Rage: Nini okwi, sasa namleta suarez toka liverpool

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Wanachama na wapenzi wa Simba SC wamekuwa kama watoto wadogo wa kuahidiwa mambo makubwa na mwenyekiti wao Aden Rage, Mbunge Tabora Mjini - CCM. Hali hii imesababisha ugumu hata wa kumng'oa madarakani kila anapovurunda. Ameifanya Timu ya Simba kupoteza dira na kuwa timu kituko na kupoteza heshima yake barani Africa.

Baada ya Emanuel Okwi kusajiliwa na Yanga, mashabiki wa Simba wamepandwa na hasira ikiwa ni pamoja na kutaka kwenda nyumbani kwa Rage, lakini wanachama hawa watarajie majibu mepesi kabisa toka kwa Mwenyekiti wao ikiwa ni pamoja na kuwatuliza kuwa atamsajili LUIS SUAREZ anaewika Liverpool, nini Okwi. Kwa ahadi hii atawaweza mashabiki wa Simba, watambeba juu, watasukuma gari lake na watarejea makwao wakishangilia kuwa SUAREZ anasajiliwa Simba, wimbi la Okwi litasahaulika.

Aina ya Viongozi kama Rage ndio waliotawala Tanzania katika medani ya Siasa. Rage huyu ndiye aliyewarubuni wapigakura wa Tabora mpaka wakampa Ubunge. Je, CCM imekuwa chama cha kuzalisha walaghai badala ya kukomboa wanyonge? Maana viongozi wengi wa CCM wamekuwa wakiongea bila kujua wanayoyasema. Walianza kuwalaghai "Maisha bora kwa kila mtanzania" na wakapewa kura. Wengine wakasema marufuku Serikali kununua Mashangingi lakini ndo kwanza yanazidi kununuliwa.

Cha kushangaza zaidi, bado watanzania wengi wamekuwa wakiwashangilia viongozi aina ya kina RAGE na wenzake ndani ya CCM.
 
yanga hua wanaiga ksajili toka simba sijui huwa hawana uwezo wa kuspot talents wenyewe
 
Huyu Mheshimiwa aachie ngazi atuache na club yetu. Hamna cha maana anachofanya zaidi ya kuishushia hadhi timu makini ya Simba. Atumie muda wake kwenye siasa au mambo mengine ila klabuni hatumtaki kama kiongozi. Yanga wanatudhihaki sana siku hizi. Tunazongwa na kupigwa masingi kila kona ya mji na nchi hii. Go away.
 
Ni kweli mkuu, Rage ni mhuni wa kutupwa. Sijui kwa nini Simba hata tulimuamini. Hafai hata kuwa mwanachama. Lkn anatuendesha kama walevi. Ila hili la Okwi kazi anayo.
 
Wanachama na wapenzi wa Simba SC wamekuwa kama watoto wadogo wa kuahidiwa mambo makubwa na mwenyekiti wao Aden Rage, Mbunge Tabora Mjini - CCM. Hali hii imesababisha ugumu hata wa kumng'oa madarakani kila anapovurunda. Ameifanya Timu ya Simba kupoteza dira na kuwa timu kituko na kupoteza heshima yake barani Africa.

Baada ya Emanuel Okwi kusajiliwa na Yanga, mashabiki wa Simba wamepandwa na hasira ikiwa ni pamoja na kutaka kwenda nyumbani kwa Rage, lakini wanachama hawa watarajie majibu mepesi kabisa toka kwa Mwenyekiti wao ikiwa ni pamoja na kuwatuliza kuwa atamsajili LUIS SUAREZ anaewika Liverpool, nini Okwi. Kwa ahadi hii atawaweza mashabiki wa Simba, watambeba juu, watasukuma gari lake na watarejea makwao wakishangilia kuwa SUAREZ anasajiliwa Simba, wimbi la Okwi litasahaulika.

Aina ya Viongozi kama Rage ndio waliotawala Tanzania katika medani ya Siasa. Rage huyu ndiye aliyewarubuni wapigakura wa Tabora mpaka wakampa Ubunge. Je, CCM imekuwa chama cha kuzalisha walaghai badala ya kukomboa wanyonge? Maana viongozi wengi wa CCM wamekuwa wakiongea bila kujua wanayoyasema. Walianza kuwalaghai "Maisha bora kwa kila mtanzania" na wakapewa kura. Wengine wakasema marufuku Serikali kununua Mashangingi lakini ndo kwanza yanazidi kununuliwa.

Cha kushangaza zaidi, bado watanzania wengi wamekuwa wakiwashangilia viongozi aina ya kina RAGE na wenzake ndani ya CCM.

Mkuu mimi siyo mwanachama wa Simba ila ni Timu ninayoipenda kwadhati.Tatizo la simba siyo Rage ni Wanachama ambao mambo wanayoyafanya yanasababisha viongozi kuwadharau na kuwadhalilisha kiasi hicho.Wakati wa vikao hawawi serious kabisa mtu utakuta anawaburuta wao wamekaa wanakodoa macho tu....hii ndo changamoto kubwa sana kwa Klabu hii...Hata akiondoka Rage atakaye kuja nihaya haya Timu hizi zinaendeshwa kwa mfumo mbovu usioweza kuleta matunda na kuendana na Teknolojia za Kisasa.

Hata hao wachezaji wanaogombaniwa ni full Kichehesho.Huyo Okwi tumemuona kwenye Challange...alaikuwa na ubora gani kumzidi Nagasa au Samatta .Shida ni uzuzu wa wanachama wakijirekebisha na kuchagua viongozi bora Klabu za Yanga na Simba zinaweza zikawa Klabu tajiri kabisa Afrika.
 
Wanachama na wapenzi wa Simba SC wamekuwa kama watoto wadogo wa kuahidiwa mambo makubwa na mwenyekiti wao Aden Rage, Mbunge Tabora Mjini - CCM. Hali hii imesababisha ugumu hata wa kumng'oa madarakani kila anapovurunda. Ameifanya Timu ya Simba kupoteza dira na kuwa timu kituko na kupoteza heshima yake barani Africa.

Baada ya Emanuel Okwi kusajiliwa na Yanga, mashabiki wa Simba wamepandwa na hasira ikiwa ni pamoja na kutaka kwenda nyumbani kwa Rage, lakini wanachama hawa watarajie majibu mepesi kabisa toka kwa Mwenyekiti wao ikiwa ni pamoja na kuwatuliza kuwa atamsajili LUIS SUAREZ anaewika Liverpool, nini Okwi. Kwa ahadi hii atawaweza mashabiki wa Simba, watambeba juu, watasukuma gari lake na watarejea makwao wakishangilia kuwa SUAREZ anasajiliwa Simba, wimbi la Okwi litasahaulika.

Aina ya Viongozi kama Rage ndio waliotawala Tanzania katika medani ya Siasa. Rage huyu ndiye aliyewarubuni wapigakura wa Tabora mpaka wakampa Ubunge. Je, CCM imekuwa chama cha kuzalisha walaghai badala ya kukomboa wanyonge? Maana viongozi wengi wa CCM wamekuwa wakiongea bila kujua wanayoyasema. Walianza kuwalaghai "Maisha bora kwa kila mtanzania" na wakapewa kura. Wengine wakasema marufuku Serikali kununua Mashangingi lakini ndo kwanza yanazidi kununuliwa.

Cha kushangaza zaidi, bado watanzania wengi wamekuwa wakiwashangilia viongozi aina ya kina RAGE na wenzake ndani ya CCM.

Kwanza tutake radhi! sidhani kama kuna mwanachama, mshabiki na mpenzi wa simba anafurahia kinacho endelea..lakini kuhusu swala la Suarez kumbe ni mtazamo wako tu kwamba atakuja na majibu ya hovyo kama alivyonukuliwa kwamba anaenda london kula kuku..Yanga wamekosea kumchukua Okwi, wangemsajili Rage kabisa! ..kuna mambo yanaudhi sana aixee!..soka la bongo ukifuatilia kwa makini unaweza ukawa MGONJWA WAZIMU!
 
RAGE, RAGE ,RAGE ni mtu mwenye record chafu za kupindukia Rage huyo huyo eti anapokelewa kwa maandamano na wanachama wa SimbaJKNA tena eti akitokea VIP rounge, Rage huyo huyo wanayamwezi wa Tabora wanadamka asubuhi kufoleni kumchagua eti awe mbunge wao.

Rage enzi za Nyerere alikuwa hakatishi katika cheo chochote cha kisiasa, ndio maana Mzee Mandela walivyoonana na Nyerere huko ahera alimtarifu kwamba Rage sasa hivi ndio mbunge wa Taboara mjini eneo la shule ulikosoma, nasikia Mzee Nyerere aliguna tu akasema hata RAGEE
 
Rage nni kifua kikuu! Anajifanya msomi kumbe mwivi, namkumbuka Mzee wangu Hassan Dalali...alikaa Simba 10 years tulikuwa na raha sana, wakaja hawa wachumia tumbo wakasema eti arasa la 7 yule, katiba haimruhusu kugombea uenyekiti! Swali, JE, YULE DARASA LA 7, NA huyu degree za kubandika nani zaidi?
 
Mnahangaika saana, ni rahisi tu
Yanga = CCM
Rage = CCM
Manji = CCM
Final results
Rage = Manji
Rage = Yanga
 
Jamani moderator hii kitu wekeni kule kwa michezo. Kuna wapenzi wengi wa kuijadili ambao sio wa huku. Wa huku jukwaa la siasa wakiitaka tutaifuata huko.
 
ISMAIL ADEN RAGE haaminiki na wala hajawahi kuaminika ,aliwahi kufungwa jela kwa wizi wa mipira pale FAT , nimewadharau sana waliomchagua kwenye ubunge na kwenye uongozi wa club yetu .
 
mtajua na mamipira yenu kwetu pwani tunashabikia taarabu tu basi hakuna presha wala nini.
 
Jamani moderator hii kitu wekeni kule kwa michezo. Kuna wapenzi wengi wa kuijadili ambao sio wa huku. Wa huku jukwaa la siasa wakiitaka tutaifuata huko.
mjomba ulikuwemo kwenye ule mgao wa fedha za OKWI kutoka TUNISIA ?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom