Rafiki yangu alitaka Tufe, Dereva wa Lorry akakubaliana naye, Mungu akamtumia Dereva mwingine Kutuokoa

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Mwaka jana Oktoba ni mwaka ambao kumbukumbu yake inanijia sana. Leo nimekumbuka zaidi baada ya kuonana ma Dereva mmoja anaitwa Richard.

Siku hiyo nilikuwa na gari yangu kubwa ni ya Diesel Manual ina Speed 240. Tumetoka Dar na jamaa yangu tunaelekea Dom. Huku kote nlikuwa naendesha mimi mpaka tumevuka Morogoro tunaelekea Kibaigwa kama sikosei.

Jamaa akaomba naye asukume ile mashine. Muda mrefu alikuwa akitamani sana jinsi navyokanyaga mashine,navyopiga mpini n.k akaona ni kitu chepesi na cha kuenjoy sana.

Mimi ni kweli na enjoy kuendesha gari hasa Manual. Akaomba naye akanyoshe nyoshe miguu. Akachukua mashine. Kiukweli jamaa hakuwa amezoea sana Manual ila alikuwa mbishi. Nlimwona anavyochelewa kuingiza gear, anavyoshindwa kurudi vizuri n.k

Nikamwambia kama inamsumbua anirudishie tu akasema hapana akiendesha kama dk 20 zaidi atakuwa master.

Tabu ilianza tumefika mitaa flani mbele yetu kuna truck yenye Trailer. Jamaa akaomba. Mwenye truck akamruhusu. But my friend akawa anajivuta sana ku overtake. Akiwa anataka kutoka mwenye truck akamkataza jamaa akawasha taa ya kulia.

Jamaa hakuelewa. Nikamwona kashaingia kulia kakanyaga accelerator. But kaingia halafu katika kubadili gear kacheka. So ikabidi atoe macho mbele aangalie anaingiza wapi gear.(asome namba).

Kule mbele tulisikia truck inapiga horn imewasha taa....imetoka speed ile mbaya. Speed hasa.jamaa kitete hatuwezi ingia kushoto sababu kuna truck ya jamaa tupo nayo usawa wa nyuma ya cabin na ina trailers zile zinakuwa iliyounganishwa na cabin na nyingine yake.

Jamaa yetu wa kushoto alishajua huu msalama. Akakamata brake tuliona gari yake tairi zikiburuza na kuchora alama barabarani huku gari ikilalamika sana. Ile ndo ilikuwa nafasi yetu finyu jamaa yangu akaingia kushoto kwa sentimita chache sana tulikoswa na lile gari la mbele yetu.halikuhangaika hata kusimama.

Sisi tuliingua kushoto jamaa akayumba na gari hivyo hivyo mpaka mbele tukasimama. Nikashuka haraka kumsimamisha jamaa wa truck ambaye alikuwa nyuma yetu.

Jamaa akaenda simama. Richard ni mmoja ya madereva wenye upendo sijawahi ona. Alishuka akitupa pole na kutuonea huruma. Mimi nlimwomba msamaha na kumshukuru sana kwa kitendo chake. Haraka nikatoa 70,000 mfukoni kumpa kama asante. Aligoma kuchukua kabisa.

Tukabadilishana namba za simu. Ilibidi gari nichukue kuendesha mimi. Tuliendelea kuwasiliana mpaka leo nmekutana naye Hospital akiwa anahangaika kumtibia mama yake. Hana Bima. Nimemsadia nlichoweza nikawasiliana na yule jamaa yangu naye ajipige pige. Tumeweza mchangia tsh 330,000 aongezee.

Jamaa ameshukuru hadi kutokwa na machozi. The man is very humble. Sijawahi ona madereva wastaarabu kama huyu jamaa.

Ndugu zangu tutendeni tu wema. Malipo tumwachie Mungu. Hulipa kwa wakati wake. Jamaa yangu since then hana hamu tena ya kuendesha manual. Ilikuwa atuue sote. Maana tungegongana uso kwa uso na truck ya mafuta. Uso kwa uso.
 
Mwaka jana Oktoba ni mwaka ambao kumbukumbu yake inanijia sana. Leo nmekumbuka zaidi baada ya kuonana ma Dereva mmoja anaitwa Richard...
ni madereva wachache ambao wanaweza kupambana kumuokoa mtu na ajali ili Hali anajua hata yy anajihatalisha,big up Richard.lakini pia Richard anafaa kuwa dereva ndani ya ikulu.anajua kuendesha lakini pia kuokoa.
 
Wema ni akiba ambayo haiozi,hadi leo hii wapo raia wenzetu ambao ni waungwana sana.Siku nyingine acha kufanya majaribio ambayo yanaweza kugharimu uhai wako na wengine.Ulipaswa kumsimamisha haraka ulivyomuona huyo rafiki yako haeleweki katika uendeshaji.
 
Mwaka jana Oktoba ni mwaka ambao kumbukumbu yake inanijia sana. Leo nmekumbuka zaidi baada ya kuonana ma Dereva mmoja anaitwa Richard...
Kati ya vitu ambavyo hupaswi kabisa hata kuwaza kumuazimisha mtu ni gari na mke!! .... Hivi unaanzaje kumwazima mtu gari lako aendeshe hata kama unajua kuwa ana leseni? Magari yanatofautiana na uzoefu hali kadhalika!.

Gari ambalo hujawahi kuliendesha unahitaji kulifanyia mazoezi kwanza ili ulizoee kabla hujaliingiza barabarani....Hii iwe fundisho kwa wamiliki wa magari, kuwa hayaazimishwi kama ilivyo kwa mke/mume wa ndoa.
 
Mwaka jana Oktoba ni mwaka ambao kumbukumbu yake inanijia sana. Leo nmekumbuka zaidi baada ya kuonana ma Dereva mmoja anaitwa Richard...
Stor ya kusisimua sanaa big up Sana.

Binafsi nimejifunza kitu kupitia hiki kisa cha kusisimua.

Mm napenda sanaa kudrive lakn linavyokuja swala la kiusalama ni bora yule mwenye uzoefu especially kwenye maswala ya safari mrefu apewe nafasi yakee.

Mungu ni wetu sote na pia kongole kwa bwana richard hili ni funzo kila mmoja kwa nafasi yakee haijalishi upo wapi kikubwa ni kuendeleze tu kutenda wema.
 
Back
Top Bottom