Rage pesa za okwiiiiiiii zimeenda wapi.....?hiki ndicho cha kujiuliza wana simba

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Arnold Okwi ambaye alikua akiichezea klabu ya SC Villa ya Uganda.

Yanga SC imempata mshambuliaji huyo msumbufu kwa mabeki wengi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ambapo kwa sasa ataitumika klabu yake mpya ya watoto wa jangwani mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.

Dirisha dogo la usajili nchini Tanzania limefungwa leo usiku wa Disemba 15, 2013 saa 6 usiku ambapo mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga wamekalilisha taratibu zote za usajili ikiwa ni pamoja na kupata hati ya uhamisho wa kimataifa maarufu kama ITC.

Usajili wa Emmanuel Okwi unaifanya timu ya Yanga kufikisha idadi ya wachezaji watano wa kimataifa wakiwemo mganda mwenzake Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu.

Uongozi wa Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki kuwapa ushirikiano wachezaji wote wa zamani na wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili.

Wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika kuimarisha kikosi cha Yanga ni mlinda mlango Juma Kaseja ambaye alikuwa mchezaji huru na Hassan Dilunga aliyesajiliwa kutoka timu ya Ruvu Shooting.

Baraka Kizuguto
 
Hata kama mnampango wa kumfukuza wekeni mpango wa kumweka ndani kuhusu hili swala lazima watu wajue cheo sio sehemu ya kumaliza matatizo yao ..
 
Okwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 

Attachments

  • OKWIIIIIII.jpg
    OKWIIIIIII.jpg
    32.2 KB · Views: 144
Hata kama mnampango wa kumfukuza wekeni mpango wa kumweka ndani kuhusu hili swala lazima watu wajue cheo sio sehemu ya kumaliza matatizo yao ..

Huyu jamaa kubamiza kaanza zamani, aliwabamiza Yanga, kawabamiza kwa Twite na muda haujapita kawabamiza tena kwa Okwi. Inabidi Simba waue mtu hapo kesho.
 
Ni wachezaji watatu tu wa kimataifa wataruhusiwa kwenye ligi ijayo. Bila shaka Okwi, Niyonzima na Kiiza. Twite na Kavumbangu watafute timu nyingine
 
simba matatizo walijitakia wenyewe kumpa huyu bwana uongozi.... mahakama ilishamthibitisha ni mwizi na ikamtia hatiani na kumfunga akatoka kwa msamaha wa rais sio kwa kukata rufaa meaning hadhi ya kwamba yeye ni mwizi bado anayo..... na lilikua kosa la wizi sasa nyie simba leo mkiibiwa mtashangaa!!!
 
Back
Top Bottom