Rage apigwa faini kwa kwenda na silaha mkutanoni

Aisee,
jamaa wanatania maana adhabu ya ukiukwaji namna ile ni mgombea kuondolewa ktk kinyang'anyiro.
Hapa tujadili namna NEC inavyovunja sheria na kanuni ilizojiwekea.

Angelikuwa mikononi mwa PAW wangekula ban ya kutogombea chaguzi tatu


Tuwaombe watalaamu wetu watujuze kuhusu hili maana liko wazi kabisa!
 
kweli maandiko yaliposema rushwa hupofusha macho haikukosea, sasa huyu jamaa, na hiyo adhabu waliyotoa wanategemea kuwa na mvuto kwa wananchi? sishangai lakini kwani kuna aliyeua kwa risasi akaambiwa alipe laki mbili!
 
Mzee Mwanakijiji alileta hoja hapa kuwa yawezekana Tanzania kama nchi haina wanasheria na inawezekana kwa maana kuna ushahidi mkubwa wa kusupport haya madai. Na sasa nimeona anakuja na hoja nyingine juu ya nchi kutokuwa na engineers (akitathmini juu ya ajali zinatotokea kila siku) na mwisho huenda tukasikia na doctors (kufuatana na watu wengi kutibiwa nje)!

My point ni kuwa 'Mh' Adeni Rage alifungwa jera lakini alivyomaliza kifungo akakata rufaa ili ionekane alionewa (nadani) na akasafishwa ili agombee ubunge. Cha ajabu alipogombea (tena Tabora mjini na sio vijijini) wakampa kura! Inasikitisha!!!!
Ni katika muendelezo huo huo haya mambo yanatokea kuwa "eti alipe Sh. 100,000/- kama faini!

Wasiwasi wangu tuangalie kama nchi tusije kufika sehemu au wakati, badala ya kutokuwa na doctors, engineers, lawyers nk, watasema kuwa "Tanzania hakuna watu"!
Tuwaombe watalaamu wetu watujuze kuhusu hili maana liko wazi kabisa!
 
Tanzania kuna sheria za wana CCM ambazo ni tofauti na za watu wa vyama vingine au raia wa kawaida. Ila CCM hiyo hiyo ni chama kikumbatiacho maharamia na wahalifu. Kwangu mimi Rage ni muhalifu toka enzi ziile za CDA hadi FAT.
 
tatizo wanasiasa wetu hawajui kuwa wanatakiwa kutumia nguvu za kiakili na utashi katika kuwa fanya wao wa heat katika siasa na sio kutumia silaha za moto hizi hapa sio mahali pake hoja na point nzito zilitakiwa kuwani silaha za viongozi wetu lkn kwasababu ni empty head ndo maana hawaishi kwenda na mapanga na pistol bado kutembea na vifaru tu.
 
sheria za tz hazifuniki watu wote kwa usawa. hawezi kufunguliwa mashtaka,yeye ni wa chama tawala. sijui tuelimishweje tuelewe. kama wa chadema ama cuf ndo angebebwa juu juu na kuchaniwa bukta kabisa!
kwa Mbunge laki moja ni kama kunywa chai gharama yake..........................nilifikiri hilo ni kosa la jinai ambalo polisi walipaswa walishughulikie kama wanavyoshughulikia kosa la kuvuliwa hijabi DC wa ccm..............................

yaelekea kuna sheria za wanaccm na sheria za wengineo..................
 
Mzani wetu wa sheria ulishapindaga siku nyingi, unahitaji calibration...sijui ndio mpaka 2015!!
 
Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini (ccm) Aden Rage ameamliwa kulipa faini ya kiasi cha shilingi za kitanzania,150,000/= na Tume ya maadili ya uchaguzi mdogo wa Igunga, kwa kosa la kupanda jukwaani huku akiwa na Bastola kinyume cha sheria, ilihali yeye sio askari polisi.

Source: Radio one.
Angekuwa ni wa Chadema nahisi wangemkamata siku ya Ijumaa ili atoke jumatatu, then angeburuzwa mahakamani kwasababu lazima kingepatikana kifungu cha kumtia hatiani, hili suala lingechukua mda mrefu kidogo mahakamani ili ku-disturb mchango wake kwenye kampeni.
 
kweli ccm kina viongozi makapi ndiyo maana ushindi wao kila mara unahojiwa kwani wanambinu za kipumbavu sana..........MI NILIDHANI ATANYANG'ANYWA SILAHA NA KUPIGWA NDANI ANGALAU MIEZI MITANO NA KUAMRIWA KUTOHUDHURIA AU KUPIGA KAMPENI KWA MUDA WA MIAKA 20..................."HII NDO CCM VIONGOZI WAKE WASHAMBA"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom