Rafiki yangu kalala kituoni siku mbili kwa kosa la kumpiga mumewe na kumvunja mkono

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,257
Wakuu, marafiki wengine sio kabisa huyo ni shost yangu wa ukweli tangu muda tu, ila mi nimeshindwa tabia yake ya kipigo japo ni mtafutaji mzuri sana kwa kweli.

Mimi nipo safarini kwa sasa nikapata meseji kutoka Kwa rafiki yangu mmoja kuwa 'una habari Ninja yupo kituoni siku mbili sasa' nikamwambia Hapana kwa kweli. Nikauliza kisa naambiwa alimpiga tena mumewe maana ni kawaida yake huyo baba kupata kipondo Kutoka kwa ninja.

Watu wamekataa kwenda kumuwekea mdhamana, sasa huko baadhi ya watu wamenipigia wanasemaa ninja anaomba sana jembe Lake nipigiwe (yani mimi) nirudi nikamuwekee mdhamana.

Huyo baba ni mpole mno na ni Msukuma lakini Ninja yeye ni mchaga.

Mimi namuonea huruma huyo mkaka wa watu maana anasema anaogopa mwanamke akitoka huko atakuja kumuua.

Nishaurini nikamuwekee au niuchune mimi.
 
Mwanaume inaonekana alipenda weupe wa kaskazini acha adundwe na atadundwa sana.
Mpaka nimekumbuka clip fulani jamaa alikuwa anamkanya kijana wake kuwa asimletee mparestina kwake.​
Kadada kako vizuri na ni katafutaji sana tu.
 
Back
Top Bottom