Mh. Magufuli karibu tena kwenye wizara ambayo uliimudu vizuri wakati wa mzee Ben Mkapa. Hata hivyo matarajio yetu ni kwamba utayapa uzito unaostahili yatuatayo:
MATUTA BARABARA KUU:
Mh. Magufuli, Tanzania, inawezekana, ndio nchi peke ambayo imeweka matuta kwenye barabara kuu bila mpangilio maalum wala alama za barabarani. Nimatarajio yetu matuta haya yataondolewa sambamba na kutoa elimu kwa madereva na wadau wengine wa barabara.
Mh. Magufuli, matuta hayo yamekuwa yakisababisha aidha foleni zisizo za msingi ama hasara kwa wamiliki wa magari. Tunajua matuta hayo pia yamekuwa yakisababisha barabara kuchakaa kabla ya muda wake, hivyo kutuongezea mzigo wananchi wa kuzikarafati tena kabla ya muda wake uliopangwa. Tuondolee kero hii.
ALAMA ZA BARABARANI
Mh. Magufuli, nchi nyingi sana zimejaribu kuondoa ama kupunguza ajali za barabarani kwa kuweka alama zinazoonekana wazi kabisa. Barabara zetu nyingi hazina alama hizo. Matokeo yake imekuwa chanzo cha rushwa kwa wanausalama barabarani, pindi wanapokamata madereva. Mfano Kariokoo barabarani nyingi hazina hizo alama na hapa ndio karibu na ofisi kuu za nchi. Nafahamu kuwa barabara zile zinaweza zisiwe chini ya TANROADS moja kwa moja ila bado wewe ndio waziri wake.
Mh. Magufuli, kutokana na hili, la kutokuwa na alama za barabarani, hasara tunayopata wananchi kama walipa kodi ni kubwa sana. Maana kuna magari mazito yanapita kwenye barabara ambazo hawaruhusiwi. Pia watoto na watu wengine wamekuwa wakivuka barabara bila kuzingatia utaratibu wowote. Nimatarajio yetu pia, utaweka usimamizi mzuri wa kuhakikisha kwamba alama zinakuwepo lakini pia elimu kwa wananchi na wadau wengine wa barabara namna ya kutumia barabara na kutoa taarifa iwapo wataona uvunjifu wa unatokea.
Mh. Magufuli sanjali na hili, hebu fikirieni kuongeza taa za barabarani za kuongozea magari kwenye miji kama Dar, Arusha, Dodoma na Mwanza. Maana hatufurahii hata kidogo tabia ambayo inaanza kuzoeleka ya kutumia maofisa wa usalama barabarani kuongoza magari wakati wote. Hawa ni binadamu pia. Wanakaa muda mrefu tena nyakati za jua kali na mvua. Tuondolee kero hii.
BARABARA ZA KISASA:
Mh. Magufuli, haitakuwa na maana yoyote kwa serikali kujenga barabara za juu kwa juu iwapo za chini zenyewe hazina viwango vya kimataifa. Hebu fikiria barabara zote za mijini zimegwa bila kuzigatia wadau wengine. Mfano, sehemu za watembea kwa miguu, walemavu, vivuko vya watoto na wanafunzi. Pendekezo letu ni kuwa madalaya kujenga barabara za juu kwa juu, ni bora pesa hizo zikatumika kupanua barabara zilizopo za mijini na hasa kwa Dar, Arusha na Mwanza. Inatushangaza sana kwamba kuona kwamba Tanzania hatuna barabara ya njia tatu au nne. Barabara za namna hii zingesaidia sana kupunguza foleni na gharama zingine kwa walipa kodi wanazoingia. Si hivyo tu, ufinyu wa barabara za kisasa unarudisha maendeleo yetu nyuma. Wakati barabara ya Mandela unakarafatiwa upya yalikuwa ni matarajio yetu ingeongezwa ukubwa na kuwa njia tatu kwa tatu kila upande.
Mh. Magufuli, tunahakika ukiweka mpangilio mzuri wa kujenga barabara za miji taja hapo juu, foleni itakuwa historia kwa miji hiyo. Lakini pia utumiaji wa barabara zilipo katikati ya jiji la Dar zinapaswa kubadilishwa na kuwa one way. Hii itasaidia magari kuwa na muelekeo moja lakini kupunguza ajali na foleni. Punguza magari kuegeshwa kila upande wa barabara matokeo yake hakuna sehemu za watembea kwa miguu. Ni matumaini yetu kwamba utalifanyia kazi hili.
MIZANI
Mh. Magufuli, mizani ni mingi sana na hatuna hakika kama inaleta tija tarajiwa ama ndio chanzo kingine kwa urasimu na rushwa. Tunapendekeza ipunguzwe. Haina maana yoyote ya kuwa na mzani kila mkoa kwenye barabara kuu. Tuondolee kero hii.
BIASHARA KANDO YA BARABARA NA UCHAFUZI WA MAZINGIRA
Mh. Magufuli, biashara hizi ndogo ndogo ambazo zimo ndani ya hifadhi ya barabara kuu ni tatizo linguine. Kwanza, zinafanyika karibu sana na barabara kiasi kwamba ni hatari kwa wafanyabiashara wenyewe na wadau wengine. Pili, biashara hizi zimekuwa chanzo pia cha uchafu pembezoni mwa barabara hizi kuu. Anzia Dar kwenda Arusha au Dar kwenda Dodoma kwenda Iringa na Mbeya; uchafu kila mahali. Barabara ya Dodoma kwenda Singida ndio pekee, ni kwa sababu ni mpya, ambayo haijaadhirika na uchafu. Kukosekana kwa juhudi za makusudi za kuzuia ufanyaji holela wa biashara ndogo ndogo pembezoni mwa barabara hizi kuu, kutaishababishia hasara kubwa nchi hii na hasa walipa kodi. Kwa kushirikiana na wizara husika ni wakati muafaka kwa biashara hizi zikafanyika mbali na barabara kuu ilikuondokana na kero hizo tajwa hapo juu. Tunafahamu baadhi watalalamika, ila haitakuwa na maana yoyote kuendelea kufanya mambo hovyo hovyo kwa kisingizio cha kutafuta riziki. Kwetu uchafuzi huu wa mazingira ndio mbaya kuliko kitu chochote. Ni matarajio yetu kwamba hili pia utaliangalia kwa jicho kuu.
MADEREVA WATUKUTU
Mh. Magufuli, kwa kushirikia na ofisi husika za serikali wamulikeni madereva watukutu. Maana bado wanatumia barabara zetu ambazo wewe ndiye mwenye zamana wa kuhakikisha zinatumika ipasanyo. Hatukubaliana na tabia ambayo imeanza kuzoeleka ya kwamba kila barabara mpya na nzuri inapojengwa basi na ajali zinaongezeka.
Mh Magufuli, madereva hao ni wale ambao hawajui sheria za barabarani, na hata wanaozifahamu hawazizingatii kwa maana wanaona wenzao wanaozivunja hawachukuliwi hatua zozote za kisheria. Madereva hawa ndio chanzo kikubwa kwa ajali nyingi. Pamoja na kwamba serikali imeanza zoezi la kutoa leseni za udereva mpya, sijaona ni namna gani itakabiriana na madereva hao. Maana wanausalama hawajapewa vifaa vya kusaidia kudhibiti madereva watukutu.
Mh. Magufuli, nimatumaini yetu kwamba utayapa uzito unaositahili haya pamoja na yale uliyona kwenye agenda zako. Mungu ibariki Tanzania