Rage apigwa faini kwa kwenda na silaha mkutanoni

Kama ni laki tu J'1 nitatia timu na gobole langu kwenye mkutano wao wa kufunga kampeni najua siku hiyo green gadi lazima aanzishe valangati wakinishika nawapa laki mbili moja ya faini na nyingine ya usumbufu.
 
Mbunge wa Tabora "Aden Rage" ametozwa faini ya sh. Laki moja kwa kosa la kupanda na silaa jukwaani siku chache zilizopita, hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya maadili huko Igunga bw. Protas Magayane. Lakini pia mwenyekiti huyo amesema kamati yake imetoa karipio kali la maandishi dhidi ya CDM kuhusu vurugu ikidai kupokea malalamiko toka chama cha mapinduzi CCM

Source: TBC Habari saa 2, 28/09/2011

Hiyo faini ni yakuwapumbaza wananchi
 
Aisee,
jamaa wanatania maana adhabu ya ukiukwaji namna ile ni mgombea kuondolewa ktk kinyang'anyiro.
Hapa tujadili namna NEC inavyovunja sheria na kanuni ilizojiwekea.

Angelikuwa mikononi mwa PAW wangekula ban ya kutogombea chaguzi tatu

 
Tena hiyo ni danganya toto ,wala senti tano hatoi,sana sana yeye ndo atapewa,na anakula posho ndefu.Niliwahi kuuliza yule OCD aliepigwa kule Maswa kuna hatua iliyochukuliwa?hata huyu isingewezekana kufanywa lolote,CCM iko juu ya sheria na kweli wapinzani wasithubutu kuiga hayo,CDM silaha yetu ni nguvu ya umma
 
Yuko wapi kilaza Nape alieandika kwenye ukurasa wake wa fcbk kuwa hakuna ttzo kwa mtu kupanda na bastola jukwaani,kweli ccm masaburi yao haifanyi kazi kabisa vilaza tupu

Wengi wa wana CCM akili zlishakuwa na ganzi kwa sababu ya mfumo ganzamizi. Hivi watanzania wangapi wana silaha nchini na bado huwa hatuwaoni kutembea nazo? Je, tukiwa tunatembea na silaha viunoni hadharani kweli tutafika huko tuendako kama Taifa? Sasa utaona huyo huyo Nape amepewa cheo hasa kwa njia ya uteuzi afanye maamuzi yanayohusu jamii. Kama kweli alisema hayo kwenye facebook yake, basi tatizo lipo kubwa nchini kwetu. Nakumbuka huyu bwana ni Mkuu wa Wilaya pia, ambapo, mkuu wa wilaya huwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya. Ndiyo hivi kweli?
 
CDM wamepewa onyo kali baada CCM kulalamika lakini majuzi CUF walilalamika kuhusu wafuasi wa CCM kumpiga kada wao mbona nao hawajapewa onyo kali la maandishi? CDM walilalamika CCM kuchoma bendera na kuvamiwa na green guard lakini sijaona karipio kali.
 
ccm imeshika hatamu,kuzivua inahitaji network ya kama egypt,determination ya kama libya,na usongo kama waarabu wa palestina.sasa jiulize watz tuanze kivipi 2015
 
Yuko wapi kilaza Nape alieandika kwenye ukurasa wake wa fcbk kuwa hakuna ttzo kwa mtu kupanda na bastola jukwaani,kweli ccm masaburi yao haifanyi kazi kabisa vilaza tupu
Nepi hana jipya alishawahi andika kwamva CDM wanampeleka M/KITI kwenye uchaguzi wa igunga,sasa anaona aibu cos magamba wamepeleka baraza la mawaziri huko igunga,nepi anatakiwa afikili kabla ya kutenda au kusema
 

Angelikuwa mikononi mwa PAW wangekula ban ya kutogombea chaguzi tatu

Ingesomeka hivi je? rejao, mwita25 na ritz wametozwa faini ya laki moja kila mmoja ili wasipigwe ban na matola, crashwise na feedback wamepewa karipio kali na PAW.
Vipi kama ingekuwa hivyo? nadhani mitusi ambayo ingefumuka humu JF, ingekuwa balaa hata kufungua mtandao tusingethubutu.
 
Kamati ya maadili imempiga faini tsh 100000/ kwa kosa la kwenda na silaha kwenye mikutano ya kampeni

kwa Mbunge laki moja ni kama kunywa chai gharama yake..........................nilifikiri hilo ni kosa la jinai ambalo polisi walipaswa walishughulikie kama wanavyoshughulikia kosa la kuvuliwa hijabi DC wa ccm..............................

yaelekea kuna sheria za wanaccm na sheria za wengineo..................
 
Hiyo faini ni hela yangu ya kula bata kwa dk 30 nikiwa na mademu zangu pale Rose Garden, Dodoma. Kwakweli sikubaliani na hiyo faini.
 
Kama ni laki tu J'1 nitatia timu na gobole langu kwenye mkutano wao wa kufunga kampeni najua siku hiyo green gadi lazima aanzishe valangati wakinishika nawapa laki mbili moja ya faini na nyingine ya usumbufu.

Mkuu hiyo ya usumbufu nitakuchangia!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom