RAI ladai USA na EU zafadhili hoja ya KATIBA MPYA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAI ladai USA na EU zafadhili hoja ya KATIBA MPYA

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Dec 30, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Gazeti la RAI - NGUVU YA HOJA -linalomilikiwa na ROSTAM AZIZ mmoja wa makada wa CCM ambaye jina lake limekuwa likihusishwa na ufisadi mkubwa mkubwa tu hapa nchini limedai kwenye makala yake ya wiki hii iliyotoka leo ya kuwa.......................

  Marekani na Ulaya ndizo zinavuruga nchi na ya kuwa zimemwaga hela kibao kwa ajili ya kufanikisha mradi wa katiba mpya................................

  Lengo hapa ni kuonyesha ya kuwa watanzania hawaihitaji katiba mpya ila ni vibaraka wa ukoloni mambo leo na mabwana zao huko nje ndiyo wanaidai katiba hiyo tajwa..............

  Mbinu hizi hazina hata harafu ya NGUVU YA HOJA bali ni HOJA YA NGUVU tu........ya kutetea mfumo uliopo ambao ndiyo umemnemeesha ROSTAM AZIZ hadi akawa na kiburi cha kukata na shoka cha kufanya atakavyo bila ya taasisi za utawala bora kuwa na ubavu wa kumwaadibisha..............

  Pole sana ROSTAM................Tanzania is bigger and better without your interferences.......................
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Mkuu ....@Ruta.... thanks for your info..... yet we still need this money to finance the whole process towards a new draft constitution.... p'se check my reply on your post regarding Mkutano wa katiba posted earlier.... i had the same concern on funds to be used....
   
 3. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,801
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Mimi nina mtazamo tofauti wenye kuangalia mbali hasa baada ya Katiba mpya ANDIKWA,
  1. kwa kuwa watakaosimamia KATIBA ni walewale si dhani kama yaliyomo kwenye KATIBA yatatekelezwa kwa wenye nazo
  2. kwa kuwa Katiba ya sasa sio mbaya sana ila wasimamizi ndio wabaya ni vizuri kukawa na mstkabali wa kitaifa wa kuweka misingi ya utawala bora na watu waadilifu kusimamia mstkabali huo
  3. kwa kuwa Maadili ya uongozi hayapo tena basi ni vizuri viongozi wetu wakajua kuwa hatupo mbali lazima zitapigwa tu ili kipigo hicho kiwe nguzo ya kujenga utawala bora au la washika dola wakae waambiane hali halisi na ukweli kama wanaitakia mema Nchi hii

  NB tumefika pabaya sasa kila mtu amekata tamaa
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo hao Rai hawaoni umuhimu wa katiba mpya ila vibaraka? Thick brains!
   
 5. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Gari moshi la Kuandika Katiba Mpya limekwisha waha moto-RA, EL, Aa wote hao wako bungeniC , wala NM (pamoja na kwamba wote hao ni wabunge)-hawa ni kura tatu tu-wabunge wa bunge hili watakuwa wasaliti kama hoja hii wabunge wote wa CCM na CUF watapinga hoja hii!!!!!!!!!!!! Mbubge mmoja mmoja atapita lakini JYT iko daima!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Watanzania wenye uchungu na nchi hii wako wengi daima!!!!! Hivyo mwenye hekima ni yule anayeelewa huko tuendako-pipoooooooos pawa-!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hata huyo bwana Gbagbo alijibinafsishia Urais na anapoulizwa na nchi za Magharibi ikiwepo UN na Ufaransa, yeye anaituhumu Ufaransa kuwa pamoja na wazungu wengine wanaingilia siasa za ndani ya waafrika!

  Hii ni ajabu kabisa. Hawa viongozi wa Afrika wanapotaka matakwa yao yatekelezwe wanatumia kila mbinu kuonyesha kuwa anayekinzana nao ni wakala wa ukoloni. Ila wao viongozi pale wanapotaka kupata madaraka, wanapopata sapport ya hao wazungu, huwa hawana kauli yoyote kuwa wazungu wanaingilia siasa za ndani ya nchi zao kuwa-support watawala hao.

  ANGALIZO:
  Siku zote watawala waovu huwa ni waoga sana wanapoona wananchi wao wanaelimika na kuingia ktk vuguvugu la kudai maslahi na haki zao ikiwemo Katiba ambao ndio msingi wa maisha yao kila siku. Watawala wa namna hii ambao ndi tunao sasa Tanzania, ndio hutumia njia nyingi kupindisha mambo na kubadili mada kwa njia yoyote ili watu watoke ktk ukweli na kuanza kupoteza lengo, kuyumbisha attention na hata kuogopesha watu, kuwakatisha tamaa na kuhakikisha wao ndio wanaendelea kutawala na kuwakalia wananchi hata bila ya ridhaa yao.

  Watatumia hata vyombo vya dola, vyombo vya habari nk..

  Hii ni hatari sana na watanzania wanatakiwa tu kuelewa kuwa mapambano sio ya siku moja, na sio ya watu lelemama na pia wanaotaka kubaki madarakani kwa katiba mbovu ni wengi na wana nguvu sana hivyo wananchi wawe imara, waungane na lengo litimie pasipo kuogopa mtu au kundi lolote la watu kama wanaochapisha habari hizi za kubadili hoja kama gazeti hili la kifisadi la RAI, "nguvu ya HOJA-ZILIZOKUFA TAYARI"

  Mungu ibariki Nchi yetu, angamiza nguvu zote za uovu wa watu hawa wanaoogopa watanzania wasipate mwanga!
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mbona ni hao hao wanaofadhili bajeti yetu? kwa nini hilo huwa hatuhoji.
   
 8. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Well said..
   
 9. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kulingana na mpendwa Celina kombani, ni kuwa katiba mpya haiwezekani kwa kuwa hatuna pesa. sasa kama wameamua kutugawia, si ndio wametusaidia? Nini logic ya gazeti hili? I don't get it!
   
 10. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wanakiogopa kivuli chao wenyewe.
  Mungu atujaze ujasiri tuidai katiba mpya kwa amani au kwa shari
   
 11. GWeLa 2003

  GWeLa 2003 Member

  #11
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  me GAZETI LARAI..TANGU SIKU NYINGI NILISHAACHA KULISOMA, HUWA HALIJENGI HOOJA
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wewe Rweyemamu ungeona jinsi gani Wana-CHADEMA na CUF wanavyochangishiana walau hata hela za makaratasi ofisini, wala usingeyaandika hayo maoni.

  Katiba mpya ya Tanzania itaandikwa na sisi wenyewe hapa hapa, kwa elimu zetu za ngumbaru hizi hizi (Bila kuletewa MADALALI HAPO KATI) na FEDHA ZA NCHI YOYOTE HATUZIHITAJI isipokua MAOMBI YA WATANZANIA BARA NA VISIWANI sote kwa madhehebu zetu maomba yatosha.

  Ndugu zangu Waislam, Wahindu kwa Wakristo, DUA NJEMA KWA MWENYEZI MUNGU kamwe haishindwi kitu!!! Sala ziendelee mpaka kieleweke bila vita wala nini hapa. Mdogo Mdogo mpaka tufike.

  MAOMBI YANAONDOA MILIMA ETI!!! MAOMBI KUMKUNJA FISADI KAMA MKEKA JAAMA!!!

  ACHENI MUNGU AITWE MUNGU, MBELE YAKE HAKUNA JESHI WALA UTAJIRI WA MTU: DILI NA SIRI NI SALA YA DHATI KWA PAMOJA
   
 13. n

  nyantella JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tatizo la nchi zetu za Africa zikigundua kautajiri baaasi amani hakuna tunatafuta kasababu tukaanzia hapo. Sasa wa TZ tunaimba wimbo wa katiba mpya na mbaya zaidi kila kundi lina interest tofauti na hakuna dalili kwamba kuna litakubali interest zake zisizingatiwe, CUF wameisha toa rasimu, CDM nafikiri sasa hivi hawalali baada ya CUF kuwapiga bao, CCM bado hawako decided whether wachukue msimamo gani.

  But wapinzani ukisikiliza critically utagundua wana agenda ya kuiondoa CCM madarakani, lakini hawajakubaliana ni jinsi gani wataishi baada ya CCM kuondoka madarakani.

  kwa mantiki hiyo ni vyema tusipuuze maoni ya mtu yeyote hata awe kichaa maana Congo wana madini karibu zote zilizopo kwenye periodic table of elements, lakini hawana amani tangu enzi za Patric Lumumba hadi leo, wazungu wapo wanachota tu wao wamepewa magitaa wanacheza ndombolo, Angola is very rich kwa mafuta, vita imeisha lakini maisha ni magumu usiombe.

  Bongo yamegunduliwa madini yanaitwa Uranium! yako kibao!!! si ya kuisha leo au kesho!! nafikiri kila mtu anajua matumizi ya madini hayo na mahitaji yake ni makubwa sana. Sasa isije ikawa na sisi tumeingia kwenye mtego huo, kuvurugana kupitia Katiba maana koote walishindwa. tukivurugana watachota uranium kama wafanyavyo kwenye nchi nilizotaja hapo juu!

  Tuwe kama Ghana! Ghana wamevumbua Mafuta Meengi sana na uchumi wao sasa upo japo hajaanza kuchimba, simply because wanavumiliana na kuheshimiana!! wakenya waliunganisha vyama vya upinzani wakawa na msimmo mmoja na wakajua wanahitaji aina gani ya katiba, na wameipata.

  Sisi wa-TZ tunataka kila chama na katiba yake, Madhehebu ya dini yana matakwa yake ambayo hayalingani maana Waislam wana mahitaji yao, wakristu pia wanataka yao yawemo so any thinking person can see the wrong direction we are heading to!

  So we have to look around, are we all clean?

  I was just thinking loud. i am out.
   
 14. m

  mzambia JF-Expert Member

  #14
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Jamani hiyo ni janja tu ya hao rai na rostam wake ili tusimshambulie kuhusu dowans na attorney power yake
   
 15. m

  mzambia JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Na tusipokuwa makini tutasahau kabisa hoja ya dowans na kukimbilia hoja ya katiba ambayo kina rai, mtanzania, majira watakuwa wanaenda against your will ili muwe mnabishana afu mwishowe muanze kuwaponda wao kuwa kwa nini wanang'ang'ania katiba haiwezekani huku dowans ishafungwa.
   
 16. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0


  First you are an all out lier. Hakuna kupigana bao au katiba ya kila chama. Ni katiba ya Watanzania pamoja na wewe. Digest your thinking before putting it to the public.
   
 17. M

  MAMA B Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MKIWA MNACHEZA NA CCM AKILI LAZMA IWE INACHEZA MARA MBILI KILA WANAPOSEMA JAMBO ATA KAMA NI LA KHERI UJUE KUNA UJINGA NDANI YAKE...........SAWA KATIBA MPYA MAANA KILA MTU NDIO ANACHOKIONGELEA ATA KAMA HAIJUI ILIYOPITA........NAYATAFAKARI MANENO YA JK KWENYE HOTUBA YAKE YA KUFUNGA MWAKA AMBAYO IMECHAGUA ISSUES BURNING ZA KUONGELEA NA KUACHA ZILE ZINAZOPIGIWA KELELE KILA SIKU.....MFANO YA DOWANS HAJAONGELEA CHOCHOTE KWA SABABU MJADALA KWENYE MAGAZETI KESHO YAKE UNGEMRUDIA MWENYEWE..........LAKINI KWANN AMEONGELEA KUANDAA MCHAKATO WA KATIBA MPYA?NI KWELE ANACHUKIZWA NAYO ILIYOMUWEKA MADARAKANI AU NI SHINIKIZO?NI KWELI ATAIBADILI TENA KWA HARAKA KAMA TUNAVYOTAKA KWA MWAKA 2015 AU NI KUMLAMBISHA MTOTO PIPI?NAANZA KUONA DALILI ZA KUITUMIA KATIBA HII KWA MWAKA 2015 KWA MAANA NAWAJUA KWA UCHAKACHUAJI WA HOJA ......CCM WANAUZOEFU NA KUUNDA TUME NA ZENYE MAPENDEKEZO MAZURI NA KUUNDA NYINGINE ITAKAYOANGALIA MAPENDEKEZO YA MWANZO MPAKA VIJUKUU VITAAMBIWA VIANDAE TUME TENA YA KUANGALIA TUTAKAYOYAPENDEKEZA.........

  HAPA NAJARIBU KUSEMA MMESHALAMBISHWA PIPI NA IVYO MTANYAMAZA KAMA MIEZI 6 NA KURUKIA KITU KINGINE KABLA HAMJAANZA KULIA TENA MAANA MTAONA KIMYA............

  KAMA TUNAHITAJI KWELI MABADILIKO YA UKWELI NI LAZMA TUJUA KUBANANA NA MUDA.....KILA SIKU INAPOPITA KILIO KIWE KIKUMBWA NA TUSINYAMAZE KAMWE ATA KAMA NI KWA UTAMU WA PIPI:teeth:
   
Loading...