Kipilipili
JF-Expert Member
- May 25, 2010
- 2,272
- 1,880
Waungwana za jikoni?
Nina rai hapa kuwa tuweke kwa kiswahili na kingereza majina ya viungo vya chakula yaani spices pamoja na ingredients nyingine za kupikia na hata majina ya vyakula vilivyokwisha pikwa ili itusaidie tunapokuwa tunasoma recipe/menu za vyakula za kingereza tujuwe kinachokusudiwa.hii itawasaidia wale wanaosafiri na waliopo nje!
Ni ukweli ulio wazi japo wengi tunaficha kuwa wakati mwingine tunapata tabu kuagiza vyakula ughaibuni au hata nyumbani ikiwa menu ipo kwa kingereza. Sisemi kuwa hatujui kingereza,la hasha ila majina yanatutatiza.
Mfano kuna siku nilikwenda marikiti nkawa nataka kununua pilipili manga(pilipili mtama) na uzile, ila hapa nilipo kingereza si lugha inayotumika na mie sijui uzile na pilipili manga vyaitwaje kwa lugha ya hapa wala kingereza chake.
Nkaenda google translator na kuandika kwa kiswahili ili nipate jina la lugha ya hapa! Duuh ilikuwa majanga matupu lilikuja jina ambalo nlipomuonesha muuzaji akawa pia hajui japo lugha ilikuwa yake.
Hangaika hangaika hatimae nkajuwa pilipili manga kwa kingereza inavyoitwa, kisha nikatumia hilo jina la kingereza kutranslate kwenye lugha ya hapa na hatimae muuzaji akaelewa.huu ni mfano mdogo tu wengi huenda mshakutana na haya!
tutirike basi mfano:
Mdalasini-?
uzile-?
Tangawizi-?
biringanya?-
Kuku alieokwa-?
Chips zege-?(#mimi49 uliwahi kutaja jina lake hebu tukumbushe)
Hiyo ni mifano tu....karibuni wote! #Invisible ukiona inafaa tafadhali hii ifanye iwe sticky note ili isaide wengi