RAI: CCM yaijibu CHADEMA; Nape amtahadharisha Freeman Mbowe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAI: CCM yaijibu CHADEMA; Nape amtahadharisha Freeman Mbowe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 7, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h] Jumatatu, Mei 07, 2012 05:00 Na Gabriel Mushi, Dar es Salaam
  [​IMG]Nape Nnauye

  * Yakana taarifa za wabunge wake kuhama
  * Nape amtahadharisha Freeman Mbowe

  KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, ameibuka na kukana taarifa zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kwamba kuna wabunge 70 wa CCM wanataka kuhamia Chadema.

  Aidha, amemtaka Mbowe kuwa makini kutokana na nyadhifa alizonazo ndani ya chama hicho cha upinzani.

  Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Nape alisema amesikitishwa na kauli ya Mbowe kwa kuwa ameitoa bila kufanya utafiti.

  “Mbowe anatakiwa kumwachia Dk. Slaa (Katibu Mkuu wa Chadema), azungumze masuala hayo ya kisiasa kwa ajili ya kuleta picha nzuri ndani ya jamii.

  “Mbowe asisahau kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, pia ni kiongozi mkubwa wa chama hicho, asizungumze masuala kama hayo yasiyokuwa na tija mbele ya jamii.

  “Anachokisema Mbowe ni sawa na mtu ambaye anapigana halafu anapigwa huku akipiga kelele kwamba, njooni mnitoe nitamuua huyu wakati yeye ndiye anayepigwa. Au ni sawa na mtu anayetaka kujiua halafu anakuja kuniambia kuwa sasa nataka kujiua, huyu anataka nikamwokoe hana maana yoyote.

  “Kwa hiyo, kauli ya Mbowe imenisikitisha sana kwa sababu naona kama amekurupuka, kwa hiyo, ninachotaka kumshauri ni kwamba, ajiheshimu kwa kauli zake, kulingana na nafasi zake za kiungozi alizonazo katika chama na jamii kwa ujumla,” alisema Nape.

  Juzi, Mbowe alipokuwa jijini Arusha alihutubia mkutano wa hadhara na kusema miongoni mwa walioomba kujiunga na CHADEMA ni mawaziri walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.

  Akiwahutubia wananchi na makada wa chama hicho waliofika katika mkutano wa uzinduzi wa Operesheni Vua Gamba, Vaa Gwanda, uliofanyika mkoani Arusha, Mbowe alisema kuna wimbi kubwa la wanachama watakaohamia CHADEMA.

  Akinukuliwa na vyombo vya habari, Mbowe alisema “Kwanza namtahadharisha Rais Kikwete katika Baraza la Mawaziri alilolitangaza jana.

  “Wapo mawaziri tisa ambao wameniomba nafasi CHADEMA, kwa nyie mlioingia leo karibuni CHADEMA, huku hakuna rushwa wala ufisadi, unapiga gwanda, unapiga kazi tu.

  “Wana CHADEMA msiwe na hofu na wale wanaojiunga na chama kutokea CCM, kwa kuwa kuna wengi walitoka huko na ni wapigania haki wazuri. Kwa mfano, Katibu Mkuu, Dk. Willbrod Slaa, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje na Makamu Mwenyekiti wetu, Said Amour Arfi, ambaye alikuwa TLP kabla ya kujiunga CHADEMA,” alisema Mbowe.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini Nape Nnauye anakana? Yeye alipokuwa anampango wa kuhama CCM; nani alimpingia? CCM iache kuwalinda wanachama wake kama wakati wa Ucomunist; it is free now they can choose where to go; what party to Join.

  Nape, hajui Mawazo ya binadamu yoyote...
   
 3. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,925
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  nadhan mbowe alijisahau
  alidhan yupo pale ikulu kwake bilicanas
   
 4. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nape hajapona tu dege dege tumfukize na mavi ya tembo wa Maige
   
 5. O

  One Man Army JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  RIP ccm
   
 6. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,925
  Likes Received: 1,853
  Trophy Points: 280
  hahahaahaa...!
  Piiiiiiiiipoooooooz....!
   
 7. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,676
  Trophy Points: 280
  Kwa staili hii ya Nape aliyotumia kanusha, kunauwezekano mkubwa maneno ya Mh. Mbowe yakawa sahihi.
   
 8. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Nape hajui kama CCM yake ina matobo kama vyandaraua vya ''kwa msaada wa watu wa Marekani''

  Inawezekana hata JK anataka kuhamia kwenye M4C ila nape hajui
   
 9. D

  Deofm JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi naamini wengi wanasubiri tu posho, hata hivyo naamini kuna watakaohama kabla ya kumbaliza msimu kama alivyofanya mpendazoe. Litakapotokea naomba Nape uwe tayari kufuta usemi wako, kwani unawasemea watu ambao wana fikra tofauti na wewe, kuna waliotarajia uwaziri wameukosa sasa wana kinyongo ile mbaya.
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yeye ni Mbunge wa Vitu Maalum akihama kuhamia Chadema nani atampa Ulaji kama anaoupata kama Mbunge?

  Wabunge wengi wezi tu hawawezi kuachia hivyo vyeo, anasema kinamuuma nadhani alitaka pia Uwaziri na hiyo Ph.D
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ukiona nape kajibu hoja za cdm ujue hapo message well delivered
   
Loading...