Rafiki wa mkeo Rafiki wa Mmeo ni wakuwaheshimu siku zote

naima79

Senior Member
Feb 27, 2009
186
195
Nipelekee kule chumban kwenu MMU, mimi nilikua na mtu wangu tunapendana sana tumekaa mwaka na nusu hapo alikua yuko Tanga me morogoro akahamia dar kikazi na mimi nikapata kazii dar tukapendana sana akaja akajitambulisha akatoa posa bahat nzuri akatakiwa aende darfur kikazi kwaio tukasimamisha taratibu za ndoa alipokua darfur alikua ananitumia sana hela nimjengeee

Nilijenga na alikua annamshirikisha mama ake kwa sababu mama alikua mgonjwa sasa nilikua nasimamia vitu mimi sasa wkt mwanaume yuko huko kuna dda anaitwa(name withheld maana hamtabiriki kama speech za Magu) tuko nae kwa grupu tulijuana kwa sababu kuna siku walipost ile unakaa wapi umjue jirani yako tukajikuta mimi na dda N tunakaa karibu mtaa mmoja
Siku akaja mitaa hii akanitafuta nikaenda kuonana nae tukapiga story mpaka tukawa marafiki nakumbuka alikua na mume anampiga sana mwanaume mlevi basi kuna siku kaja kwangu saa nane usiku anatoka damu kwa kipigo basi nikampokea nilimpeleka hospital akapona wakajja wakaachana maana hawakuoana

Sasa mwanaume akarudi from darfur mambo yakaendelea akatoa mahari vikao vikaanza november mwaka huu Ila niliumwa sana miguu ilikua inajaa maji, inavimba nikahangaika mpaka kwenye maombi ikapona sijakaa sawa bleed nableed mpaka nazimia madaktar wamepima hamna kitu nikaponea kwa mwamposa, sasa Mungu mkubwa siku mama mmoja muuza genge akaniita akasema mwanangu ukiendeleea ushoga na flan tutakuzika huyo dada ndo zake imekua kasumba mtaani alipokua anaishi ni mchawi na wanaume zote aliowai kuishi nao walikua wa mashoga zake lakin dawa zikiisha wanampigagaa kama mbwa

Nilianza kuona labda kweli ila nikachunguza kwa kuuliza nikapata maajibu hayo hayo sasa wakat najiuliza nifanyeje nikakuta msg kwa mwanaume yaan kumbe wameshaanzisha mahusiano sasa kingine nilichoambiwa mumewake wa mwisho alikua ameathirika nikambana mwanaume akakubali kua aliteleza sijui nilikua naumwa tangu arudi hatujakutana nilimfuata yule dada nikamsema na nikasema nikiumwa hata mafua ndugu zangu watamuua sasa nikamsamehe mwanaume ila nikasema tukapime, mwanaume yuko positive yaan kaathirika

Nikamwambia aliekuambukiza ni flan me na ww basi tena mama wa mwanaume amelia kama mtoto mwanaume ni askari alimfuata Dada shoga akampigaaaaaaaaaaa sasa shoga kahama mtaani.

Onyo: ukimwi upo kuweni makini, hapa ni kwa Neema tu mpaka rafiki huyu ameponyoka kuupata
 

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,154
2,000
Pole sana dada. Mungu amekuepusha na mengi.
Mungu ni wa kumuomba atupe marafiki wazuri..na kipind cha kuelekea katika harus hua kunakua na mambo mengi sana ni vema mwanamke na mwanaaume muwe mnaomba pamoja au kila mmoja kumuombea Mwenzie, believe me it helps sana
 

Simara

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
5,037
2,000
Pole sana kwa huyo kaka, wanawake tujifunze rafiki wa kweli ni ndugu zako tu dunia imeharibika...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom