Mjomba wa taifa
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 231
- 161
Wanachama na wapenzi wa Simba SC wamekuwa kama watoto wadogo wa kuahidiwa mambo makubwa na mwenyekiti wao Aden Rage, Mbunge Tabora Mjini - CCM. Hali hii imesababisha ugumu hata wa kumng'oa madarakani kila anapovurunda. Ameifanya Timu ya Simba kupoteza dira na kuwa timu kituko na kupoteza heshima yake barani Africa.
Baada ya Emanuel Okwi kusajiliwa na Yanga, mashabiki wa Simba wamepandwa na hasira ikiwa ni pamoja na kutaka kwenda nyumbani kwa Rage, lakini wanachama hawa watarajie majibu mepesi kabisa toka kwa Mwenyekiti wao ikiwa ni pamoja na kuwatuliza kuwa atamsajili LUIS SUAREZ anaewika Liverpool, nini Okwi. Kwa ahadi hii atawaweza mashabiki wa Simba, watambeba juu, watasukuma gari lake na watarejea makwao wakishangilia kuwa SUAREZ anasajiliwa Simba, wimbi la Okwi litasahaulika.
Aina ya Viongozi kama Rage ndio waliotawala Tanzania katika medani ya Siasa. Rage huyu ndiye aliyewarubuni wapigakura wa Tabora mpaka wakampa Ubunge. Je, CCM imekuwa chama cha kuzalisha walaghai badala ya kukomboa wanyonge? Maana viongozi wengi wa CCM wamekuwa wakiongea bila kujua wanayoyasema. Walianza kuwalaghai "Maisha bora kwa kila mtanzania" na wakapewa kura. Wengine wakasema marufuku Serikali kununua Mashangingi lakini ndo kwanza yanazidi kununuliwa.
Cha kushangaza zaidi, bado watanzania wengi wamekuwa wakiwashangilia viongozi aina ya kina RAGE na wenzake ndani ya CCM.