Rafiki yangu anataka kulipiza kisasi kwa mtu anayetembea na mke wake

Prof Decentman

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
276
140
Nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi leo. Ameniambia jambo limeniuma sana. Kanieleza rafiki yake anatembea na mke wake. Mara nyingi amekuwa akisafiri na hapo ndipo mke wake anatoka na jamaa.

Amenieleza anajua cha kumfanya mke wake ili alipize kisasi sasa anajiuliza amfanye nini huyo rafiki yake ambaye amemuumiza?

Mimi nilimshauri asamehe lakini kasema amejaribu ameshindwa. Kwa kweli haya mambo ni mazito.

NB:
Wanaume wenye tabia ya kutembea na wake za watu muache maana maumivu mnayosabisha kwa wanaume wenzenu ni makubwa mno.
 
Kusamehe na kujitafakari wewe kwanza kama haumridhishi au kunamigogoro baina yao ni hatua nzuri ya mwanzo lakini cha mwisho kama anaamua kuachana nae ni vizuri aachane kwa wema maana atapata anayempenda wakaishi kwa furaha na amani mwisho akate mazoea na baradhuli huyo
 
hahahaha... hii kesi kama naifaham ...muulize baada ya kumpiga simuliitisha kikao cha wazazi wa pande zote mbili? pili nasikia umeamua kuwa chapombe na ulikuwa hunywi pombe?
 
Mwambie aache huo ujinga kabisa,hapo ni mtu kaamua kutumia mali zake so ye atulie na atafute namna ya kuachana nae huyoo
 
Atapata faida gani kwa kufanya hivyo. Anaiga upumbavu,anaweza akawa mpumbavu zaidi. Anayecheka mwisho, hucheka sana.
 
Back
Top Bottom