Raha ya tendo la ndoa ni uthibitisho kuwa maneno ya kwenye Biblia yana ukweli na kwamba yametoka kwa Mungu/Nature

umewaza parefu sana mkuu,kwangu mimi hii ni the best thread of the day.tunaweza kupinga uwepo wa Mungu kwa nguvu zote lakini kwenye hoja kama hii ujanja wote kwisha,kusema ukweli ni lazima kunaye creator mwenye uwezo wa ajabu aliyeweza kubuni na kubalance haya mambo.
Asante sana mkuu!!
 
Na raha hio iko kwa pande zote mbili mwanamke na mwanaume.Kusema kweli ni moja ya burudani haswa.Halafu dunia imejaa wanawake wazuri.Mtoto wakike katengenezwa kiumaridadi kila mwanaume ana type yake anayoitamani.Hakika mahali nilipomuona Mungu ni mkubwa ni namna alivyomtengeneza mwanamke...Mwanamke kawekwa vizuri mlaini,,anaringa,,staki nataka,,anapenda kweli kweli.
Nyumba bila mwanamke inakuwa chafu,,kimya,,hakuna wa kupika mapokopoko na mahanjumati...kitandani ndio anatukomesha Kabisa....Ama kwa hakika mwanamke sifa zake ni nyingi...Na Mungu ana maksi za kutosha kwa huyu kiumbe ambae dunia imeharibu uzuri wake.
👊👊👊👊
 
kuna haya maneno katika kitabu cha Mwanzo yanayosomeka hivi:

Mwanzo 1:28 BHN
Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.”

Hapa ndipo mtu unapopaswa kujiuliza ni kwanini tendo la ndoo/kujamiiana linaambatana na starehe/burudani kwa viumbe karibu wote?

Kwa upande wangu,naweza kusema lengo la kuwepo burudani katika hili tendo ni ili kutekeleza agizo hili la Mungu/Nature na si vinginevyo kwani bila uwepo wa raha ya tendo la kujamiiaana,huenda kuzaliana kusingekuwepo kwa kiwango cha kuijaza dunia hasa kwa wanyama ambao sidhani kama hata wangezaliana kabisa na hapa ndipo unaona maneno haya ya kwenye Biblia yanapata ushahidi kwani alieumba viumbe hai hawa ndio pia alieumba/kutengeneza raha ya tendo la kujaamiiana.

Picha nyingine ninayoipata ni kuwa moja ya makusudio makubwa ya Mungu/Nature ni kuona huu ulimwengu unakuwa na viumbe hai wakati wote na ili hili litimie,ndio maana akaweka burudani ya tendo la kujamiiana burudani ambayo viumbe hai hawawezi kuiepuka.

Labda jiulize hali ingekuwaje au nini kingetokea,hasa kwa wanyama,kama tendo hili la kujamiana lisingekuwa na raha/burudani ndani yake.

Jibu rahisi hapa ni kuwa moja ya priorities kubwa za muumba/nature ni kuhakikisha hii dunia kamwe haiwi na ombwe la viumbe hai ila ni kwasababu gani,hili nalo ni swali la kujiuliza.

Sijui wewe mwenzangu mpaka hapa unaonaje.
Mimi huwa najiuliza ilikuwaje (hapo mwanzo) mnyama au binadamu akatambua kwamba hiyo raha inapatikana kwa kuingiza male sexual organ into female sexual organ, tena lazima kuwepo to and from motion? Yaani walijuaje kwamba hii inaingizwa pale? Acha Mungu aitwe Mungu!
 
Back
Top Bottom