Rage: Nchi hii tunaitafuna wenyewe, mwishoni tutatafunana wenyewe

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Mwenyekiti wa Club ya Simba na Mbunge wa Tabora Mjini anasema Nchi hii tunaitafuna wenyewe siku tukiimaliza tutafunana wenyewe. Anashangazwa na utajiri wa Wafanyakazi wa Serikali kumilki Geust House Ishirini [20] ukimuuliza chanzo cha mapato ya ujenzi wa miradi hiyo nini hana cha kukupa?

Mfanyakazi wa Serikali anamiki mali kupita Mfanyabiashara.Rage anasema kama Misri na Libya raia wa Nchi hizo wametaifisha Mali za Marais hao,je sisi mbona hatutaifishi mali za watu wanaotuibia mali zetu kama mchezo wa kuuzwa kwa UDA.

Jamani Rage kafunguka kama sio Rage yule wa zama zile za Ndolanga!!!!!Kumbe kifaa.

Nawsilisha.
 
Mwenyekiti wa Club ya Simba na Mbunge wa Tabora Mjini anasema Nchi hii tunaitafuna wenyewe siku tukiimaliza tutafunana wenyewe.

Ana maana kwamba wao, pamoja na yeye, wanaitafuna nchi na watakapoimaliza wataanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe kama ilivyo desturi ya manyang'au mzoga unapokwisha. Na kweli kuna dalili mafisadi wameanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe, shuhudia sakata la fisadi Simba na fisadi Kusena, na bado. Chama cha Mafisadi karibu kinasambaratika !
 
ccm bye bye sendeka kishasema dalili zote za kufa na wamekua mafisi kwa sasa wanagawana chochote kilichopo
 
kifo cha ccm

Sipendi Kife natamani waendelee kuwa chama kizima kisha nao waje wapitie hatua ambazo vyama vingine vimepitia kisha kutoka hapo kitakuwa chama makini tofauti na sasa kuwa ni chama kikongwe badala ya kuwa chama makini.Tena hawaoni aibu kila siku majigambo yao uwa ni chama kikongwe badala ya kuwa na misemao kama chama bora,chama cha kisayansi,au chama cha kizarendo nk.

Kutokana na kuwa na Watu wazee wengi kinakosa vijana wanaofikilia kukifanya kionekana cha kileo zaidina chenye vijana damu zinachemka.Vijana wote waliomakini wakikisogelea chama hicho wanapigwa vita matokeo yake kimekomaa kwa kuchukua vijana wazuri kwenye mambo yetu yale.......!!!!!!!!!!!. Wakati wanatakiwa kuwa na vijana wanosoma dunia hii inavyokwenda kwa kasi wajuzi wa kubuni mbinu na mikakati ya kisasa na kuibua majibu ya haraka dhidi ya Wananchi.

Na kuwa chama ambacho ni chepesi kukabiliana na ukweli kuliko kuupinga kwa kunyamazisha.Kwani kwa kunyamazisha unajenga utando wa Muda mfupi na utakapo kuja kufumua kutakuwa na usaa na mwanzo wa kuwa na kidonda uozo kufuata.

Kitendo cha mwenyekiti kiti cha Spika kuzuia Bunge lisiandike hassard ya Mbunge wa Ludewa Furukunjombe dhidi ya maneno yake ya kuwa Wataandamana na ushauri wake kwa Serikali kuwa ni vyema ikawa na mfumo wa kuwanyonga viongozi haswa mawaziri wanaoshindwa kuwajibika ipasavyo.Nimeona ni UJINGA ULIOPITILIZA kusema maneno aliyoyasema mbunge huyo yasiandikwe kwenye hansarrd.

Ni kuwanyima vizazi vijavyo ufahamu wa kujua kiwango cha mchango wa wabunge wao wa miaka iliyopita yaani kipindi kijacho.
 
Mwenyekiti wa Club ya Simba na Mbunge wa Tabora Mjini anasema Nchi hii tunaitafuna wenyewe siku tukiimaliza tutafunana wenyewe. Anashangazwa na utajiri wa Wafanyakazi wa Serikali kumilki Geust House Ishirini [20] ukimuuliza chanzo cha mapato ya ujenzi wa miradi hiyo nini hana cha kukupa?

Mfanyakazi wa Serikali anamiki mali kupita Mfanyabiashara.Rage anasema kama Misri na Libya raia wa Nchi hizo wametaifisha Mali za Marais hao,je sisi mbona hatutaifishi mali za watu wanaotuibia mali zetu kama mchezo wa kuuzwa kwa UDA.

Jamani Rage kafunguka kama sio Rage yule wa zama zile za Ndolanga!!!!!Kumbe kifaa.

Nawsilisha.

CCM watakuwa wamekuwa "Unleashed" na maboss wao CC, kuwa mchezo wanaoufanya wa kutetea uozo si mzuri kwa masilahi na uhai wa chama kama kweli wanataka support ya wananchi. Watakuwa wameambiwa "Attack" japo ni kinafiki, na unajua what next when that command comes from the owner.
 
Labda baada ya kuota joto la JIWE; Kuwa Jela anajua maradhi yake...
 
Mwenyekiti wa Club ya Simba na Mbunge wa Tabora Mjini anasema Nchi hii tunaitafuna wenyewe siku tukiimaliza tutafunana wenyewe. Anashangazwa na utajiri wa Wafanyakazi wa Serikali kumilki Geust House Ishirini [20] ukimuuliza chanzo cha mapato ya ujenzi wa miradi hiyo nini hana cha kukupa?

Mfanyakazi wa Serikali anamiki mali kupita Mfanyabiashara.Rage anasema kama Misri na Libya raia wa Nchi hizo wametaifisha Mali za Marais hao,je sisi mbona hatutaifishi mali za watu wanaotuibia mali zetu kama mchezo wa kuuzwa kwa UDA.

Jamani Rage kafunguka kama sio Rage yule wa zama zile za Ndolanga!!!!!Kumbe kifaa.

Nawsilisha.

Wanaona upepo wa kizazi cha dot com unawajia inabidi wabadilike. Ndio leo anayajua hayo? Au amesahau ufisadi wake FAT na kwengineko? Kizazi hiki kinachokuja ni vigumu kwa kiongozi kukubalika kama hana moyo wa uzalendo.
 
yaaaaaaaaaaah naona katika picha hiyo hiyo unayoiona wewe na sio devil advocate kama wengine wanavyoona.Wamejua kuwa kumbe ukiwa mkweli [Mzalendo] wananchi watakuchukua kwa namna yoyote kama ilivyokuwa kwa shibuda.
 
Buriani Ccm kwaheri ya kuonana waasisi walishatangulia nenda nenda nenda Ccm msalimu Mwalimu na Kawawa vipi Muungano huko vipi?Kolimba mlimdhulumu atawapokea tuu vizuri.
 
jamani waombeeni wakae pembeni waone nao jahazi likiwa la endeshwa na nahodha mwingine linaendaje.Tuwaombee wapate nao nafsi ya kuwa wapinzani waone wengine nao wanaendeshaje Mashua wao wakiwa abiria na chama kingine wakiwa manahodha.
 
Nilimsikia Ragea jana akiongea kwa masikitiko makubwa na kwa kweli ameongea yale ambayo yako mioyoni mwa watanzania wengi. Tamaa ya viongozi wetu (baadhi) itakuja kuleta machafuko yasiyo na sababu kwa watu kujichukulia sheria mkononi. Lakini lingine ninaloliona kwamba ni hatari, ni uwezekano wa wananchi kudharau hata vyombo vyetu vya dola baada ya kubaini kwamba viko kwa ajili ya kushughulika na petty offenders huku wale wanaoleta madhara ya kweli kwa umma wakiwa huru na wakifurahia matunda ya udhalimu na ufedhuli wao. Mungu tuepushe na janga hili!
 
Ukiwa mwizi na ukitaka kuonekana wewe siyo mwizi basi wananchi wakifukuza wezi wenzio na wewe unga msafara tena uwe yule anaewasha kibiriti kuwachoma moto. Utaonekana unachukua sana wizi.
 
Haha ahaha ahaha!!!!! Mbopo bana!!!!!!!!!!!!! hapo kwenye baadhi tunaanza kumuengua JK kwanza siyo?
 
Ukiwa mwizi na ukitaka kuonekana wewe siyo mwizi basi wananchi wakifukuza wezi wenzio na wewe unga msafara tena uwe yule anaewasha kibiriti kuwachoma moto. Utaonekana unachukua sana wizi.

Itakuwa nzuri sana ukiwa mwizi ukashiriki kumsulubu mwizi mwenzio,uzuri wake ukiwa wakikujua kuwa nawe ni wale wale watamsurubu vibaya kuliko mwzi walieshriki nae kumsurubu.Kwa kuwa wataona ule msemo wao wa kiswahili kikulacho ki nguoni mwako ndio umepata mahali pake.
 
Rage anajaribu kuelezea habari ambazo karibia viongozi wote wa serikali ndio tabia zao pamoja na yeye!
Walivyoitafuna FAT yeye na kina Ndolanga
 
Back
Top Bottom