Rage nae atoa mkataba aliosaini Yondani simba mwaka jana 23-December, 2011. Kazi ipo jamani.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rage nae atoa mkataba aliosaini Yondani simba mwaka jana 23-December, 2011. Kazi ipo jamani..

Discussion in 'Sports' started by mzee wa njaa, Jun 7, 2012.

 1. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  . mkataba wa yondani simba.jpg rage.jpg mkataba wa yondani simba.jpg

  Huo ndio mkataba wa Yondani alionguka wakati anaichezea Simba mnamo mwaka jana.....Na huku madeni ya maharage akionesha picha iliyotolewa na baadhi ya mitandao ya kwamba Yanga wamemsainisha Yondani jana usiku. Sasa hawa Yanga wamemsainisha Yondani mwaka jana mwezi wa 11 au jana usiku?

  Jamani nani mkweli hapo?
   
 2. Mdomo wa Mamba

  Mdomo wa Mamba Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndiyo ubaya wa wachezaji ambao hawajaenda shule. Hapo Yanga ni lazima ikubali kuingia gharama ya kuvunja mkataba.
   
 3. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amesema Klabu ya Yanga inajidanganya kumsainisha Kelvin Yondani kwani ni Mchezaji wa Simba halali kwa kuwa ana mkataba na Klabu Hiyo ya Msimbazi Hivyo Yanga walichofanya ni kuwafurahisha Mashabiki wao katika kuelekea Uchaguzi wa Klabu hiyo ya Jangwani.Huku akiwa ameshika Picha inayomuonyesha Mchezaji huuyo akisaini huku Mabunda ya Pesa yako mbele yake anasema Yanga hilo ni changa la macho.

  Mie na wewe tukae na tuone nini kitafuata baada ya hapo katika ulimwengu huu wa soka la Bongo ambapo mauzauza haya yalishawahi tokea miaka ya tisini Je yanarudi teena ?

  TAARIFA YA KLABU YA SIMBA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Simba Sports club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patric Yondani kwa kuzungumza naye na baadae kwa ushahidi wa picha kuonekana wakimuandikisha makaratasi ambayo baadae imeripotiwa na vyombo vya Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young Africans.
  Kwamba katika picha hiyo ameonekana mjumbe wa Young aliyejiuzuru bwana Seif Ahmed na hilo lilitoa shaka kama utaratibu huo umefanywa na klabu ya Young, lakini shaka hiyo imeondolewa pale ambapo tovuti ya Young imetangaza kumsajili mchezaji huyo wa Simba SC, lakini zaidi ya hilo picha inaonyesha fedha zikiwa zimewekwa mbele ya mchezaji jambo linaloonyesha mazingira ya kurubuniwa kwani kwa utaratibu wa kifedha, pesa nyingi kiasi hicho malipo yake yanashauriwa/yanapashwa kupitia benki.
  Mbali ya hayo picha hiyo inamuonyesha Kelvin akiwa katika jezi ya mazoezi ya timu ya Taifa na yenye logo ya Kilimanjaro na kumbukumbu zinaonyesha mkataba kati ya TBL na TFF tarehe 9/5/2012, kwa haraka haraka tukio hilo limefanyika katika kipindi chini ya mwezi mmoja ingawa taarifa za ushahidi zinaonyesha tukio hilo limetokea jana tarehe 6/6/2012.
  Simba Sports Club ilipenda kuamini kwamba tukio hilo haliihusu klabu ya Young kwani bwana Seif Ahmed alishajiuzuru kutoka kwenye kamati ya Young Africans, kwani Young ni klabu kongwe na inayojua taratibu zote za usajili.
  Kwamba Simba Sports Club imeshawasiliana na jopo lake la mawakili na inajiandaa kuishtaki klabu ya Young katika chombo husika cha mpira na kudai adhabu ya kutopitisha majina yote ya usajili ya Young kwa mwaka 2012/2013 na miaka mingine miwili ijayo na Simba SC ipo tiyari kufuatilia suala hili hadi katika mahakama ya mpira ya FIFA.
  Kelvin Yondani ni mchezaji halali wa Simba Sc aliye na mkataba hadi 31 mei 2014 mkataba ulioongezwa tarehe 23/12/2011 kuundeleza mkataba wa awali uliokuwa unaisha tarehe 31/5/2012. Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati mmoja.

  Imetolewa leo tarehe 7/6/2012.
  MH. ISMAIL ADEN RAGE (MB)
  MWENYEKITI
  SIMBA SPORTS CLUB
   
 4. T

  TUMY JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanzoni nilimuungana mkono Yondani katika suala hili, nikiamini hakuwa amesaini simba tena na niliposikia anapewa mil 30 ila kuona mktaba wa simba ukionyesha amelipwa mil 25 basi huo ni ulimbukeni na hizo ni tamaa sasa.Kama alikuwa anataka kwenda yanga hakuwa nasababu ya kusaini tena simba ila kuna haja ya vilabu vya tanzania kubadilika, wewe unaacha mkataba wa mchezaji hadi unabaki mwezi 1 ndio unamuita mezani,wabadilike mpira ni biashara kubwa
   
 5. S

  SNAKE HOUSE Member

  #5
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina shaka na mjelajela huyo..........bila shaka analeta za kijelajela !
   
 6. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Rage kabla hajaendelea kuongea arudishe hela zilizompeleka jela za tff
   
 7. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Hahahahahaha!na yeye si nasikia kaomba kwenda yanga ili awe msemaji?
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,290
  Likes Received: 19,438
  Trophy Points: 280
  jina lako haliendani na wewe
   
 9. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Mbona hamna sahihi ya YONDANI hapo wala dole gumba?
   
Loading...