Rafiki yako amenisaliti na kuzaa nje...

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,432
2,892
Kuna mtihani umenijia nashindwa kuutatua.

Nimepata mashtaka toka kwa mke wa rafiki yangu. Ni kwamba jamaa amezaa na mwanamke mwingine nje ya ndoa. Na huko inaelekea ametekwa haswaa... Maana hata mapenzi sasa yamepungua ndani ya familia.

Jamaa nikimtafuta nimuelekeze anapotezea. Kiufupi hataki mawasiliano na mimi. Shem ameomba niongee na Mumewe lakini jamaa ananikwepa. Shem ameumia na anatamani kuliwazwa lakini brother muda hana.

Hebu msaada kidogo hapa tafadhali, tusije kuingia kwenye mitego ya shetani.
 
Umesikiliza upande mmoja ,Stori yako haina mzani. Jamuhuri ya muungano imekupa onyo next time Utalipa fine.
 
na wewe pia ukumbuke ni mwanaume kama yeye hivyo unavyojaribu kumshauri uhakikishe uko makini sana usije ukaharibu zaidi
 
Tumechelewa Sana Ndugu Zangu
Hayo Ni Mambo Madogo Sana Yanazungumzika
Muhimu Jitahidi Sana Usiingie Kwa Ndani
Mambo Ya Unyumba Yana Siri Nzito Sana
Unaweza Kuonekana Mbaya
 
Chai ! Kama kweli wewe ni Shem basi ungejua hata huyo mchepuko ni nani na ungekuwa na ABC zote za jamaa yako na kwanini anayumbisha familia
 
Mwambie maisha mafupi haya

Kila mtu ana kifanyio chake

Na yeye atafute liwazo lake afaidi kifanyio chake
 
Kesi za ndoa waga ni ngumu sana huwa zna ntoa jasho any way ukbahatika kuonana na huyo mdau msstize abalance upendo kote kote asije
 
Sasa kama mtoto keshazaliwa..wewe unataka kumshauri nin huyo jamaa ako?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom