Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,458
- 29,151
Hivi karibuni katika mahakama ya juu mkoani kagera iliamuliwa mwalimu alieua kwa kuchapa bakora anyongwe mpaka afe, adhabu hii naiona ni kubwa sana na itafanya morali ya ufundishaji kwa walimu kushuka.
CWT kimtetee katika basis ya kwamba mwalimu alikuwa kazini hivyo alitoa adhabu kama mwalimu na sio mhalifu.
Anapohukumiwa kunyongwa sawa na mtu ambae ameua kwa ujambazi ni uonevu na pia huyo mtoto hakuwa na cheti cha ugonjwa kwamba asichapwe. Na suala la kusema kuwa hakuiba pochi hilo lilikuja baadae baada ya kijana kuchapwa.
Kwa hali hii sisi tuliosoma shule za Makongo na Jitegemee enzi hizo tena tunapigwa na wanajeshi bakora mpaka unashindwa kukaa basi wangefungwa sana. Mtu anaweza kufa hata kwa kupewa adhabu ya magoti tu pale mbele ya darasa je mwalimu pia anyongwe? Tusifanye kazi ya ualimu ikawa adhabu.
GENTAMYCINE amesema sasa ndio wanafunzi watavutia bangi darasani na kufanya mapenzi ofisini kwa head teacher maana kila mtu anaogopa kunyongwa. Tafadhali hukumu ya mwalimu yule ifanyiwe rejeleo.
Sent using Jamii Forums mobile app