Rafiki yangu anataka nifanye tendo la ndoa na mkewe!

kijana gazeti mwambie rafki yako awe kama michael jackson, akamchukue mpaka hosp then wakampandikizie mbegu za watu wasiowafahamu then atazaa vzr kuliko wewe kuhusika, mke wa mtu sumu kaka kama hauamini jaribu then utaniambia, michael jackson hakuwa na mtoto, wote walikuwa wa kupandikiza, kama unampenda rafki yako, na unakiri kuwa n rafki yako wa ukweli mshauri atumie njia ya kupandikiza au wewe toa mbegu hosp then zikapandikizwe kwa uyo bibie kuliko wewe kulala na mke wa rafki yako, umenielewa? au ndo unamtaman mke wa rafki yako? umenielewa?
 
Ni jambo ambalo ameomba liwe siri sijui kama itakuwa siri tena nikileta hivyo
vipimo hapa, hata hivyo mimi sijaviona hivyo vipimo!

Hilo jambo dogo sana tu yakhe, wote watatu nendeni mkamwone doktor achukue damu yako ya mke wa rafiki yako vichanganywe kwenye chupa kicha arudishiwe mke wa rafiki yako mambo yamekamilika. Huhitaji kupoteza nguvu na kutoka jasho na pengi njie hii itakusaidia kutoathirika kisaikolojia ya kujamihiana.
 
Ni wiki ya pili sasa toka nipate ombi hilo kutoka kwa rafiki yangu wa karibu sana.
Hilo limekuja baada ya kupata uthibitisho wa vipimo vya kitaalamu kutoka Hospitali
Kuwa hana uwezo wa kupata mtoto katika maisha yake. Hivyo anaomba nifanye
hivyo kwa mkewe ili apate mtoto. Naomba mnishauri juu ya jambo hili kwani nimempa
jibu moja tu kuwa avute subira nitafakari. Pia amenieleza kuwa hilo jambo wamejadili
na mkewe na wameshakubaliana.

Naomba ushauri wenu waungwana!

MUOGOPE MUNGU NA TUNZA HESHIMA YA URAFIKI WENU. Kama yupo tayari kuwa na mtoto ambaye si wakuzaa yeye mwenyewe ni bora aende aka adopt, mshauri hivyo na mwambie asifanye mambo kwa ajili ya kuwapendezesha binadamu kuwa ana uwezo wa kuzaa bali amfurahishe Muumba wake. Mwambie kuwa mkewe si nduguye itafika siku watatofautiana na mkewe na kila kila kitu kitakuwa hadharani.
 
ni vigumu kuamini hili hasa kama hujawahi kulisikia ila lipo hili kabisa hata mimi nimesha wahi kuliona
 
If u r both fit medically and he and wife gat no issues and u won't want the kid, go ahead! Its an honor to be asked
 
sijasoma comments za watu wengi,bt kama issue ni sperm donation, agha khan wanafanya artificial insermination. unatoa sperms ww (baada ya kupimwa afya yako, japo hata kama una hiv inawezekana pia kuzitenga mbegu na kusiwe na maambukizi). hizo sperms zinapandikizwa kwa kifaa maalum kwa mke wa rafikiyo. huhitaji kufanya nae tendo la ndoa!
 
there goes another very usefull advise. japokua umeongea kitu cha muhimu sana: mkewe si nduguye. je haki ya huyo mama kupata mtoto iko wapi? ukumbuke kuwa teknolojia inabadilika,huenda jamaa akapata matibabu ya kumfanya apate mtoto 20 yrs to come, wakati huo mkewe yuko 50 yrs na hawezi kuzaa tena! na ushasema si nduguye,so atajichukulia dogodogo na kuzaa. umenipa wazo kuwa ushauri huu ni typical wa kimfumo dume. angekua mwanamke ndo hawezi kuzaa,ungetoa ushauri wa ku-adopt? sorry,i am just thinking aloud from another angle
MUOGOPE MUNGU NA TUNZA HESHIMA YA URAFIKI WENU. Kama yupo tayari kuwa na mtoto ambaye si wakuzaa yeye mwenyewe ni bora aende aka adopt, mshauri hivyo na mwambie asifanye mambo kwa ajili ya kuwapendezesha binadamu kuwa ana uwezo wa kuzaa bali amfurahishe Muumba wake. Mwambie kuwa mkewe si nduguye itafika siku watatofautiana na mkewe na kila kila kitu kitakuwa hadharani.
 
Ndugu yangu sikushauri ufanye kitu kama hicho kwa sababu ni kitu kibaya na cha kukudhalilisha wewe na mkeo na pia kumdahlilisha huyo rafiki yako na mkewe pia! Kama wanandoa hao wana upendo wa kweli sifdhani kama wanaweza kukubaliana kufanya hivyo. Kama imefikia wamekaa pamoja na kukubaliana hayo nahisi inawezekana kukawa hakuna upendo wa kweli ndani yao.
Ushauri wangu ni kama kweli vipimo vinaonyesha kuwa jamaa hataweza kamwe kuzaa, naungana na hao waliyopendekeza yafuaatayo...

- Mkewe apate sperm donation
- Mshauri aka-adopt mtoto/watoto
- Kama ni mtu mwenye imani, akawaone wazee wa maombi wakamuombee

tafakari ..... chukua hatua ....
 
there goes another very usefull advise. japokua umeongea kitu cha muhimu sana: mkewe si nduguye. je haki ya huyo mama kupata mtoto iko wapi? ukumbuke kuwa teknolojia inabadilika,huenda jamaa akapata matibabu ya kumfanya apate mtoto 20 yrs to come, wakati huo mkewe yuko 50 yrs na hawezi kuzaa tena! na ushasema si nduguye,so atajichukulia dogodogo na kuzaa. umenipa wazo kuwa ushauri huu ni typical wa kimfumo dume. angekua mwanamke ndo hawezi kuzaa,ungetoa ushauri wa ku-adopt? sorry,i am just thinking aloud from another angle

Be honest, huyo jamaa angekuwa mtoto wako wa kuzaa na akaja kwako akakueleza mawazo yake, je wewe kama mama ungekubaliana na wazo kuwa amtafute mwanaume mwingine alale na mkewe ili aweze kupata wa(m)toto? Si suala la mfumo dume, bali ni suala la feasibility, justifiability, practicality and acceptability in our living society kuwa mwanaume ambaye mkewe hawezi kuzaa kabisa aweza kupata wa(m)too either kwakuoa mwanamke mwingine au kwakuzaa nje ya ndoa lakini mwanamke ambaye mwanaume wake hawezi kuzaa si rahisi kufanya kile ambacho mwanamume angefanya. Najua kina mama mnatetea sana haki zenu lkn mtambue kuwa it doesn't holds in all circumstances, kwa hiyo si suala la mfumo dume ni suala la nature of tradition of the business. Nafahamu kwamba mnaumia sana juu ya hili lakini ndivyo hali halisi ilivyo. Naomna hapa nimeusisitiza mfumo dume.....
 
kama vipi badilishaneni, wewe kwa vile tayari una watoto mpe mkeo na wewe chukua mke wake, kwa vile unaambiwa huelewi, naona unapepo la ngono.
 
Mkuu hiyo na dalili kuwa majaribu yako mengi kwako na unatakiwa kuwa makini sana upon your decisions. Usijaribu hata siku moja kufanya mapenzi na mke wa mtu. Hakuna ujamaa katika tendo la ndoa. mwambie kuwa; imani yangu hainiruhusu kufanya hivyo, amtafute mtu mwingine. because, ukianza tu kulala na mke wake na akijua, huo wivu alionao kwa mkewe unaweza kukuletea matatizo makubwa. Labda kama ww ni play boy is ok.
 
Najaribu kuvuta kumbukumbu ya hii sinema.

Nlishawahi kuiona kipindi flani. Jina lake nimelisahau kidogo.

Katika ulimwengu wa kawaida kabisa. Hata majogoo yasiyo na akili hayawezi kufanya utumbo kama huu. Sembuse binadamu mwenye akili na utashi............ Sinema nyingine watu hata hawajui kuzitunga zikaleta kauhalisia japo kwa asilimia kumi. khaa!

Imagine eti mke na mme wamekaa na kukubaliana mke akamegwe na rafiki ya mme.......kisa mtoto! Can't swallow this!
 
Hivi imekuwaje hili suala ambalo ni la kweli kwa 100% linashindwa
kuaminika. Vyovyo mtu atakavyosema lakini sina jinsi ya kukanusha
jambo hili isipokuwa nasisitiza tena na tena kuwa ni kweli imetokea
100% kama kuna filamu inafanana na tukio hili narudia tena sijawahi
kuiona hiyo filamu.
Nasisitiza tena na tena TUKIO HILI SI LA KUBUNI!
Ukitaka ijadiliwe vizuri ipeleke facebook kule. Kuna vijana wa sekondari na primary, hadithi kama hizi wanazipenda sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom