Rafiki yangu mpendwa amemuoa kipenzi changu wa sekondari

Pole sn mkuu ila nna iman ulishapata mwenza na una familia tayari,.
Cpati pcha baada ya kumcmulia rafk ako khs ulvyokis na zubeda cjui atakua alimpga au alimnunia jomoniii, ulimsababishia mararizo
Maisha yanamengi swahiba siku ile baada ya kuupata ukweli nilikunywa bia nyingi.Nililia sana mapenzi yanaumiza moyo nikakumbuka jinsi nilivyokuwa ninampenda Zubeda wangu lakini haikuwa ridhiki sikulala hata kidogo.Siku iliyofuata niliondoka nikiwa ninalia huku naendesha gari yangu kuelekea mjini Lindi nikiwa nasikiliza wimbo wa bushoke "kama ulikuwa hutaki kuishi nami bora ungesema mapemaaa" nimewakumbuka kwa kuwa alikuwa nimpendae na rafiki wa utoto wangu.
 
Zubeda atakuwa aliumia sana baada ya kujua mambo yako yashakuwa safi halafu yeye bado yuko kilage anasugua gaga
 
Ulitaka aMuoe wa
Tulimaliza wote shule ya msingi pale majengo Nachingwea. Mimi na rafiki yangu hakika tulishibana na mungu akatujaalia tukafaulu Nachingwea day. Tukiwa form one nikapendana kwa dhati na bibie Zubeda, hakika tulipendana na rafiki yangu mpendwa alimuheshimu na kumjali. Wakati wa kurudi shule niliwapakia mpenzi wangu Zubeda na kwenye kitako alikaa rafiki yangu mpendwa.

Mwaka 1999 nilihamishwa shule nikahamia Ndanda sec hapa nikalazimika kuishi mbali na Zubeda daah hakika ilikuwa ni machungu mnoo. Nilimuaga rafiki yangu akae vizuri na nitakuja kila likizo kumuona Zubeda na rafiki yangu.Tuliendelea kuwasiliana kwa barua na kuonana hadi tulipomaliza shule 2001.

Nikasota na maisha ya ulimwengu na hatimae nikapata kazi mwaka 2003 na mwaka uliofuata nikatembelea nachingwea nikiwa nafuraha tele kwenda kumuona Zubeda tena nikiwa niko vizuri kama kijana nipo na gari ndogo corolla ae100. Nikaonana na Zubeda akalia sana kwani muda ulipita hatukuonana nikamuuliza kama ameshaolewa akanijibu hapana.

Tulifurahi tukaagana kwa miadi ya kuonana siku inayofuata. Siku ya pili nilianza kumtafuta rafiki yangu mpendwa tangu shule ili nimsalimie na nimpe michapo ya jana yake nilivyokutana na Zubeda na makiss tuliyofanya.

Nikaonana naye tukafurahi nikamuuliza kama ameshaoa akanijibu amemzalisha tuu mwanamke mmoja na kwa sasa yupo tuu. Nikaanza kumuhadithia juu ya nilivyokutana na Zubeda tulivyokiss na mambo mengi tuliyoahidiana lakini niliona kwa mbali rafiki yangu akiwa amebadilika na macho yakimuiva na kuwa mekundu basi nikawa sielewi nini kimemsibu nikaaga nikaelekea zangu bar moja hivi inaitwa the ganners.

Nikafika bar nikapiga moja moto na moja baridi baadae nataka kutoka nikaitwa jina langu kugeuka heee classmate wangu kasidi basi tukakumbushiana story za shule nikamwambia sasa ninamchuma na naelekea kwa miadi nikakutane na Zubeda. Kasidi alishangaa na akaniambia Zubeda amekwisha olewa na rafiki yangu mpendwa ambaye muda mfupi uliopita nimetoka kuongea nae akawa anawiva macho kwa story zangu kuhusu Zubeda.

Nimehadithia hii kwa kuwa muda umepita na nimewakumbuka sana rafiki yangu pamoja na Zubeda nawatakia waishi salama.
Vidududuu
 
Bonge LA gwege ww hukupaswa uwe mwanaume


Mwanaume huwa hana upuuzi Wa kumwekeza mtu yeyote kwa kina mahusiano mwanaume huwa tunasema kifupi tu huyo bado wangu

Hadith za kumweleza mtu mapenzi ni za wanawake na si wanaume


Ww bado akili yako changa sana
 
Back
Top Bottom