Raha na furaha ya kupata mtoto wa kiume imepotea kwenye familia kabisa

kamituga

JF-Expert Member
May 31, 2019
1,195
1,919
Wakuu habar za jion!!!!!
poleni na pilika pilika za hapa na pale ktk kutafuta chochote ili siku zijisukume.

Pasipo kuchelewa nielekee kwenye mada maisha yamebadilika kabisa zile furaha shangwe na vifijo vilivyo kuwepo awali pale inapotokea mwanamke akajifungua mtoto wa kiume imegeuka simanzi kubwa kwa familia. Hata yale majina tuliyokuwa tunawaita watoto wetu mfano (jembe langu, kamanda wangu) tukiwa na imani kuwa amepatikana mlinzi wa familia na amani nyumbani pale tu umri utakapo kuwa umetutupa mkono hiyo furaha imegeuka simanzi baada ya shetani kuingia kazini.

Usodoma umepamba moto kila mzazi anahofu na mtoto wa kiume tofauti na zamani bora binti abebe mimba nyumbani mara kumi kuliko hii ya sasa ya vijana wa kiume mambo yamebadilika siku hizi security inawekwa kwa watoto wa kiume na sio mabinti tena WAZAZI WENZANGU TUMUOMBE MUNGU HII BALAA IPITE MBALI NA UZAO WETU.
 
Mbona bado Raha IPO Sana ya kupata mtoto wa kiume?

Shida wakizaliwa wanakuwa na urafiki Sana na mama zao kupindukia .

Mtoto wa kiume inabidi uwe na urafiki wa karibu na Baba na ikiwezakana mtengenezee mazingira ya kiume kiume.

Mtoto wa kiume anabidi ajue Mambo yafuatayo kabla ya miaka kumi na tano.

1.Ajue kazi zote za kiume nyumbani .mfano kufunga Milango( security),kushika panga,kama kuna mifugo asimamie yeye,kushika nyundo,mizigo ikiletwa nyumbani abebe yeye,nk nk yaani kimsingi mpeni kazi za kiume.Yaan Baba ukifika nyumbani muulize muulize yeye kama kila kitu kiko Sawa.
2.ajipeleke mwenyewe kama shule sio kila mara na mama yake ,saa nyingine muandikie vitu kwenye karatasi akaemee,nk

3.baba akae Sana na mtoto wa kiume msome Tabia zake na ukiona anafanya kazi za kike kike mkataze haraka.

Naamini kufikia miaka ushirini mutakuwa na mwanaume nyumbani
 
Mbona hili suala linakuzwa sana? Yaani ushoga upo tangia enzi za mababu na mabibi, na propotion yake kwenye population sidhani hata kama inafika 1%
Sasa huu upumbavu wa ushoga, ushoga, ushoga imekuwa too much sasa, au nyie ndio mashoga wenyewe?

Nimesoma sekondari, sijawahi kuona shoga hata mmoja shuleni, wala mwenye dalili hizo, mtaani ninapoishi sasa hivi, sijaona shoga hata mmoja.
Juzi ndio jamaa alikuwa aki share picha ya shoga kamtoa Instagram kwenye group la Whatsapp akidai sijui Dunia imekwisha blah blah, nikauliza wewe unatafuta picha za mashoga mtandaoni kisha unalalamika? Unawa follow mashoga mwenyewe kisha unalalamika? Wewe pia shoga unatupima upepo?

Tangia kuzaliwa kwangu hadi leo nimekutana na mashoga wawili tu, na sioni kama ni tatizo, maana nakutana na mamilioni ya watu ila wawili tu ndio walikuwa mashoga, sasa Dunia imeisha kivip?

Nyie mnaolilia ushoga kila mara huwa mnawaonea wapi?
 
Mbona bado Raha IPO Sana ya kupata mtoto wa kiume?

Shida wakizaliwa wanakuwa na urafiki Sana na mama zao kupindukia .

Mtoto wa kiume inabidi uwe na urafiki wa karibu na Baba na ikiwezakana mtengenezee mazingira ya kiume kiume.

Mtoto wa kiume anabidi ajue Mambo yafuatayo kabla ya miaka kumi na tano.

1.Ajue kazi zote za kiume nyumbani .mfano kufunga Milango( security),kushika panga,kama kuna mifugo asimamie yeye,kushika nyundo,mizigo ikiletwa nyumbani abebe yeye,nk nk yaani kimsingi mpeni kazi za kiume.Yaan Baba ukifika nyumbani muulize muulize yeye kama kila kitu kiko Sawa.
2.ajipeleke mwenyewe kama shule sio kila mara na mama yake ,saa nyingine muandikie vitu kwenye karatasi akaemee,nk

3.baba akae Sana na mtoto wa kiume msome Tabia zake na ukiona anafanya kazi za kike kike mkataze haraka.

Naamini kufikia miaka ushirini mutakuwa na mwanaume nyumbani
Jirani yangu hapa nyumba ya pili, kijana wake very handsome hakuchaguliwa form V credits hazikutosha. Alimtafutia chuo VETA ajifunze mechanics mtoto amekataa wakati dingi amelipa ada tayari.

Yule kijana ametafuta chuo cha unesi, juzi usiku tunatoka party ninamuona amevaa blouse ya kike kabisa. Ni girl friend wa mtu kabisa.
 
Back
Top Bottom