Rafiki yangu amekuwa tajiri mkubwa Dodoma, ninafuata njia zake. Tuzifuate

Johnny Impact

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
2,723
2,000
Hiyo biashara unayotaka kufanya ishapitwa na wakati. Pesa haipatikani kirahisi namna hiyo.
Nenda kibwaigwa, fanya research, onana na huyo jamaa akupe mbinu alizotumia. Kisha fanya biashara wewe km wew kwa msaada tu wa jamaa, lbd anaweza kuunganisha na wakulima.
Naku PM Mkuu na Mimi uniwekezee milioni 30 kwa huyo jamaa yAko...please please...aisee..au nikuone wapi!?
 

Mubarridi

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
22,188
2,000
"Kama unataka mali,utaipata shambani".

Hii kauli tunaipata katika kitabu fulani hivi (Jina limenitoka) cha Kiswahili.
 

Latvia

JF-Expert Member
May 2, 2019
352
1,000
Nimeanza kukuelewa, kuwa huenda mke wake ndio anachangia hayo.
Ishawahi kutokea kwa Mtu wa karibu, poleni Sana. Huyo kurudi kwenye muombe Mungu tu, hapo kishaachana na nyie. Sometimes wanawake sio kabisa
Thanks mkuu nimekuelewa.

Baasi kutokana na mafanikio yake kwen kilimo ndio maana nakuunga mkono ufanye hiyo business, bro ana heka 1000+ kwa msimu anapiga kama 350+M.
We kuwa tu makini na matapeli. All the best.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
24,518
2,000
Hana akili huyo mwaka.juzi 2019 mwishoni yalifika hadi 20000 kwa debe, na hiyo ni Bei nzuri Sana .
Uko sahihi.

Na wengi tulitarajia atatapisha godown lake kipindi hicho badala yake akasema kwa muda ameyatunza anataka kufidia na hizo gharama
 

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,046
2,000
Thanks mkuu nimekuelewa.

Baasi kutokana na mafanikio yake kwen kilimo ndio maana nakuunga mkono ufanye hiyo business, bro ana heka 1000+ kwa msimu anapiga kama 350+M.
We kuwa tu makini na matapeli. All the best.
Kulima hapana, kulangua YES
 

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
3,955
2,000
Huu uzi wengi wanaupinga ila kuna rafiki yangu kipindi hicho alipata pesa nyingi sana pale, alikua anapeleka mzigo Kenya baadae mpaka ukafungwa ndo akapata hasara
 

dawa yenu

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
2,690
2,000
Mkuu nenda na kiteto kule mashamba ni makubwa na ni bei rahisi hayana thaman unaweza kupata shamba heka 20 kwa 500,000/= (laki tano tu) mahindi yanakubali sana na kupalilia watu wanapalilia heka 1 kwa tsh10k tu hivyo hivyo nq kuvuna.
Kwenye heka moja unaweza kupata had gunia 9 na gunia moja ni 45,000/=
Ukivuna heka 20 una uhakika wa 8M kama mambo yataenda vizuri
Huku wewe ukiwa umewekeza Sana sana 600k .
Mimi nimepata bahat ya kupata shamba heka 20 kwa laki mbili tu
(Nenda mwenyewe kafanya utafiti kama una nia kule pesa ipo na mvua ni nying tofaut kdogo na dodoma )
Yaani ulime heka 20 kwa laki sita?
 

MKIBAIGWA

Senior Member
May 25, 2017
165
500
Anything is possible.mm kibaigwa napajua sana biashara karibia zote.
Labda sijaelewa biashara yenu lakini kwamba biashara ya mahindi ununue malori mmmmh hapo nina Mashaka.

Wafanyabiashara wakubwa wa mahindi kibaigwa wanapeleka unga Zanzibar na faida ni ndogo sana.

Kenya wanapeleka wenyewe wakenya wanakuja kununua sokoni.Kwa mtanzania kupeleke Kenya ni ngumu kulingana na masharti ya wizara.

Mkuu nakushauri fuatilia hizo hela zako ni ngumu sana mtu kumaliza chuo 2018 ajue biashara ya kibaigwa Kwa mda mfupi.pale kibaigwa watu wanatapeliwa,wakenya wamelizwa sana (sijaamaanisha jamaako tapeli).

Kingine ambacho kinatakiwa kikushtue ni faida aliyokutajia yaani kutoka mil 25 hadi 60mil ni parefu sana.

Watu wanaopiga hela kidogo kibaigwa niwale wanaoweka stoo kina Gwajima wamejenga godowns lakini bado hawapati faida uliotaja.

Biasahara ya mahindi nimefanya tangu miaka 2005.

Take care
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom