza kwa Chatanda ni za msingi na zenye ushahidi, tunashindwa kuzitolea ushahidi kwenye vikao kwa sababu ya vitisho vya kuuawa au kufukuzwa uanachama. Halmashauri ya Mkoa ni ya watu wenye uwezo na utashi wa kufanya uamuzi wa busara, haitayumbishwa na hisia, watumie busara kusaidia chama ili suala hili libaki ndani ya mkoa.

  "Wana uwezo nalo, wasisaidiwe kufikia uamuzi kwa sababu ya msukumo wa waziri ambaye tunajua ana kazi moja tu-kuwamaliza wote anaodhani ni wafuasi wa Lowassa.

  "Kama ni kufukuza, watafukuza wote, lakini hisia zetu zitabaki kumbukumbu na historia ndani ya chama chetu…kubwa hapa ni kwamba hatuna imani na Chatanda," alisema kijana mwingine.

  Shigella azungumzia Kamati ya Maadili
  Katibu wa UVCCM, Shigella, amezungumzia Kamati ya Madili ya CCM iliyotumwa mkoani Arusha kupata ukweli wa kiini cha mgogoro na kutoa mapendekezo ya kuumaliza.

  Kwanini ilipelekwa Kamati ya Maadili ya CCM badala ya UVCCM? "Tumekubaliana na chama kuwa mgogoro ule si wa UVCCM tu, ni wa UVCCM na Chama. Kwa sababu hiyo tukaona tume na timu ya pamoja inayojumuisha wajumbe kutoka UVCCM na katika Chama.

  "Sisi ndiyo tuliyotoa hadidu za rejea, zimetolewa na Vijana, tumeelekeza masuala ya kuchunguzwa na mapendekezo, kazi inaendelea, mapendekezo tutayafanyia kazi," alisema Shigella.
   
 2. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Hapo kwenye red hapo huyo dogo mwache tu anenge'neke na baba ake akitoka madarakani labda akimbie na asijaribu kugombea hata ubalozi wa nyumba kumi kwa CCM huyo waziri tunamcheki tu sijui anawashwa na nini? ili so soon atachanwa live Vijana Arusha hatutaki vibaraka, tunajua mnatafuta watu wa kuwaweka hasa ktk urais ili mlinde maslahi yenu na kudefend uadui mlioupandikiza. wewe Riz1 wewe ngoja nimeona nimtaje tu huyu ndo anatuvuruga na kuongea na kujisifu saana, afu hajui baadhi ya hao wapambe wake ni mandumilakuwili wanapeleka taarifa zote side. We carrier yako ya siasa mwisho 2014 tutaona ka utaweza survive bila godfather
   
 3. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sijui nina matatizo gani, kila ninapoisoma hoja inayotolewa na gazeti la Mtanzania uwa naishia kuegemea upande wa kinyume na muelekeo wa mwandishi wake, na kuishia kuwa-against na wale wote wanaotetewa na waandishi wa magazeti ya Rostam.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yeah the Main ni kutoka NewHabari nadhani wanamiliki magazeti hayo yote chini ya Rostam it seems Rostam na Lowassa ni pamoja
   
 5. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Tutasikia mengi maana marafiki hawaaminiani tena! Mwisho wa mpambano wao,watajikuta wote wamekosa! Millya na vijana wenzako maadam sasa mmegundua Chatanda ni tatizo CCM Arusha,tunaomba mtusaidie jambo moja... mtueleze ni nani ama akina nani walivuruga taratibu na sheria za serikali za mitaa,wakalazimishia Chatanda kuwa mjumbe wa baraza la madiwani wa manispaa ya Arusha badala ya Korogwe, Tanga.
   
 6. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  yap,hapa ndo wanaweza kuisaidia jamii. Gud pointi!
   
 7. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Ccm taifa inechelewa sana kuchukua hatua kwa mgogoro vijana arusha,sasa tatizo halitibiki tena mpaka uchaguzi 2015,ni hatari kubwa kwa ccm na ni faraja kubwa kwa upinzani!
   
 8. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ccm nyambinyambi
   
 9. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hii
  1.onyo
  2.onyo kali
  3.karipio
  4.karipio kali
  5.kujivua gamba/ kuvuliwa gamba
   
 10. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tepetepe,rojorojo
   
 11. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Nimefurahishwa saana! Jamvini mada zozote,kutoka popote na za chama chochote hudadavuliwa! JF oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Wacheni wafu wazike wafu wenzao.
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hivi bado kuna ccm arusha!?
   
 14. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Endeleeni kukomaza gamba. hata ikibidi kwa juju. lakini mtakiona cha moto safari hii. Tepelepe CCM
   
 15. W

  Wavizangila Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Upuuuzi upuuuzi tu. Unajua ccm iko dodoma pale,iko lumumba. Mikoan na wilayani ni umbea umbea tu.
   
 16. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  teh teh teh 2015 kivumbi nadhani utakua ni uchaguzi wa kihistoria
   
 17. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ccm ikifa ndio furaha kwangu, ccm wakigombana ni jambo la heri na la amani katika muendelezo wa laana zinazowandama, siwahurumii hata kigo, waache wafe, na tutawazika katikakati ya bahari kama Osama .
  [​IMG]
   
 18. s

  siraji Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 13, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni baadhi ya vijana wa Arusha kutumiwa na wanasiasa wenye maslahi binafsi na sio maslahi ya wengi.Mgogoro wa Arusha unasababishwa na mafisadi ambao hawako tayari kufa peke yao.Wito wangu kwa vijana wa CCM Arusha ni kuachana na upuuzi huu wa kutumiwa na wanasiasa ambao zama zao za kisiasa zinaisha.Pia, magazeti mengine yaache kuwa vipaza sauti vya wezi kwa mwendo huu ninaouona ni kwa baadhi ya vyombo vya habari kutumikia sana mfalme(BOSS) badala ya walalahoi.
   
 19. Rocket

  Rocket Senior Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawa vijana wa Arusha wanatumikia mafisadi badala ya kusimamia msingi na maadili chama chao CCM,waondolewe tuu!!!
   
 20. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kauli yako nimeipenda sana kwa mtu ajua siasa za arusha atakubaliana nawe kabisa,
  Me ntawadokezea kidogo tu kwa upeo wangu nilio nao na jinsi nilivyo iona siasa ya mji wa Arusha.

  Chimbuko la haya yote ni kwanza siasa chafu na chuki fitna mizengwe uchu wa madaraka na kubwa kabisa ni ulevi wa madaraka ndani ya CCM kwa muda mrefu na hile hali ya sisi ni wana wa Arusha na kasumba fulani ya ukabila ipo.

  Hoja nyingine ni kuwa kipindi cha uchaguzi wa huu UVCCM waliopo madarakani kuanzia Uchaguzi wa UVCCM wilaya hadi Mkoa ndipo kulipo anzia chimbuko hili pia la kisiasa ndani ya CCM mkoani Arusha kanini nasema hivyo kipindi cha hizo chaguzi za UVCCM wilaya na Mkoa kulikuwa na watu nyuma ya hao viongozi waliopo sasa walifadhili na kupitisha hongo za hawa viongozi waliochaguliwa na ndio wapo sasa na vigogo ndani ya Chama CCM i mean wakubwa walitaka UVCCM iongozwe na watu wao wanao wataka kwao by any means na kweli walifanikiwa sana na wengine hawakufanikiwa na hii yote ilikuwa ni mbio za kuelekea uchaguzi wa 2010 wabunge na madiwani hadi Urais.

  Sasa kwa Arusha kikubwa sana kilikuwa ni Ubunge/Udiwani na ndipo mpasuko mkubwa ulipo shamili kukawa na serious upinzani ndani yao kwa wao wenyewe na kuwekeana chuki kabisa na vitisho na ndipo hapo CCM arusha ikaanza ku perform badly katika jukwaa la siasa na hapo ndipo wengi wao walio tengani waka support CDM hilo liko wazi kabisa na lipo kundi lingine lenyewe liko kimya tuu haliko upande wowote na hawataki kabisa hata kusikika wakiongea na wako ndani ya UVCCM na niviongozi wa juuu katka mabaraza ya UVCCM wilaya na Mkoa kwani hawa wameona alama za nyakati na kuwaachio hao mafaari wawili wa UVCCM wilaya na Mkoa. Tatizo hili liko mpaka huko chini ngazi za shima matawi kata sasa sielewi hiyo kamati iliyokuja ndio itapata suruhisho la mgogoro wa Arusha na siasa za CCM chafu sidhani.

  Kwangu njia nyepese ni kuwa transition of power ndani ya UVCCM ilikuwa ni mbaya sana haikuangali viongozi vijana wajao bali viongozi wazeee waliangali kulinda maslahi yao na kuwaweka watoto zao ndungu na jamaaa ili kulinda interest zao huku wakikiua chama bila yao kujua au kukiua makusudi kabisa kwani hawa wazee au vigogo walisha ona kuna kasi kubwa ya vijana wasomi wanakuja na fikra mpya na itawaweka pabaya na ndipo fitna na siasa chafu kukua Arusha.

  Jingine la kufanya ni kuwa vijana wengi waliondani ya CCM ni kama vile walijisahau sana na kujiendeleza na shughuli zingine wao walitegemea CCM kama chama chao kitawanyanyua kiuchumi matokeo yake ikawa sivyo walisha ndanganywa na pesa za chaguzi mbali mbali kuhongwa vibaisikeli na kudumaaa siku zote na viposho ndicho kimewavuruga vijana wengi ndani ya CCM Arusha i mean NJAAAAA kwa UVCCM ni kubwa na ndio migogoro inapo anzia hapo leo hii nenda kaulize UVCCM arusha wana mradi gani wa kimaendeleo mpya kweli umetekelezwa na Uongozi uliopo wa UVCCM Mkoa hadi wilaya?? non zero ni majungu na fitna tu na hao viongozi wao wa UVCCM kutmiwa na Viongozi wa ngazi za juu CCM yaani aibu sana vijana wamekuwa ni wakutumiwa tu humo ndani ya CCM hii ndio hali halisi. Najisi ya kutatua hilo ni kweli watu wachukuwe jukumu la uwajibikaji kama umekutwa na kashfa chafu achia ngazi tuu basi ndio mtakinusuru chama na sio kunyoooshea vidole
   
Loading...