RAGE awanyang'anya vifaa vya muziki bendi ya Sensema Malunde | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAGE awanyang'anya vifaa vya muziki bendi ya Sensema Malunde

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mjukuu wa bibi Pili., Dec 24, 2011.

 1. Mjukuu wa bibi Pili.

  Mjukuu wa bibi Pili. Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa jimbo la Tabora mjini Ismail Aden Rage amechukua vyombo vya muziki vilivyokuwa vikitumiwa na bendi ya sensema malunde ya mkoani humo hali iliyopelekea bendi hiyo kusitisha kufanya maonesho kwa wiki tatu sasa.

  Wakizungumza na gazeti hili viongozi wa bendi hiyo kwa sharti la kutotajwa majina walisema hatua hiyo ya Rage imewasikitisha sana na ina lengo la kuivuruga na kuiua bendi yao.

  Walisema mapema mwaka jana kabla ya uchaguzi mkuu uliohusisha wabunge,madiwani na rais,Rage aliufuata uongozi wa bendi ya Sensema Malunde akawaeleza kuwa atanunua na kuleta vyombo vya muziki vipya kwa ajili kufanya matamasha pamoja na kushiriki katika kampeni za uchaguzi za chama cha mapinduzi.

  Aidha walieleza kuwa mbali na makubaliano hayo pia walikubaliana baada ya vyombo hivyo kuanza kutumika asilimia 80 ya mapato yatakwenda kwa mmiliki ambaye ni Rage na asilimia 20 itabaki kwa viongozi.

  Walisema makubaliano mengine ni pamoja na kulipa mishahara ya wanamuziki na vyombo vya bendi vya zamani viwekwe ndani.

  Wameongeza kuwa baada ya vyombo hivyo kuwasili,kazi ilianza mara moja ikiwemo upigaji katika kumbi mbalimbali za burudani katika mji wa Tabora na vitongoji vyake.

  Aidha wamebainisha zaidi kuwa pamoja muziki kupigwa kwenye kumbi mbalimbali za burudani pia bendi hiyo ilikuwa ikifanya kampeni zake za ubunge.

  Wanasema hali ilianza kuwa mbaya mwanzoni mwa mwaka huu,ambapo hadi kufikia mwezi machi mwaka huu wanamuziki walianza kusotea mishahara yao na ndiyo ukawa mwisho wa na mparaganyiko wa bendi.

  Walisema Rage alichukua vyombo vyake vya muziki,na kuvifungia ndani na baadhi ya wanamuziki amewahamishia jijini Da-es-Salaam kutokana na tetesi kuwa anataka kuanzisha bendi yake huko.

  Mwisho-
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 6,027
  Trophy Points: 280
  Mijitu mingine bwana! Hivi walitegemea nini kutoka kwa wanasiasa wa aina ya jamaa. Au niwaulize kivingine, hivi kondomu ikishatumika huwa inafanywaje? Siasa za kimagamba ndivyo zilivyo. Next time watie adabu badala ya kudangaywa kama mitoto midogo kwa njaa zao.
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wakome na ujinga wao! sasa c mwenye mali kachukua? alishawatumia hana haja nao tena!
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160

  Naunga mkono hoja!
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,290
  Likes Received: 19,438
  Trophy Points: 280
  ana mguu wa kuku yule waambieni kabisa
   
 6. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Ameamua kuwavua gamba, wasubiri 2015
   
 7. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #7
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Ati huyu anawakilisha Umma..Jizi nyonyaji kubwa hili
  Hata hivyo Matatizo yanayotokana na Ujinga ,Huelimisha!
   
 8. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  hahahaaaa...!!. Mkuu umenifurahisha sana. Mia
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Akisimama jukwaani anasema ataleta maendeleo na kutengeneza fursa za ajira kwa wanajimbo lake!!lol!!aibu sana!ataibuka na kusema walikuwa hawampi pesa zake....
   
 10. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wajinga hao, kwanini hawakuandikiana mkataba? haya ni mambo ya kawaida sana kwenye biashara, partners wanafarakana na kampuni huvunjika. cha msingi ni makubaliano ya mkataba kabla ya kuanza biashara ambayo hupelekwa mahakamani na kila upande kupewa haki yake. "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" asema BWANA
   
 11. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Wasubirie 2015 watakapoitwa kwa sasa kibarua kimeota majani waende wakafyeke nyasi huko Dar. Msomali Rage amepata alichokuwa anakitafuta. 2015 watume cv zao mapema kwa Magamba :lol:
   
 12. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,183
  Trophy Points: 280
  Wasubiri 2014 atawarudishia
   
 13. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Wajinga ndio waliwao.
   
 14. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hakuna mbunge wa Tabora mjini anayekaa zaidi ya muhula mmoja; hivyo jamaa[ Al shabab] anajua 2015 hatarudi mjengoni ndio maana anawafanyizia hao wanamuziki!
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  preach preach
   
 16. Ondio Osio

  Ondio Osio Member

  #16
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 11, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana kwani walikua hawalijui hilo next time wajifunze.
   
 17. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,128
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Jela imemuathiri huyo! Bado ana akili ya Mfungwa.
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wajinga ndio waliwao... 2015 march atawarudishia, watamvika na uchifu, 2016 machi atawanyanganya watatuma mtu tena jf, 2020 april atafanya tena

  siwaonei huruma waliomuamini mtu ambaye alishawahi kufungwa jela kwa masuala ya kukosa uaminifu
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yawezekana walimmega
   
 20. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #20
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Dah! Mambo ya "mguu wa kuku" tena? Cool! This is as old school as it can get dude! Lol!
   
Loading...