Rafiki yangu na Rais wangu wa TFF Karia kwa yanayoendelea Uwanja wa Songea nimekusamehe ila Kosa hili lisije likajirudia tena

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,874
Nimetoka Kumsikia Msimamizi Mkuu wa Uwanja wa Maji Maji huko Songea (Mkoani Ruvuma) utakaotumika katika Nusu Fainali ya ASFC Kesho kati ya Azam FC na Simba SC nimebaki Kusikitika na hata Kukasirika pia.

Ukweli ni kwamba hadi GENTAMYCINE naandika Uzi huu hivi sasa Uwanja upo tayari kwa 75% hadi 85% tu huku Magoli yakiwa bado hayajichimbia vizuri na Cement, Nyasi zenyewe haziko imara, Majukwaa yapo yenye 'Kreki' na huko Vyooni ndiyo balaa na huenda Kesho Mashabiki wakishikwa na Haja Kubwa basi wakanyeana tu Vichwani mwao.

Rais wa TFF Wallace Karia leo sitaki Kukusema (Kukusiliba) ukizingatia Wewe pia ni mwana Msimbazi Mwenzangu 'lia lia' ila Msimu ujao Nusu Fainali hizi za Fainali mzipangie katika Viwanjani vizuri ama hapa Dar es Salaam au kule Kisiwani Zanzibar.

Ninakutakia Ushindi mwewa hapo TFF.
 
wanaharibu hii michuano kwa kulazimishwa mechi zipelekwe kwenye viwanja vibovu, ni bora wangefata taratibu za kuruhusu kila mwenye uwanja aombe nafasi vikaguliwe na vile bora vipewe.
 
Huo uwanja wa Majimaji ni mbovu karibu mwaka wa tano sasa. Sijui kwa nini walishindwa kuufanyia ukarabati.

Kitu pekee nilichokipenda ni huu utaratibu wa kupeleka mechi kubwa kwenye Mikoa isiyokuwa na Timu za ligi kuu. Mashabiki wanapata hamasa kubwa sana ya kuziona timu zao

Mama amekubali hivi viwanja viwekewe nyasi bandia, hivyo huu uwanja wa Majimaji ni vizuri ukakumbukwa ikiwa ni pamoja na marekebisho ya vyoo na majukwaa.
 
Back
Top Bottom