Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Ni vyema kufanya kazi na watu unaowaamini.
Rais John Magufuli amekuwa akinukuliwa mara nyingi akilalamika kuwa watendaji anaowateua wanamuangusha. Kuna wakati mpaka akahoji au hamjanielewa bado ninachokitaka?
Leo ninapoona amemteua tena rafiki yake wa muda mrefu katika nafasi nyeti ya kiutendaji Wizara ya Mambo ya Ndani, ambayo ni juzi tu alikiri ndio Wizara inayompa wakati mgumu kuliko wizara zote, basi inatoa picha kwamba anamuamini mno Christopher Kadio.
Kabla ya uteuzi huu, C. Kadio alikuwa RAS wa Mkoa wa Mwanza.
Kwa wasiomfahamu: Christopher Kadio ni yule anayeonekana akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais Magufuli ndani ya maabara wakifanya practical ya Kemia, enzi wakiwa wanasoma.
Ndugu Kadio. Usimuangushe mheshimiwa Rais. Nenda ukafanye kazi kwa uadilifu na kuzingatia sheria. Weka urafiki pembeni.