Ifahamu Biashara ya supu ya pweza

kokosai

Member
Dec 25, 2018
49
19
1603631768972.png


Mchanganuo wa biashara ya supu ya pweza
Pweza ni mazao ya bahari ya Hindi. Samaki wa aina tofauti, pweza, ngisi, dagaa kamba na kadhalika ni baadhi ya vinavyopendwa na wakazi wengi.

Biashara hii ni rahisi kuifanya kwani haihitaji mtaji mkubwa wala ofisi na pia hivyo vyakula huuzwa kwa gharama ndogo ambayo kila mtu anaweza kuimudu.

Biashara hii mara nyingi hufanyika muda wa jioni kandokando ya barabara na kwenye vituo vya mabasi ambapo watembea kwa miguu na abiria wengi hupita wakirejea makwao

Biashara ya supu inaonekana kuwa ni biashara ya kawaida sana miongoni mwa biashara zinazofanyika katika mitaa yetu kila siku hasa hasa mijini lakini biashara hii siri yake kubwa ni kwamba haihitaji uwekezaji wa mtaji mkubwa sana kusudi mtu aweze kuanza, siri nyingine kubwa katika biashara hii ni kwamba supu safi, halali na nzuri hupendwa sana na watu wa kada mbalimbali, haijalishi mtu ni wa dini gani au kabila, karibu kila mtu anapenda supu hasahasa nyakati za jioni.


Ni biashara endelevu kwani mtu anapokunywa supu leo na kukuta ina ladha nzuri ya kupendeza na kesho yake atakuja tena na tena na hivyo kukupa faida endelevu. Siri kubwa ya kuvuta wateja kwenye biashara ya supu ya pweza ni USAFI katika vyombo, eneo lenyewe la biashara na mhusika anayewahudumia wateja.

Mtaji wa biashara ya kuuza supu ya pweza.

1) Eneo au mahali pa kuuzia supu ya pweza na meza ya kuwekea pweza wako.

2) Vifaa kama vile jiko, sufuria, sahani, bakuli, kisu na vijiko.

3) Pweza na viungo vyake kama pilipili, ndimu, tangawizi, nk.

Ukitazama vitu hivi vikuu vitatu ambavyo ndiyo mahitaji yetu makubwa kwa ajili ya kufungua biashara ya kuuza supu ya pweza ni mahitaji ambayo bila shaka yeyote kama mtu utaamua kikamilifu hayawezi kukushinda. Ni kweli kabisa hata mimi nafahamu kuanzisha biashara yeyote ile hata ikiwa mtaji ni mdogo kiasi gani lakini kama hauna pesa yeyote mfukoni hata ungeambiwa zinahitajika shilingi elfu tano tu, inakuwa ngumu.

Eneo.
Eneo kwa ajili ya kuuzia supu, halina usumbufu mkubwa sana kupatikana kutokana na biashara yenyewe kuwa ni ya muda mchache maalumu. Supu inaweza ikauzwa kwa wastani wa masaa mawili mpaka matatu tangu kuiva hivyo eneo litakalotumika linaweza likawa siyo la kudumu kama vile barazani, stendi ya magari, mbele ya duka baada ya kufunga nk. Hivyo unaweza kuona ni kwa namna gani biashara hii inaweza ikawa na urahisi katika sula zima la eneo la kuuzia.

Vifaa mbalimbali.

Sufuria kubwa la kuchemshia supu ya pweza, jiko la mkaa au kuni, kisu, bakuli kadhaa na sahani zake, vijiko, meza pamoja na viti au benchi ndiyo vifaa muhimu zaidi vitakavyohitajika. Hapa kidogo panaweza pakawa na gharama lakini itategemea, wakati mwingine mtu unaweza hata kuazima vyombo vyako mwenyewe kutoka nyumbani ukavitumia mpaka pale mambo yatakapokuwa “super” basi ukanunua vya biashara.

Pweza na viungo vyake.

Pweza na ngisi, hawa hupatika baharini, unawahi wakati wavuvi wametoka kuvua hivyo unapata kwa bei nafuu ili uweze kupata faida kubwa zaidi.

Viungo
Viungo mbalimbali vinavyoambatana na supu itategemea na mtayarishaji mwenyewe ataamua kuweka viungo gani. Wengine huweka tangawizi na vitunguu, wengine karoti, pilipili hoho, kuna wengine pia hawaweki chochote zaidi ya chumvi na mteja hujiwekea mwenyewe kwenye bakuli viungo vingine kama vile ndimu na pilipili.

Mtaji wa kununulia vitu hivi siyo mkubwa sana ukilinganisha na ununuzi wa bidhaa au malighafi katika biashara nyingine, na uzuri wake ni kwamba biashara ya supu ni biashara inayofanyika na kuisha siku moja hiyohiyo, unafahamu umepata fedha kiasi gani, unatenga kabisa pesa kwa ajili ya kwenda kununulia malighafi kwa ajili ya siku inayofuata na faida pembeni. Hata kama unakopa mtaji wa mtu kwa maana ya fedha taslimu au vifaa, inakuwa rahisi sana jioni kumrudishia fedha zake zote ukabaki na faida yako mkononi.


Kwa kawaida supu ya pweza huendana na vitafunwa hasa kachori, Vitafunwa hivi kama huwezi kuviandaa mwenyewe unaweza ukamtafuta mtu atakayehakikisha kila siku vinapatikana na katika ubora wa hali ya juu.

Pilipili na chumvi pamoja na vitunguu
Pembeni utakuta wanaweka pilipili iliyoungwa vizuri na wakati mwingine kachori au kababu Ukitaka upate wateja wengi na wa uhakika kila siku kuwa mbunifu katika suala la usafi kwani watu wengi supu hii wanaipenda sana lakini huogopa mazingira ya uchafu na kushea vyombo.


Wadau wanaotaka kufahamu kuhusu biashara ya Supu ya pweza
Manahoza wa jf nataka nianze biashara ya kuuza pweza morogoro mjini so mwny kujua changamoto zake anifahamishe??
----
Habari zenu kama kichwa cha habari kinavosema naomba mnisaidie natamani sana kufanya hii biashara, Ila sielewi ni mtaji kiasi gani utatosha na pia ni vitu gani niweke ili biashara iwe nzuri
----
Habari JF,

Leo nimekutana na dogo mmoja nikaanza kupiga naye stori anitafutie mfanyakazi wa kutembeza biashara.Ila katika mazungumzo ya biashara ambayo niliplan dogo akanikatisha tamaa akanishauri nifungue biashara ya kuuza supu ya pweza na pweza akaanza kunipa na darasa la kunishawishi, ila mimi naona kama anataka aniingize cha kike vile?

Hebu wataalamu wa hizi biashara za pweza na supu ya pweza hebu kaeni humu mara moja mtupe uzoefu wenu maana nasikia watu wanapiga sana supu mjini hapa.

Maoni ya Mdau juu ya biashara ya pweza
naomba nijibu kadri mungu atakavyonijalia......mtaji ukitoa meza,jiko, karai, sahani ,vikombe , na vifaa vingine,basi mtaji ni mdogo tu, pweza wanauzwa kwa kilo ,kilo moja haizid buku kumi,inategemea na siku hiyo, so inategemea na kilo unayoitaka, kachori mtaji wake hauzid 10000, hapo toa mafuta na mkaa. kuhusu pilipili,kule kule zinauzwa uliza pilipili ya pweza,kuna babu anauza hiyo pilipili,na ndio maana unakuta maeneo mengi pilipili zinafanana kwa utamu. location nzuri has a ni sokoni au stend ya basi au kwenye mkusanyiko wa watu wengi. kuhusu mchuzi,unaponunua pweza kule feri,vuka upande wa pili wakati unatoka nje,utaona kunasehemu wanachemsha na kukaanga hao pweza,so wanachemsha kwanza kisha unapata mchuzi unaweka kwenye kidumu chako,kisha unamkaanga kwa gharama ndogo tu........pia kuna wengine wanaweka na samaki hapo hapo kwenye meza so integemea na maamuzi yako........NB sijawahi kufanya hii baishara ila nilitaka kufanya ,hivyo nikafanya research kwanza kujua ABC zake.,......... ila kwa wenyewe wanasema inafaidaa, so Mimi hii biashara niaifahamu kwenye makaratasi,so ukichukua ushauli wangu,usije kunihumu huko baadaye..........tuendelee kuombea ndege yetu waiyachieeeee.
 
Mkuu hivi test yake ikoje? Unajua nikiwa Dar huwa naona mtu anakuwa thermos na vipande vilivyokatwa katwa mezani. Hivi wateja wanapokuwa wanakula vipande muuzaji huwa anahesabu ili wasimuibie?
Mkuu huwa hana muda wa kuhesabu bali huwa wanaaminiana tu.
Mara nyingi wanaokula huwa ni watu wa pwani ambao wengi wao ni waislam.
Ila ingekuwa wateja wake ni watu wa kaskazini wangemliza
 
Mkuu huwa hana muda wa kuhesabu bali huwa wanaaminiana tu.
Mara nyingi wanaokula huwa ni watu wa pwani ambao wengi wao ni waislam.
Ila ingekuwa wateja wake ni watu wa kaskazini wangemliza


Kwahiyo sisi ni watu hatari sana kwenye biashara za watu?
 
Back
Top Bottom